Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Ufinyu wa elimu ndo unamfanya awe alivyo-anajitutumua!

Masikini ni wengi n.a. kila mmoja hutoka kivyake.Si ajabu angesoma asingekuwa alivyo.Angekuwa mstaarabu wa "kinywa".

Masikini akiokota matako hulia mbwata. N.a. damu ya watafiti wetu inawalilia watu wa aina yake. Ujinga ni mzigo!
 
Sawa.Tumekusoma.
 

Mkuu Paskali, Hakuna uwekezaji mzuri wenye kulipa Duniani kwa wapenda madaraka kama Ujinga, Na bila shaka lolote CCM katika hili wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana namaanisha uwekezaji mkubwa kwenye Ujinga. Na uzuri CCM hili wanalijua kabisa juu ya huu uwekezaji katika Ujinga.. Ukipiga vita ujinga utakuwa umepiga vita CCM na lazima hapo upambane na CCM.

Suluhisho: Aina nyingine ya ukombozi unahitaji hapa hasa wale waliojitambua kuwanasua wajinga walio wengi kutoka kwenye ujinga aka "undondocha", Ni vizuri wale wenye kuelewa kujaribu kuelimisha zaidi jamii ya kitanzania dunia ilipo na Tanzania ilipo na tatizo ni nini na hapa tutakuwa tumesaidia jamii. Tunapoenda kupambana na CCM wakati jamii bado imetopea kwenye ujinga kama mtaji wa CCM tutajikuta wachache na huyu adui CCM/UJINGA atatumaliza.
 
Hoja hii inaukweli, niliwahi kuizungumzia hapa.
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?
P.
 
Safari hii ukurugenzi wa kagera unao
 
Kipi amefanya Hadi aonekane kichwa
 

Kutoka kwenye kurekebisha kanda na bi Edina pale kwa Komba hadi kufikia kumiliki majumba, magari ya kifahari na mashamba ndo hapajazungumzwa. Nadhani hiyo akili kubwa unayoisema ndo ipo katikati hapo. Majumba, magari na mashamba ni matokeo, sasa tupe mchakato uliotumia hiyo akili kubwa kuleta hayo matokeo.
 
Watumishi wa umma wako wa ngazi mbili, Luna maofisa na wafanyakazi wa kawaida. Hao maofisa wanalipwa vizuri, wanalipiwa nyumba, wakisafiri wanalipwa per diem kubwa kuwazesha kulala hotel na 'blangeti'!. Wafanyakazi wa kawaida, wanalipwa mishahara kiduchi, hawalipiwi nyumba, na wakisafiri, wanalipwa per diem ndogo kuwatosha kulala guest na sio hoteli.

Mimi nilianzia kazi ya utangazaji RTD, kwa ngazi ya afisa, hivyo kuanzia Mkurugenzi na maofisa wote wanaishi nyumba za serikali, sisi Watangazaji tulipangiwa nyumba zinalipiwa na ofisi, wafanyakazi wa kawaida hawapangiwi nyumba wanapanga vyumba uwazi!.

Amini usiamini, hao maofisa kuanzia Mkurugenzi, hadi wanastaafu, wamestaafu hawajajenga nyumba, kama sio ule mpango wa Mkapa kuwauzia watumishi wa umma zile nyumba za serikali, kuna watu wangeumbuka!.

Sisi watangazaji kutokana na umaarufu, nyumba bure, starehe bure, bia na pombe bure, mademu wanatupapatikia, wengi wa watangazaji wa zamani pesa zetu ziliishia kwenye starehe.

Lakini huwezi amini, wale wafanyakazi wa kawaida wa kada za chini wakiwemo madereva, wote wana nyumba zao za kujenga na wanakula kodi!. Wengi wana mashamba, pesa yao kiduchu wanafanya mambo ya maana.

Hivyo mtu aliyezoea shida na kuishi maisha ya kimasikini anakuwa more financial conscious, anaweza kuishi with more savings kuliko walioishi kwenye utajiri!.

Mfano mzuri ni linganisha life style ya JK na JPM!.
P
 
Akili yake imemsaidia kula good tyme. Imefikia kiwango anasahau akiumwa kifua anaenda kutibiwa na mwanafunzi wa profesa.

Infact hakuna nchi maprofesa wanatukanwa kama TZ. Sijui ni nani alowaloga watz. Sijui pia maprofesa walowakosea nini watanzania.


basi sawa Paskali.
 
Hapa umejielezea wewe ambaye ulikuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira. Yeye alitumiaje akili yake kubwa kufika huko hadi akawa na uwezo wa kupambana na Malechela huku akiwa ni darasa la tatu na hana back up yoyote. Huo mchakato ndiyo utakaowahamasisha vijana wasio na elimu kujifunza kutoka kwake na kutokata tamaa.

Tuambie alifanya nini hapo katikati?
 
Mimi nitajuaje?.
P
 
Na huwezi kuwa na akili timamu ukafikiria TL anaweza kuwa rais wa nchi hii.. kwa akili zako kuna siku utasema hata Lusinde au Kibajaji anaweza kuwa rais...watanzania wenye akili wanakusoma wanakuoa kiazi sana.
Mkuu GuDume, hapa Unamaanisha nini?, unamaana wote wanaomuona Tundu Lissu anaweza kuwa rais wa nchi hii, hawana akili timamu?.

Kwanini unamdharau Kibajaji?
Msome kwenye bandiko hili.

P
 

Paskali,
Unataka kuniambia Kibajaji anakuxidi akili kweli? Darasa la 3, mtu ambaye hata cheti Cha Shule ya msingi Hana...!!!You must be seriously joking!
Lakini sishangai kwa Wana CCM kusifia na kushangilia watu Kama Kibajaj simply because anajua Kutukana, kushambulia na kubeza Wapinzani.
Kwangu Mimi Lusinde Kibajaji is a Low IQ like any other uneducated guy!? Huu ujinga wa kuendekeza Wabunge wenye Low IQ ndo umeifikisha CCM hapa ilipo.
Bunge zima la CCM lenye Madokta na Mapro-fedha wanakaa kusikiliza Ushauri wa mtu wa Darasa la 3 na wanaupokea na kuufanyia kazi....!!! What a shame to Graduands and the educated class in Tanzania? Huu Ni udhalilishaji wa Elimu ya Tanzania kwa ujumla wake. Haiwezekani Watu wasomi wapokee maelekezo toka kwa mtu aliyeishia darasa la 3!!
Na hii tabia iko Sana Bunge la Tanzania. Leo utamsikia Kibajaji na kedho utameikia Msukuma Joseph Kasheku akinanga Maprofedha wa CCM halafu wanabaki kumshangilia kama mazuzu! What a non-sense!
Unasema ati anaonekana ana Powers fulani...!! What Powers are you talking about? Darasa la 3 awe na Powers zipi? Nikakubaliana na wewe kwa 100 % Kama unazungumzia MAGICAL POWERS (Nguvu za Kichawi/Vigagula). Ninajua Majitu mengi ambayo hayakwenda shule yanaishi kwa kutegemea NGUVU ZA GIZA Kama ndumba, uchawi, majini na kuroga kwenda mbele!!!
 
Umenikumbusha Hussein mwinyi mtoto wa mzee mwinyi, Nape mtoto wa mtoto wa mzee nape, jenister mhagama mtoto wa mzee mhagama, Riziwani mtoto wa mzee kikwete, January makamba mtoto wa mzee makamba, Fred Lowasa mtoto wa Mzee Lowasa. Karume mtoto wa Mzee Karume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…