Liyumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu

kama recruitment process haikufuata taratibu basi zoezi nzima la kuwaajiri hao watoto wa vigogo ni batili,sasa hapa inategemea contract of employment waliyosaini inasemaje? kama haijafikia standards za contract of employment kama sheria ta ya kazi ya namba 6 ya 2004 invyoelekeza. kunauwezekano wakatiwa hatiani.

na kama waliajiriwa wakiwa hawana sifa kwa nafasi zao then wakapata sifa wakiwa tayari wameshaajiriwa ni kosa kisheria.

Naunga mkono hoja ya kufanya human resources auditing na independent firm ili kubaini taratibu za ajira zilizokiukwa.

ahsanteni sana
AM
 


Inawezekana umeshajibiwa vizuri zaidi huko nyuma. Kama bado, basi fahamu kuwa rushwa ni kitu chochote anachopata mtu ili atoe upendeleo wa aina fulani kinyume cha utaratibu wa kisheria. Kuna rushwa zinazomfaidisha mpokeaji kwa njia ya mali na rushwa zisizokuwa za mali, kwa mfano kupokea rushwa kwa kupewa uroda na na kupokea rushwa kwa kupewa usalama fulani kazini kupitia kwenye memo .
 
Msalie mtume Simon,tena temea mate chini,usiwe so hateful.Unayemzungumzia kwamba kaungua maini kwa pombe ninamfahamu na cause ya illness yake sio pombe.So long as tunapumua tuwe tajiri au maskini,fisadi au mwadilifu lolote linaweza kutokea katika afya zetu,huo ndio uhalisia wa maumbile na ndio maana hakuna anayeishi milele.Ni haki yetu na pia wajibu kuchukia ufisadi lakini tusiwe so personal kwa yale ambayo hatuna uhakika nayo asilimia mia,naomba kuwasilisha.
 
Oyaa....vipi yule mzungu wako wa kwenye trailer park....? keshakutosa nini

....nenda kamsikilize Limbaugh maana executive order za Obama zinawafanya muonekana dumb,2012 hakuna election labda mjaribu 2016!
 
KLHN International

Watumishi wawili wa Benki Kuu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar wakikaribiwa na mashtaka mbalimbali ambayo ni pamoja na kutumia madarka vibaya na kusababishia hasara serikali ya zaidi ya Shilingi Bilioni 220. Watumishi hao Bw. Joachim Liumba ambaye ni Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Benki hiyo na Deogratias Kweka ambaye ni Meneja Miradi walitakiwa kuwa na dhamana ya kiasi nusu ya kile kinachodaiwa. Wameshindwa dhamana na sasa wamepelekwa Keko wakisubiri kesi yao kutajwa tena.

Kesi hiyo inayowakabili inahusu ujenzi wa ziada wa majengo ya Minara Pacha ya Benki Kuu ambayo imedaiwa kwa muda mrefu kuwa imetumia kiasi kikubwa cha fedha ambapo ujenzi wa Minara hiyo hadi sasa umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 300 na kufanya majengo hayo kuwezekana kuwa ni yenye gharama kubwa zaidi katika Afrika ukilinganisha na ukubwa wake na sehemu ya soko.
Mradi wa minara miwili ya Benki Kuu unaigharimu Tanzania Dola 8625 kwa kila mita ya mraba ambapo gharama ya mita kama hiyo sehemu nyingine Tanzania (na Jijini Dar hususan) ni dola 700. Ujenzi wa aina hiyo kwenye majiji ya New York (Marekani) na Tokyo (Japan) haizidi dola 3000 na vyumba hivyo vinakuja vikiwa na samani.

Majengo hayo ambayo yana mita za mraba 40,000 kama yangegharimiwa kwa kutumia viwango vya New York yasingezidi dola milioni 120. Na hapa tunajumlisha gharama za vikolombwezo vyote vikiwemo vifaa vya usalama, teknolojia nyingine, kusimamia dhahabu n.k

Bodi ya Wahandishi wa Tanzania, Bodi ya Wasanifu Majengo, na Bodi ya Wakandarasi zote zilipinga gharama na mchakato mzima wa ujenzi wa majengo hayo lakini serikali ya CCM iliamua kuendelea nayo. Hadi kifo chake Gav. Ballali aliweza kutumia zaidi ya dola milioni 345 katika ujenzi ambao hadi hivi sasa haujakamilika.

