Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,215
- 3,076
Mkuu mtindio yaani hii ya Liumba na mimi inanipa shida sana kuamini na akam ni hivyo ndivyo BOT inavyoendeshwa basi kuna haja ya kutengua the whole BOT uongozi na kuleta consultant hapo (ulaji mwingine.. lol) atutengeneee tructure ya kueleweka!!!!!
...maamuzi yoyote ya Bodi yanapewa baraka na Bodi Nzima ya Wakurugenzi. Bodi yoyote ni 'colegial' body na kama kuna makosa kwa pamoja bodi yote inapaswa kuwa mshukiwa.
Swali la kujiuliza, kwa nini bodi ya BOT ambayo ndo yenye dhamana ya uongozi isishtakiwe kwa kulitia hasara taifa?
Kwa tabia ya mswahili pesa yote ile, inawezakuwa ilisha kwenye matanuzi.
No investments.Mahakama inapo demand bail amount kama hiyo ya 50%,hapo ndipo majuto yanapoanzia.If what is said is true,kwamba huyo Liyumba alikuwa na maisha ya HOVYO,basi ataozea huko mahabusu.
SOMO HILO WAKULU.
Comrade Mpayukaji
Re: Liumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu
Ama kweli ukishangaa ya Musa utaona ya firauni!!! Mbona Rais mstaafu wamemwacha kwenye hili la Twin Towers?
Invisible
Kwa sasa ishakuwa ngumu. Wamepelekwa Keko kwani bail yao ilikuwa ni nusu ya kiwango kinachoaminiwa kuibiwa (Bilioni 221).
Vogue ya Liumba ameiacha pale PCCB[/QUOTE
Yaani hii nchi yetu ni tajiri wa kutupwa! Kabisa, anayebisha mwache abishe! Haiwezekani mabilioni yote hayo yakwapuliwe- EPA akaunti moja tu ya BoT tena kwa mwaka mmoja tu2005 (tena hiyo ni sample katika ukaguzi wa Ernst and Young, wangefanya in datails zingekuwa pesa nyingi zaidi), Twin Tower plus yale tusiyoyajua. Hii ni aibu kubwa kwa Rais Mstaafu na nathubutu kusema kuwa kwa kweli hakusaidia ila alijisaidia mwenyewe na kuwawekea mizizi mirefu Mafisadi. Nataka kuamini kuwa ni shemu ndogo mno ya pesa za Serikali na Wafadhili hutumika ipasavyo.
]Kuna haja ya ku-revisit the foundations of this nation na kuona ni wapi tulienda wrong. Siku zote tumekuwa tukibeza corruption ktk Nigeria lakini kumbe na sisi wamo kwa sana tu. Hata ile taasisi ya kuhunguza/ kuevaluate ufisadi TI - Tranparency international nadhani imekaa kimazabe mazabe tu si walituambia kama miaka mitatu iliyopita kwamba ufisadi umepungua mno nchi hii!!!!!!!
You are quite right Nyambala, tunahitaji Kiongozi Mwingi mabaye atakuwa Mwasisi wa Maendeleo ya Tanzania, kabisa!
Haya hizo hapo sehemu ya mashitaka yenyewe.
Nina maoni ambayo nahitaji wanasheria wanisaidie. Shitaka la kwanza linasema Liyumba alifanya uamuzi bila kuishirikisha bodi, mashitaka yanayofuatia wanaambiwa waliipotosha bodi iliyofanya uamuzi wa kutoa fedha hizo. Sasa shitaka la tatu linalifuta la kwanza kwa kuwa kama waliipotosha bodi ikafanya maamuzi ina maana kwamba waliishirikisha bodi.
Hoja ya pili ni kwamba kwa mashitaka haya ina maana kwamba watendaji wote watashitakiwa kwa makosa ya uamuzi wa bodi zao na kwamba bodi itasifiwa tu kwa mambo mazuri mabaya waachiwe wenyewe.
Hapa si kwamba Liyumba na mwenzake ni safi sana katika hili lakini ni kwamba wote walihusika na hapa hakuna cha bodi wala watumishi wa idara husika, wote wezi
hahaha Simon hizo nyingine ni chachandu yaani mashuka mekundu? Mlijuaje? na je alikuwa akiingia gust anaagiza kabisa mashuk aya rangi hiyo au alikuwa anatembea nayo garini ili akifika tu chumbani anatandika?... ah kama mchawi basi!!!Huyu si ndiye yule aliwahi kuzungumzwa na mmojawapo wa viongozi wa juu nchi hii siku ya ukimwi duniani kuwa akiwanunulia visichana magari mekundu, nguo nyekundu na kufanyia mapenzi kwenye shuka nyekundu and of course akiwalipa noti nyekundu nyekundu za 10 thousand? SI ndiye huyu? Huyu hakuhusika na kusimamia ujenzi wa twin towers huyu? Jamaa mbwembwe na maringo mengi sana akitembea mabega juu. Yuko mwingine pia alihusika na kuileta Net Group Solutions pale TANESCO akishirikiana na shemeji wa kigogo mmoja wa awamu ya tatu. Naye alikuwa anapiga maji sana kwam vile fedha ilikuwepo mpaka maini yakaungua na figo kujaa mawe. Kufuru ya fedha na ufisadi. We acha. Kweli malipo ni hapa hapa duniani.
unakosea... jana hiyo hiyo on the spot liyumba alitoa nyaraka za mali yenye thamani ya bilion 55 na kwa sasa ni uhakiki tu wa mahakama unafanyika atatoka saa yeyote kuanzia sasa!!!! UKWASI HUO TUNAITA
Hivi Ballali yuko wapi?yeye atakuwa anajua vizuri sana kuhusuina na haya.Hata kama tulizugwa amekufa si aliacha ushahidi kwa Mwanasheria wake?
Mie haingii akilini kuwa BOT walitumia zaidi ya billioni 221 bila ya ofisi hizi kufahamu.
1.Wizara ya fedha
2.Gavana wa Benki Kuu
3.Katibu Mkuu Kiongozi
4.Wakurugunzi wa bodi ya BOT
5.OFISI ya CAG
Umesahau, na OFISI YA RAIS
Mkuu mtindio yaani hii ya Liumba na mimi inanipa shida sana kuamini na akam ni hivyo ndivyo BOT inavyoendeshwa basi kuna haja ya kutengua the whole BOT uongozi na kuleta consultant hapo (ulaji mwingine.. lol) atutengeneee tructure ya kueleweka!!!!!
Hawa jamaa si wataifishiwe mali zao tu kieleweke.
Mtu kala bilioni 200 na usheee duh akimpa hakimu bilioni 1 itakuwaje hapo agawane na wenzake.