Livingston Lusinde: Bashiru Ally alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu

Livingston Lusinde: Bashiru Ally alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu

Attachments

  • IMG_20211029_105959.jpg
    IMG_20211029_105959.jpg
    11.8 KB · Views: 3
"Kwenye dini tunafundishwa kushukuru. Yeye (Dkt Bashiru Ally) alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu (kuteuliwa). Mtu ambaye ugali wake unatokana na Ikulu, anakerekage Ikulu kusifiwa. Kama anakereka ... basi apishe." - Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Chawa huwa ni watu wasio na elimu au wana elimu feki za rushwa au kuiba. Dkt Bashiru ni msomi nguli.
 
Bashiru anamuwakilisha aliyemteua, haileti mantiki kumkosoa, anatakiwa amsemee na kumtetea yeye, sio kumkosoa.
Ubunge wa kuteuliwa na wa viti maalum ufutwe.
Kwahiyo analipwa 12M kwa mwezi nje na posho kibao ajili ya kumsifia aliyemteua?
 
"Kwenye dini tunafundishwa kushukuru. Yeye (Dkt Bashiru Ally) alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu (kuteuliwa). Mtu ambaye ugali wake unatokana na Ikulu, anakerekage Ikulu kusifiwa. Kama anakereka ... basi apishe." - Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Safi Sana Lusinde Hakuna kung'ata maneno
 
"Kwenye dini tunafundishwa kushukuru. Yeye (Dkt Bashiru Ally) alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu (kuteuliwa). Mtu ambaye ugali wake unatokana na Ikulu, anakerekage Ikulu kusifiwa. Kama anakereka ... basi apishe." - Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Sijaelewa hapa, kwani unapewa Ubunge kama asante ama unapewa kwa sababu ya uwezo wa utendaji wako wa kazi.?

Kama ni kweli mtu anapewa Ubunge sababu ya ushikaji, uchawa, kuzibwa mdomo ama asante basi tuna safari ndefu mno watanzania na kama tutafanikiwa kufika basi tutafika tukiwa tumechoka saana.
 
Bashiru atakumbuka kitabu kilichoandikwa kheri yangu mimi sijasema
ha ha ha... huyo ni mtu wa tatu, baada ya wengine 2 wa mwanzo kusema "mnawakanyaga wenzenu kama majani"

Hii ni hadithi iliyohusu vita katika ufalme fulani, ambapo wapiganaji watatu wakiwa vitani waliamua kujificha kwa kujifunika na nyasi, bahati mbaya adui akawa anapita eneo lile na kuwakanyaga bila kujua. Mmoja wa wapiganaji hao akalalamika; “kwanini unawakanyaga wenzio kama nyasi?” Yule adui akashtuka kuwa pale kuna mtu kajificha akamchoma mkuki na kumuua. Mpiganaji wa pili akamuonya mwenzake; “kwanini wewe unasema, je, tukigundulika?” Adui akamchoma mkuki na kumuua pia. Yule wa tatu kwa kujiamini akiamini kuwa yeye yuko salama akasema; “heri mimi sijasema”. Naye akachomwa mkuki na kufa. Huo ukawa mwisho wa wapiganaji wale watatu.
 
"Kwenye dini tunafundishwa kushukuru. Yeye (Dkt Bashiru Ally) alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu (kuteuliwa). Mtu ambaye ugali wake unatokana na Ikulu, anakerekage Ikulu kusifiwa. Kama anakereka ... basi apishe." - Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Kumbe Sasa unaweza kuona Aina ya viongozi tulio nao kwa kupitia matamshi Yao.

Cheo ni dhamana anahopewa mtu kwa niaba ya watu Ili awaongoze kufikia matarajio Yao ya kila siku. Uongozi wa kisiasa sio ajira, ni utashi na uwezo wa kuwaleta watu Pamoja Ili kwa Pamoja waweze kupata maendeleo yao kwa ujumla na mmoja mmoja.

Kwa kauli ya lusinde ubunge ni ihsani ya kupata mahala pa kujilimbikizia Mali na kupata ugali wa kila siku.

Kwa maana hiyo mbunge awe wa kuchaguliwa (ndugai) au wa kuteuliwa (Bashiru) hapaswi kusimamia maslahi ya wananchi dhidi ya serikali ambayo wao ndio wameiweka madarakani Bali wanapaswa kukaa kimya na kuinyeyekea.

Hii ni Cancer ya Taifa na hii utamaduni ukiendelea viongozi hawataogopa wananchi Bali wananchi watawaogopa wanasiasa!

Hata wananchi wa kawaida wanashangaa Sana ikulu inavyosifiwa kwa hata mambo ambayo hayapo kabisa.

Na kwa kulitambua Hilo wanasiasa wetu wangepitia mitandao yote ya kijamii Leo hii waone response ya wananchi juu ya matamko Yao na mamma Bashiru alivyoungwa mikono.

Wakitokea kina BASHIRU watano au Kumi naamini watanzania wataona mkono wa dola hadharani! And this is what we want, people with courage to stand on Mass's side! Badala ya kuwalamba miguu watawala! People who have nothing to loose except their integrity!

Mshindo mmoja tu chawa kibao wamejitokeza!
 
Bunge letu msimu huu limepata wabunge wa hovyo kuwahi kutokea....... ukitazama bunge ni kama unatazama kikao Cha walevi wa banana....
 
"Kwenye dini tunafundishwa kushukuru. Yeye (Dkt Bashiru Ally) alipaswa kuwa chawa mkuu sababu Ubunge wake unatoka Ikulu (kuteuliwa). Mtu ambaye ugali wake unatokana na Ikulu, anakerekage Ikulu kusifiwa. Kama anakereka ... basi apishe." - Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Halafu ameongea kwa mamlaka kabisa kama vile bado ni katibu mkuu wa CCM. Mimi ni mwenyeji wa Kagera nilichojifunza tangu 2015 ni kwamba watu wa mkoa huo hatuna sifa ya kuwa na vyeo vikubwa vya kutuweka ikulu.

Tuna superiority complex kubwa sana na huwa na madhara katika maamuzi na ufuatiliaji wa kinachoamuliwa.
 
Back
Top Bottom