Licha ya tuhuma kuwa kuwa Gav. Ballali alipokea rushwa/hongo ya karibu dola milioni 5 serikali haikumchunguza na kumuacha aendelee na mpango huo baada ya kampuni ya Sanska ya Uswedi kuondolewa. Gav. Balali aliendelea kwa kuajili kampuni ya Group 5. Tatizo ni kuwa Group 5 ni kampuni tanzu ya Sanska. Kwa maneno mengine walinyang'anywa kwa mkono huu wakapewa kwa mkono mwingine.

Gharama ya hasara kwa Tanzania ni karibu dola milioni 265 ambazo zinaonekana leo kwenye mashtaka dhidi ya kina Liumba. Mashtaka haya dhidi ya kina Liumba ni wazi ni katika kutekeleza ahadi aliyoitoa Gavana Benno Ndulu karibu miezi mitatu hivi iliyopita ambapo alisema kuwa Benki Kuu imeajiri makampuni ya kimataifa kufanya ukaguzi wa gharama halisi za majengo hayo.

Kampuni ya M/S Mekon ARC ya nchini ilipewa jukumu hilo ikishirikiana na kampuni ya AQE Associates na Bureau for Industries ltd. "Tunataka kujua kama fedha tulizotumia zinalingana na thamani ya majengo haya au la......tuliahidi kuwa tutakagua mahesabu ya ujenzi wa majengo haya na sasa ndiyo tumeanza" Alisema Gavana Ndulu aliyechukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha Gavana Ballali.

Mashtaka haya dhidi ya kina Liumba yanatishia watumishi wengine wa serikali ya awamu ya tatu ambao walisimama kutetea ujenzi wa majengo hayo wakiwa Bungeni na ambao bila ya shaka maamuzi yao ndiyo yamechukuliwa kuwa ni baraka za ujenzi huo. Aliyekuwa Waziri wa Fedha Bi. Zakhia Meghji alizungumza wakati wa kufunga mjadala wa Wizara yake mwaka 2006 na kutetea ujenzi wa majengo hayo.

Hata hivyo Waziri Meghji alikumbana na wakati mgumu alipobanwa na Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Siraju Kaboyonga (CCM) ambaye aliuliza "Nafikiri waziri hajajua swali langu, nasema hivi, mtaji wa BoT ni sh bilioni 20, lakini thamani ya majengo yake, haiendani na mtaji huo, fedha hizo za ujenzi zimetoka wapi" Waziri Meghji alionekana kubabaika wazi hadi alipoweza kuokolewa na Naibu Spika Mhe. Anna Makinda.

Hata katika kikao cha bajeti cha 2007 kiongozi wa upinzani Bungeni Mhe. Hamad Rashid Mohamed naye alihoji juu ya ujenzi wa majengo hayo.

Gavana Ballali mwenyewe alijitetea mwaka 2007 Julai na kuelezea kuwa madai ya kutumia fedha zaidi kwenye ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ilikuwa ni mwendelezo wa tuhuma dhidi ya magavana wa Benki Kuu na yeye hakuwa wa kwanza. "Gavana Charles Nyirabu (marehemu) alikuwa na mpango wa kupanua jengo la BoT, alikumbwa na kashfa kama ya sasa.

"Alivyokuja Gilman Rutihinda, naye alipanua sehemu ya jengo tunalolitumia sasa, naye aliibuliwa kashfa, akaacha na alipokuja Gavana Idrisa Rashid, akaendeleza ujenzi huo naye alikumbwa na kashfa hiyo hiyo na mimi nilivyoingia mwaka 2000 na baadaye kuanza ujenzi wa ‘Twin Tower', maneno yameibuka tena" alisema Gav. Ballali ambaye baada ya sakata la EPA kuibuka alitoweka nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kufuata matibabu huko Marekani katika hospitali isiyojulikana. Alitangazwa kuwa amefariki dunia muda si mrefu tangu ombi langu la kujiuzulu kukataliwa na Rais. Alifukuzwa kazi na Rais wakati akitangaza kuundwa kwa timu maalumu ya uchunguzi wa EPA .

Wachunguzi wa mambo ya kisheria nchini wanaangalia kama watendaji wajuu wa wizara nao watafikishwa mahakamani kama walivyofikishwa Bw. Basil Mramba na Daniel Yona ambao nao kutokana na nyadhifa zao wanatuhumiwa kuzembea na kufanya maamuzi ambayo yamelisababishia taifa hasara kubwa. Kiasi kinachodaiwa katika suala la majengo pacha ya Benki Kuu ni mara 22 zaidi ya kile kinachodaiwa katika kesi ya kina Mramba na Yona.
 

