Liverpool imeiumbua E.P.L , sio ligi ngumu kama tulivyoaminishwa

"ambapo juve anachukua kwa miaka kama 7 mfululizo hili jambo ni nadra kutokea hata kwenye zile farmers leagues" . sijaelewa hapo kwenye farmers leagues ni ligi ya wakulima au wafanyakazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Mada aliipost jamaa Fulani kwenye group la what's app nikamuelimisha mwisho alinielewa nashangaa amekuja tena kupost huku.!!
Twende kwenye facts, Liverpool ni team iliyo kwenye kiwango bora kwa sasa maana kwa msimu uliopita ilimaliza ligi na points 97 point moja nyuma ya aliyekuwa bingwa man cty ambaye alikuwa na point 98.!
Msimu huo wa 2018/2019 Liverpool ilitwaa mataji matatu makubwa duniani yani
CL
Super cup na
FIFA World Club champions
Hakuna team inayotamani kucheza na Liverpool kwa sasa duniani.
Wachambuzi uchwara walisema kwa Liverpool ile kushindwa kutwaa epl msimu wa 2018/19 basi hawatatwaa tena kwa miaka ya karibuni Leo wapo wapi??
Wachambuzi uchwara walisema ngoja ifike Dec,na katikati ya Jan Liverpool watachemsha Leo wako wapi??
Wachambuzi uchwara walisema man cty ina kikosi kipana unaweza ukatoa vikosi vitatu Leo wako wapi??wachambuzi uchwara walisema ngoja Mane aumie team itapoteana Mane kaumia na bado team inashinda sasa wamekuja na epl ni ligi mbovu na sio ngumu Kama tunavyoaminishwa!!
Leo hii mashabiki wa man u, Chelsea,arsenal wanaacha kuangalia ubovu wa team zao wanakuja na propaganda wa ligi sio ngumu je isingekuwa ngumu wao wangekuwa na point 30?????????
Acheni uchambuzi uchwara Liverpool ipo kwenye kiwango bora sana kwa sasa na Hakuna team inayotamani kukutana nao kwa sasa Messi na barca yake walipigwa INE pale anfield

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PROPAGANDA ni kitu kibaya sana. Wengi wanaokuja kukwambia EPL ni ligi bora huwa na hoja za kijinga sana
Liverpool bingwa CL
Chelsea bingwa Europa ligi
CL final Liverpool v spurs
Europa ligi final Chelsea v arsenal
Team zote kutoka epl.!
Hzo ligi zenu bora huo ubora unaupatia wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligi ya kweli, ngumu na yenye msisimko kwa sasa ni EPL, zilizobaki ni ovyo tu.
Kuingiza timu 4 robo finali ya UCL siyo jambo dogo.
Timu nne za ligi moja kucheza fainali zote mbili za Ulaya msimu uliopita si jambo la kupuuzwa.
Hata hivyo kuchagua upande wa kupenda kama ulivyofanya mleta mada ni jambo la kawaida kwa kila kibinadamu
 
Kwa hiyo EPL ni ligi bora baada ya kutamba msimu uliopita tu? Walikuwa wapi miaka 10 mfululizo La Liga ilipokuwa juu?
 
Kwenye mchezo wa soka huwezi kuwa mbabe milele, ndiyo maana nimesema kwa sasa EPL ni kali na yenye
msisimko zaidi.
Hali kama hiyo iliwahi tokea kwa serie A na hata Laliga, lakini kwa sasa EPL imekamata mpini ingawa hulazimishwi kulikubali hilo.
Kwa hiyo EPL ni ligi bora baada ya kutamba msimu uliopita tu? Walikuwa wapi miaka 10 mfululizo La Liga ilipokuwa juu?
 
Kwenye mchezo wa soka huwezi kuwa mbabe milele, ndiyo maana nimesema kwa sasa EPL ni kali na yenye
msisimko zaidi.
Hali kama hiyo iliwahi tokea kwa serie A na hata Laliga, lakini kwa sasa EPL imekamata mpini ingawa hulazimishwi kulikubali hilo.
Ni timu moja tu ya Liverpool. Wengine wote vibonde kama kawaida yao.
 
Coach wa Man city amesema Liverpool msimu huu inaweza kuchukua ubingwa ligi yoyote kubwa Ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…