Livingston Lusinde: Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna wanaomsema vibaya Magufuli

Livingston Lusinde: Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna wanaomsema vibaya Magufuli

Mbunge wa Mtera Livingston Lusinde almaarufu kama Kibajaji, amewashukia kama mwewe Wabunge na Viongozi wa Serikali 'wanaomsema Vibaya Magufuli'. Akiongea kwa jazba huku na kutokwa povu, alijikita kwenye hoja hizi:

1). Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama kuna baadhi ya Watanzania na Wabunge wanamsema Vibaya Magufuli

2). Leo najitoa Muhanga, haiwezekani tuwe na viongozi ambao wanajaribu kupinga mambo mazuri aliyoyafanya Magufuli

3). Wanaomsema vibaya leo Magufuli, Watamsema kesho Samia

4). Huwezi kuondoa legacy ya Magufuli kwenye nchi hii na bara la Afrika

5). Wabunge tuko humu ndani sababu ya Magufuli na Samia, kuna watu wako humu walikuwa hawachaguliki, akawatetea Wakachaguliwa sababu ya Magufuli na Samia

6). Leo hawa watu wanamsema Vibaya Magufuli sisi tupo na hata 40 haijaisha?

7) Mheshimiwa Spika hili jambo halikubaliki, Hawa watu washike adabu na adabu ziwashike, hatutaki warudie Mambo ya kipuuzi kama haya.

MY TAKE:

Je, Amani yetu mnataka muifanye nini, na Kwanini hutaki kumuita HAYATI Magufuli unamuita Magufuli tu?

Je, hao Wabunge ni wa Chama gani na Viongozi wa Serikali ipi?

Je, Chama hakina vikao halali vya kuongelea Maswala ya chama?

Je, kumtetea Magufuli lazima utumie lugha ya Matusi, Kejeli, dharau na Uongee kwa Sauti ya Juu ndo uonekane Unamtetea?

Je, Kibajaji ni lini utaandika Kitabu cha Kumuenzi Hayati Magufuli?

Je, Kibajaji unadhani kujikomba kwa Marehemu na Kumuona Mama Samia(Mwenyekiti wa Chama chako) kama si lolote si chochote, itakusaidia kupata Ubunge 2025

Polepole atakuponza, Mwenzio hagombei. Anakutanguliza mbele kupima upepo. Kwanza na chama kipya kinachoanzishwa hakitatoboa, kisubiri Uchaguzi wa 2024 na 2025 uishe.

Pia, soma:

View attachment 2003005
Mbona Watu wanakosa utulivu wa roho,kwani mwendazake Taifa ilikua mali yake, ? alikuepo Kama kiongonzi tu basi , hata angekua hajatwaliwa ipo SIKU angekuja mwingine nae angekaa pembeni Kama ambavyo waliomtangulia wamefanya , ni Ujinga kumtukuza mwanadam ,na hatukomi naona imeanza KWA mama pia, Tabia ya kijinga sana
 
Yuko sahihi 100% !

Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM ndani ya hili bunge walipita kwa msaada mkubwa wa JPM na sio uongo kwamba asilimia kubwa yao ni wanafiki.
 
Back
Top Bottom