- Mkuu Halisi tupo pamoja hapa, lete dataz I Love this Kisutu's thing yaani the Mtakujas! Tupo wote mkuu saafi sana, sasa ngoja tutafute yaliyojiri behind the scene na this.
 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,

Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?
 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,

Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?

absolutely... mazingaombwe ni sanaa ya kuaminisha visivyoaminika na kufanya vile vilivyopo kushawishi kuwa havipo. Mazingaombwe siyo kufanya kitu bali kukifanya kitu hicho kiasi cha kufanya kiaminike kuwa kimefanyika. Kwani tatizo ni kufika mahakamani? Well wanaweza kupelekana wote mahakamani. Kama hilo linakuridhisha sawa. Kwani hawa ni viongozi au watumishi wa kwanza kupelekwa mahakamani? Hakuna kiongozi au mtumishi au mfanyabiashara yoyote ambaye amefikishwa mahakamani sasa hivi ambaye kesi yake haina mfano katika TAnzania.
 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,

Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?

- Mkuu Kasheshe, pole pole maana ni innocent until proven guilty sasa tuwape nafasi waliofikishwa kwenye sheria wapate the due process affodable by our law, wakishafika tu kwenye sheria siasa inasimama kwanza na kutoa nafasi kwa sheria kufanya kazi yake, kwani rais wetu anahusika vipi na sheria ya jamhuri ambayo ilikuwepo hata kabla hajawa rais?

- Sasa tusije tukadanganyana hapa maana wote tunajua kuwa sheria yetu inafanya kazi ndio maana Mtikila ameishinda serikali yetu mara nyingi tu, ndio maana maofisa wa serikali walimshitaki Mkapa akiwa rais na wakamshinda, familia ya Kombe iliishitaki serikali na kuishinda pia,

Wakishafikishwa kwenye sheria ni vyema kuipa nafasi sheria ichukue mkondo wake kama vile kwenye kesi ya "Carlifornia People Vs OJ Simpson", ingawa wengi tuliamini alikuwa guilty sheria haikusema hivyo na haina maana ile kesi ilikuwa ni Ze Comedy, kama sheria zetu ni mbovu that is another ishu of its own!
 
Nakubali kabisa kuwa BOT TWIN TOWERS ni scandal ya hali ya juu na gharama zake ni kubwa mno, ambayo moja kwa moja inaprove kuwa rushwa na uzembe ulitumika.

1)Lakini siamini kuwa watu hawa wawili walikuwa na power ya kufanya Twin Tower cost ziwe inflated kwa kiasi kikubwa.

Lazima Waziri wa fedha, Gavana Ballali, Naibu Gavana, Board ya Bank, Ofisi ya Rais, TISS kote huko nako kutoe wazembe waliosababisha hasara hizi.

Anyways, Kwa Liumba malipo ni duniani so kukaa kwake jela ni sawa, ila lazima Takukuru waongeze watu zaidi sababu uzembe ulikuwa sehemu nyingi mno.
 
Last edited:
Hakimu alikuwa nani jamani........je ni yule yule Mlokole Mwankenja au?

Hili suala la majengo ya BoT tulishalitolea maelezo mengi sana huko nyuma.......na hata sehemu za kufuatilia ili kuonyesha ulaji uliokithiri kuhusiana na huu Mradi.........inafurahisha kuona sasa hatimaye watu wanapelekwa mahakamani..........thats a good thing.......

kinachonisikitisha ktk hili ni kumkosa Balali.......maana Jeuri aliyokuwa nayo........haikuwa na kifani......na Jeuri (BWM blessings) hiyo aliipata toka kwa BWM mwenyewe.......ikumbukwe pia before BWM alishatamka kuukataa huo mradi......kwamba haukuwa na tija na kwamba Taifa lina priorities za msingi za ku-take-care.........suprisingly alipomuweka tu rafiki yake Balali hadithi ikabadilika...........

Invisible............hivi hizo gharama za ujenzi tunazoambiwa......je zimejumuisha procurement process tokea mwanzo?......kumbuka huu mradi uliahirishwa kama sikosei mara tatu tena under different designs na consultants wakala pesa za bure.......ofcourse halikuwa kosa lao (hao consultants).....lakini ukifuatilia kwa undani utakuta yule mhindi Architect ana influence kubwa sana ktk utekelezaji wa mradi mzima (with changes introduced) + costs........

