Liwalo liwe, kila mtu na lwake!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
Liwalo liwe, kila mtu na lwake, ndiyo hatima ya Tanzania!
 
Ndugu tafadhali weka heshima unapoweka post yoyote sio kila post lazima uweke kwenye jukwaa la siasa , na sio lazima kila mara uweke post
 
Liwalo liwe, kila mtu na lwake, ndiyo hatima ya Tanzania!

It real sounds like that pastor!

Wakitokea wanaotaka kutupeleka kuzuri wanakatishwa tamaa, ukijifanya unawapenda watanzania unashushuliwa!

Huu msemo wako wana utekeleza kw vitendo walimu wa vyuo na baadhi ya wasomi, kuna msomi mmoja hamjui waziri wa mambo ya ndani! professor!
 
Stop asking what your country can do for you and ask yourself, what can you do for your country. by JFK 1960s
 
Liwalo liwe, kila mtu na lwake, ndiyo hatima ya Tanzania!
Kweli mchungaji, hebu angalia mvutano usio na aibu wa posho za wabunge, yaani ni kama mchezo wa watoto huyu anamwaga ugali na yule anamwaga mboga halafu tukose wote,..................... "Hosea anazuia suruali yake huku anataka kuwavua wabunge nao wabunge wanazuia wasivuliwe suruali zao wakati huo huo wanataka wamvue suruali Hosea"
 
Yes mchungaji!

Sema upo USA....lkn kwa walio Bongo hicho ndicho kinanachotokea sasa! Public goods, zinabinafsishwa, watu wachache sana wanazifaidi...labda bado hewa tu....lkn nayo inakuwa polluted etc!

Pia ukiangalia maisha yakawaida ya watanzania, kila mmoja anastruggle kivyake! Ukiuguliwa na mtoto, baba, mama, wewe mwenyewe...utahaingaika weeee, mara sijua Agakhan, Mikocheni,tumaini etc (only km unatusenti) au India or SA........! wenye watoto, kila mmoja anahangaika kivyake wapi mtoto atapata elimu nzuri, wapi atapata entertainment, wapi atapata ajira, wapi atatibiwa etc! Ukitaka ardhi/kiwanja....basi wale wenye undugu/urafiki na wenye dhamana na ardhi ndio wanakatiwa mapande ya ardhi kama mapande ya nyama bucha, huku wale wenzangu na mimi wakibaki kutoa macho wasijue hatima yao na watoto wao! Ili mradi tu, mstakabali wa mtanzania mmoja mmoja (has masikini) pamoja na watoto wao upo juu ya wao wenyewe sio kama taifa....kila mtu anapigania mkate wake na watoto wake tu.......!

Bongo now kila mmoja anastruggle kivyake vyake, hakuna uzalendo wa kweli, hakuna umoja wa kweli, hakuna amani ya kweli, kila mmoja anavuta kamba kwake tu!
 
Ndugu tafadhali weka heshima unapoweka post yoyote sio kila post lazima uweke kwenye jukwaa la siasa , na sio lazima kila mara uweke post

na wewe sio lazima kila post uwe unajibu.by the way who are you hapa JF unajifanya kiranja hapa..kwenda zako bana
 
Jamani msameheni Shy, nitamjibu kejelizake.

