Loan Calculator ya HESLB ina kasoro gani? Huyu mnufaika Loan Board anadaiwa mkopo wa karibu Bilioni 48!

Taifa linakusanya kodi kutoka kwa wananchi kisha inawakopesha kodi hizo hizo kuwasomesha wananchi halafu inawadai na riba kubwa.. yaani pesa zako mwenyewe unakopeshwa

Marejesho yameongezeka kutoka bil 2 Hadi bil 16.... Kwa wizi huu marejesho lazma yaongezeke...
 
Walishakanusha wakasema kuwa figures zinazoandikwa kwenye salary slip si za kwao.

Waajiri wanajiwekea figure tu ila ukitaka kujua kiasi halisi cha deni wasiliana nao
Tatizo ni kwamba hata kama hiyo figure imewekwa kwa makosa, mfumo wa lawson unaendelea kukata hadi isomeke zero, na hela zinaenda huko huko HESLB wanakokanusha
 
Jamaa deni lake kama taasisi kubwa inadaiwa, so sad!
Body ya mikopo hainipati ng'o...natamba nimesoma bure sirudishi hata senti.
Unalipia kuomba mkopo, unakosa, una-appeal, unapata tena kwenye batch ya mwisho alaf kirahis wanataka kukata mshahara wa mtu.... hahahaha hii haipo aisee

TutasumbuanaTu Hakuna namna
 
Kama mwenye deni 4.5m kwenye salary slip deni halisi heslb Ni 12m, je mwenye 48bn si litasoma 123 trillions?
 
Pamoja na majibu mazuri ya wahusika hapo HESLB, je ule mpango wa kuweka picha za wadaiwa sugu bado upo pale pale au la? Hilo mimi naliona kama udhalilishaji wa aina fulani vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…