JF Member
JF-Expert Member
- Dec 14, 2014
- 7,914
- 10,793
Nashauri kama hari ndio hii basi vyuo visiwe vinafunguliwa hadi pale Loan Board inapokamilisha ugawaji wa mikopo na kuhakikisha kila anayestahili kupata amepata na kisha kutangaza kufunga dirisha la kupanga mikopo.
Wanafunzi wanateseka hawajapewa mikopo/accommodation huku masomo yameshaanza, yaani watoto wa masikini wako chuo hawajui watakula nini, wana tembea tembea tu na kuomba omba kwa watu. Mtoto ametoka Kigoma/Bukoba/Katavi/Mara/Songea kaja hapa Dar hajui anakula nini. Huu ni unyanyasaji.
Kuna wengine wameshindwa kutoka nyumbani kwenda vyuoni wakisubiri uhakika wa loan board iwapo itawapangia mikopo ama lah. Wengine wako radhi kuahirisha mwaka wasubiri Loan Board iwapangie mikopo.
Ushauri kwa Serikali: Databae ya wanafunzi wanaomaliza form six mnazo mapema kabisa. Fanyeni mpango muwape mikopo wote ama mshushe ada ili watoto wajilipie kama ilivyo kwa form six. Punguzeni ubaguzi kwenye Elimu.