  1. Shirika la Bima linafilisiwa baada ya kubinafsishwa kutokana na mfumo wa uchumi huria. Baada ya Ubinafsishaji kumalizika, Serikali itaanzisha shirika jipya la Bima.
  2. Sekab wamejitoa kwenye ule mradi wa Miwa ya mafuta, sababu hazieleweki lakini tulishawapa ardhi kibao na misamaha kibao. Najiuliza, tuliwapa hii ardhi kwa ajili ya bei ya mafuta kupanda mwaka jana au vipi
  3. Membe kachimbia mkwala mabalozi wasisaidie vyama upinzani. Lakini misaada kwa Tanzania inayopitia CCM na Serikali yake ni ruksa hata kama itahakikisha CCM inaendelea kutawala milele!
  4. Mradi wa Umeme kule Mbeya uliosimama miaka 11 kufanyiwa kazi, unaanza tena, swali ni nani aliboronga na sasa hivi utatusaidia vipi kwenye shida yetu ya umeme?
  5. IPTL impewa ruksa kutuzalishia umeme huku kuna ugomvi mkubwa wa kufilisiana kati ya wenye hisa ndani ya IPTL. Zaidi, Serikali yetu imesema itagharamia kila kitu kuhusiana na uzalishaji huu wa umeme wa IPTL unaoanza kesho. Je tumepunguziwa bei kwa kila kilowati ya umeme unaozalishwa ikiwa mafuta ni yetu na kila kitu ni chetu na wao kazi yao ni kutumia mitmbo yao?
  6. Spika anadai Takrima si dhambi, kupewa posho ni utamaduni wa Kitanzania na hivyo tukipeana posho na takrima ni jambo sahihi. Je lini tutapiga vita ufisadi?
  7. Sakata la Richmond limeamuliwa ki-CCM kama nilivyotabiri. Kama kamati ya Chama, pande zote mbili zimeafikiana kulizungumza ndani ya kamati ya madini na si Bungeni (publicly) na hivyo kila mtu kanyamazishwa kuinusuru CCM na Serikali yake!
  8. Edward Hosea kachaguliwa kuwa mjumbe kwenye Bodi ya Ushauri UNDP kweye masuala ya kupigana vita na rushwa!
  9. Wabunge na Serikali wanapigana vifua, wanakataa kupelelezwa na TAKUKURU! Wabunge wa CCM wanadai Posho Ruksa, wale wa Upinzani wanadai Posho ni rushwa!
  10. Simba kaifunga Yanga, refa kaionea Simba na kutoa kadi nyekundu, Nguza akata rufaa, Ferre Gola na Shikito wanakuja Tanzania, Minofu ya Samaki kugawiwa wananchi, Serikali kununua mazao kutoka wka Wakulima, Mwekezaji Kapunga Rice kapigwa mkwala na Rais....
  11. nk, nk, nk, nk, nk, nk, nk GT bado anawatafuta Free Masons, I mean Freeman Mbowe, wengine wanajiuliza kuhusu Azimio la Arusha na Shy anadai Mchungaji Punguani!
 
na wewe sio lazima kila post uwe unajibu.by the way who are you hapa JF unajifanya kiranja hapa..kwenda zako bana

Shy ni kama mgonjwa fulani wa kifafa. Kuna wakati mwezi ukiwa kati basi kinamtokea hakiponi bali hutulia tu. Kitakapo tulia tena atarudia akili yake.


asante mkuu kama kuna mtu hataelewa hapa basi huna jinsi ya kumsaidia
 
Ama kweli kila mtu la LWAKE!


[ame="http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM&feature=player_embedded"]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM&feature=player_embedded[/ame]
 

Mchungaji,

Aisee nimeguswa sana na mlolongo /orodha ya mambo mengi yanayotokea bongo kwa sasa...and yes, the conclusion of it...ni kila mmoja na lwake! Aisiye na mwana aelekee jiwe!
 
Stop asking what your country can do for you and ask yourself, what can you do for your country. by JFK 1960s

Ndugu tafadhali weka heshima unapoweka post yoyote sio kila post lazima uweke kwenye jukwaa la siasa , na sio lazima kila mara uweke post

No wonder that's why hata ulizushiwa kifo hapa..........! Shirikisha ubongo wako kabla hujapost bana!
 
Tuseme Haleluja, hatakama mchungaji anongea pumba, hii ndio tamaduni yetu!!!

Haleluya, Ameen
 
Wakati JK Nyerere akiwapinga Kina Lowasa na Kikwete kuna watu walidhani yule mzee alikua amepitwa na wakati, sasa ni dhahiri kua kila Mtanzania mwenye kufikiri anaona namna nchi inavyoyumba, kwa mambo ya hovyo-hovyo.
Rais anaeshughulikie kubadili Picha zake za ukutani nnchi nzima kweli anajua vipaumbele vinavyoikabili nchi, anapata wapi muda wakutazama picha zake ? taifa limeingia kwenye njaa kali, serikali inasambaza waraka kutaka picha zote katika taasisi zinazo muonyesha rais zibadilishwe, ziwekwe mpya ambapo Rais anaonekana Handsome zaidi.
Tunafanya mambo yetu hovyohovyo. nchi haina dila wala mwelekeo, ama kweli kila mtu na lwake.
 
Bhagosha,

Mchungaji Post yako nayo ni kali ila kwa upande mwingine nataka niwakumbushie kitu kimoja tu na sio kwamba ati nachochea bali kuliweka bayana na mlijue, Hizi choko choko na maneno ya hapa na pale toka kwa viongozi mbali mbali kila serikalini,viongozi wa dini zetu raia nao kwa mtindo huu huuu ndio chanzo cha Vita ya Huko Rwanda na Burundi kwani yalisemwa mengi na viongozi husika hawakuchukulia hayo mambo seriously na matokeo yake gafla mitutu ikaanza tembea nasi ndiko am sure twaelekea kaeni chinjo na mauaji ya viongozi nayo yata anza damu ita mwagika muda si mrefu ngojeni mtaona kama hatuta pata kiongozi mwenye hekima na kutuliza hili joto sijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…