.......ninachojiuliza na inachoumiza ni wale wazalendo (wanajulikana) waliokuwa wakipinga mradi huo.......na hata wakawa frustrated kazini.......sijui wako wapi saa hizi.......smart pple (wazalendo) mara nyingi huwekwa aside....kwani huonekana tishio kwa ulaji wa watu....na hata wakati mwingine.......na kufukuzwa kazi kwa visa vya ajabu kabisa........wakati akina Liyumba and Kweka's wanatanua

Invisible....kwlei kabisa.......Mramba and Yona case ni cha mtoto kwa hili la twin Towers na hata EPA.........

.......pia sehemu nyingine ambayo Taifa inaingizwa hasara kubwa hivi sasa ni kupitia TANROADS with its CEO Mrema.......trust me ujinga/upumbavu wa huyu jamaa kwenye procurement.....unaingiza hasara kubwa sana Taifa.......one could argue that...procurement inafanywa as a team.......but check decision za Mrema zinavyo-lead kwenye hizo procurements!!!.......ni balaa tupu
 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,

Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?


Kwa vile JK siyo Mungu, nakushauri ukubaliane fundisho la mtume Thomas katika biblia: "Unless I see the nail marks in his hands and put my finger where the nails were, and put my hand into his side, I will not believe it." (John 20:24)
 
Hivi hawa jamaa wakati wanapanga kuiba hizo fedha walijua kuwa ni Bilioni 221?

Najiuliza katika Tanzania hiyo mtu unawezaje kufikiria kuiba Dola Mil 221..!!!
 
Ex-BoT bosses in court over 221bn/- loss
BETTY BHOKE
Daily News; Tuesday,January 27, 2009 @20:03


Source: Tanzania Standard Newspapers|Home

I swear something needs to be done about the quality of journalism in TZ.
 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,

Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?

Kesi inafikishwa mahakamani mwaka wa nne tangu aingie madarakani, kama siyo lege lege nini!!!!? Alidhani haya yatasahaulika maana huko nyuma Watanzania tulikuwa hatuna tabia ya kupigia kelele na kufuatilia maovu chungu nzima ndani ya serikali na mashirika yetu ambayo yanaifanya nchi yetu kutopiga hatua yoyote ile kimaendeleo. Baada ya kuona kwamba Watanzania wa leo ni tofauti na wale wa mwaka 47 basi imebidi aachie sheria ifuate mkondo wake, vinginevyo haya yote ya BoT, EPA, Meremeta, Mikataba ya dhahabu, Kiwira na mengineyo yangeshasahaulika. Umesahau kauli yake ya "Mwacheni Mzee wetu astaafu kwa amani"? Angetaka kustaafu kwa amani basi angefuata maadili ya uongozi na kuhakikisha analinda mali na rasilimali za Watanzania siyo kuwa mstari wa mbele kutufisadi.

Alutta Continua!
 

Mkuu Field Marshall ES,

Nakushukuru kunisaidia kujibu hoja za wale wanaona ambayo wengine hatuyaoni... ati Mkuu wa Nchi ndiye Jaji pia, na Ndio Hakimu pale... Kisutu... ati mpaka wafungwe watuhumiwa wote ndio serikali itakuwa imefanya kazi.

Ndio wale wanaosema uchaguzi huru na haki ni pale chama pinzani kinaposhinda tu... Tarime uchaguzi ulikuwa huru, Mbeya vijijini uchaguzi umeibiwa, daftari la kudumu la wapiga kura lina mapungufu, as if hili daftari limeandikishwa juzi, wakati lilikuwepo muda mrefu si wangefuatilia.


Ndio wale wanawapa kichwa CUF kwamba waende mahakamani kusema uchaguzi umeibiwa kura... si wakishinda mahakamani si watarudi kupigiwa kura tena,,, je watashinda...
Hivi wananchi wa tanzania ni wajinga kiasi gani? kuchagua watu ambao wanapatikana wakati wa uchaguzi tu.

Tanzania yetu inasikitisha... nijuavyo mimi upande wa Serikali umekamilisha... si cheo cha Felesi kiko kikatiba in fact haitwi yuko ndani ya Serikali. Maana ana uhuru wa kukataa au kupeleka jambo mahakamani kulingana na anavyoona... ndio maana Hakumpeleka faili la Karamagi.
 
Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu

Chanzo: List of Shame - Orodha ya Mafisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…