Livingston Lusinde: Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna wanaomsema vibaya Magufuli

Livingston Lusinde: Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna wanaomsema vibaya Magufuli

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mbunge wa Mtera Livingston Lusinde almaarufu kama Kibajaji, amewashukia kama mwewe Wabunge na Viongozi wa Serikali 'wanaomsema Vibaya Magufuli'. Akiongea kwa jazba huku na kutokwa povu, alijikita kwenye hoja hizi:

1). Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna baadhi ya Watanzania na Wabunge wanamsema Vibaya Magufuli

2). Leo najitoa Muhanga, haiwezekani tuwe na viongozi ambao wanajaribu kupinga mambo mazuri aliyoyafanya Magufuli

3). Wanaomsema vibaya leo Magufuli, Watamsema kesho Samia

4). Huwezi kuondoa legacy ya Magufuli kwenye nchi hii na bara la Afrika

5). Wabunge tuko humu ndani sababu ya Magufuli na Samia, kuna watu wako humu walikuwa hawachaguliki, akawatetea Wakachaguliwa sababu ya Magufuli na Samia

6). Leo hawa watu wanamsema Vibaya Magufuli sisi tupo na hata 40 haijaisha?

7) Mheshimiwa Spika hili jambo halikubaliki, Hawa watu washike adabu na adabu ziwashike, hatutaki warudie Mambo ya kipuuzi kama haya.

MY TAKE:

Je, Amani yetu mnataka muifanye nini, na Kwanini hutaki kumuita HAYATI Magufuli unamuita Magufuli tu?

Je, hao Wabunge ni wa Chama gani na Viongozi wa Serikali ipi?

Je, Chama hakina vikao halali vya kuongelea Maswala ya chama?

Je, kumtetea Magufuli lazima utumie lugha ya Matusi, Kejeli, dharau na Uongee kwa Sauti ya Juu ndo uonekane Unamtetea?

Je, Kibajaji ni lini utaandika Kitabu cha Kumuenzi Hayati Magufuli?

Je, Kibajaji unadhani kujikomba kwa Marehemu na Kumuona Mama Samia(Mwenyekiti wa Chama chako) kama si lolote si chochote, itakusaidia kupata Ubunge 2025

Polepole atakuponza, Mwenzio hagombei. Anakutanguliza mbele kupima upepo. Kwanza na chama kipya kinachoanzishwa hakitatoboa, kisubiri Uchaguzi wa 2024 na 2025 uishe.

Pia, soma:

 
Hayati Mwl. Julius K. Nyerere, muasisi na baba wa taifa hili anasemwa na kukosolewa na nchi na amani vipo, atakuwa Mwendazake John P. Magufuli ambaye binafsi namuona kama hakuwa na mbele wala nyuma...?

Lusinde acha utani wa kijinga bwana...!

Na sijui inakuwaje mnaogopa saaaana kusemwa kwa kukosolewa....

Mnapokosolewa, dawa siyo kujibu kwa kumwaga povu kama ufanyavyo wewe Lusinde au kujibu kwa bunduki na risasi, bali ni kukaa chini, mkajichunguza ili kuona mlipoangukia na kisha mkarudi nyuma na kuanza kujirekebisha....

Tunawakikishia kuwa nyie hamna nguvu yoyote. Nyie siyo wenye nchi. Wenye nchi ni sisi wananchi. Vyama vya siasa na serikali huja na kupita lakini nchi na wenye nchi huwako na kudumu siku zote na wao ndiyo huamua mchezo...!
 
Back
Top Bottom