Loan Board mnatutesea Watoto. Jitahidini kwenda na muda

Sina maisha safi maana hata bodaboda similiki ila nina dhamira ya kuhakikisha watoto wangu wanasoma kwa kuungaunga na sio kulialia. Nakosea?
Hukosei boss lakini unapofanikiwa wewe kuweza kufanya kitu fulani usidharau au kubeza walioshindwa boss.
 
Duh! Hivi una akili kweli?? Moja ya jukumu la Serikali,nikuwapa watu wake Elimu,ili walisaidie Taifa lao kwenda mbele! Sasa unataka watu wenye Elimu watoke nje ya taifa ndiyo waje watusaidie kweli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma maelezo yangu kwa niliowajibu utaona mantiki yangu Ila sio lazima ukubaliane nayo.
 
Vuteni subira.. Next time mmje na fedha za kuwasukuma walau three weeks..
 
Duh! Hivi una akili kweli?? Moja ya jukumu la Serikali,nikuwapa watu wake Elimu,ili walisaidie Taifa lao kwenda mbele! Sasa unataka watu wenye Elimu watoke nje ya taifa ndiyo waje watusaidie kweli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mzee haelewi hata anachoongea, hajui asilimia kubwa ya vigogo waliosoma kipindi cha Nyerere walitoka familia duni huko vijijini hawakuwa hata na uwezo wa kulipa hata nauli kwenda shule, walisafirishwa bure, kusoma bure hadi nje ya nchi serikali ililipa.......serikali ingekuwa na mawazo kama ya huyu mzee, hii nchi leo hii ingekuwa imejaa vilaza kila kona.
 
Kwakweli ni mateso makubwa sana kuna mdogo wangu nimemshauri aende veta tu maana mkopo hawajampa,chuo wamempangia mbeya,ovyo kweli
 
Duh! Kwa hiyo Private hawana sifa zakupewa loan, hivi unadhani loan board ilianzishwa special kwa ajiri ya Public University Students only??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipindi cha nyuma kabla ya kuanzisha loan board serikali ilikuwa inatoa ufadhili kwa wanafunzi waliokuwa wamedahiliwa kwenye vyuo vikuu vya umma kama UDSM, SUA na Mzumbe........waliokuwa wanaenda vyuo vya binafsi walikuwa wanajilipia, kwa hiyo ni logical kusema kwamba serikali ijikite kuelimisha watu kupitia vyuo vyake yenyewe na watakuwa na uwezo wa kuongeza udahili kulingana na bajeti waliyo nayo.....kuliko hivi sasa wanavyohangaika.
 
Hivi loan board wenyewe,wakiona majina ya watoto wa wanene,ndiyo kwanza wanawapa mikopo! Wakati baba zao wanauwezo wakulipa ada na mazaga mengine yote

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao maofisa wanaofanya hivyo ni washamba! Kuna Prof. mmoja akitoa lecture siku moja akatueleza ya kwamba alishangaa sana kuona jina la mwanae lipo kwenye orodha ya wanafunzi watakaopewa mkopo!
 
Hao maofisa wanaofanya hivyo ni washamba! Kuna Prof. mmoja akitoa lecture siku moja akatueleza ya kwamba alishangaa sana kuona jina la mwanae lipo kwenye orodha ya wanafunzi watakaopewa mkopo!
Huyo Prof nae, kwani hadi mtoto wake apewe mkopo si anaomba na kujaza fomu na mdhamini ambae ni mzazi nae anasign, sasa huyo Prof anashangaa nini
 
Huyo Prof nae, kwani hadi mtoto wake apewe mkopo si anaomba na kujaza fomu na mdhamini ambae ni mzazi nae anasign, sasa huyo Prof anashangaa nini
Mkuu achana na hawa watoto. Kwani Bodi wanaijua sahihi ya Baba? Mtoto anaweza ingia kozi ya mwezi kuiga sahihi ya Mdingi! Achana nao hao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…