Watumishi wa umma wako wa ngazi mbili, Luna maofisa na wafanyakazi wa kawaida. Hao maofisa wanalipwa vizuri, wanalipiwa nyumba, wakisafiri wanalipwa per diem kubwa kuwazesha kulala hotel na 'blangeti'!. Wafanyakazi wa kawaida, wanalipwa mishahara kiduchi, hawalipiwi nyumba, na wakisafiri, wanalipwa per diem ndogo kuwatosha kulala guest na sio hoteli.
Mimi nilianzia kazi ya utangazaji RTD, kwa ngazi ya afisa, hivyo kuanzia Mkurugenzi na maofisa wote wanaishi nyumba za serikali, sisi Watangazaji tulipangiwa nyumba zinalipiwa na ofisi, wafanyakazi wa kawaida hawapangiwi nyumba wanapanga vyumba uwazi!.
Amini usiamini, hao maofisa kuanzia Mkurugenzi, hadi wanastaafu, wamestaafu hawajajenga nyumba, kama sio ule mpango wa Mkapa kuwauzia watumishi wa umma zile nyumba za serikali, kuna watu wangeumbuka!.
Sisi watangazaji kutokana na umaarufu, nyumba bure, starehe bure, bia na pombe bure, mademu wanatupapatikia, wengi wa watangazaji wa zamani pesa zetu ziliishia kwenye starehe.
Lakini huwezi amini, wale wafanyakazi wa kawaida wa kada za chini wakiwemo madereva, wote wana nyumba zao za kujenga na wanakula kodi!. Wengi wana mashamba, pesa yao kiduchu wanafanya mambo ya maana.
Hivyo mtu aliyezoea shida na kuishi maisha ya kimasikini anakuwa more financial conscious, anaweza kuishi with more savings kuliko walioishi kwenye utajiri!.
Mfano mzuri ni linganisha life style ya JK na JPM!.
P