Hii ndio Tanzania, amani iwe nanyi !
Napendekeza tuwe na kitu kinachoitwa "LOCAL TRANSPORT CARD". Hii iwe kadi maalumu itakayo jazwa pesa kupitia mifumo ya kifedha ya hapa hapa nchini (Local Banks, Mpesa, Tigo Pesa, Z-pesa, Airtel Money Halopesa nk) na kutumika kwake iwe kwa scan pekee katika kutoa pesa kwenda kwenye vyombo husika (Magari au Kampuni ya Usafiri wa Umma).
Hii kadi (LTC) itumike katika vyombo vyote vya Usafiri wa Umma hapa nchini kuanzia Bodaboda, Bajaji, Daladala na Mabasi ya Mikoani.
1. Kwa kupitia njia hii itapunguza sana usumbufu katika usafiri wa Umma kuanzia Bodaboda, Bajaji, Daladala, Mabasi ya kwenda mikoani.
2. Tutakuwa tumeondoa kabisa changamoto ya usumbufu kwa mwananchi kutembea na fedha nyingi atakapo kusafiri.
3. Tutaimarisha Usalama wa nchi kwa Serikali, Abiria na Wamiliki wa vyombo vya Usafiri.
4. TRA mtakusanya mapato yenu kwa njia rahisi sana sambamba na nyie halmashauri husika mliopo maeneo husika.
5. Tutakuwa watu waliostaarabika, tutalindana utu wetu na tutajipatia maendeleo kwa haraka.
NB
Local Transport Card (LTC) ni njia salama na sahihi kwa usafiri wa umma hapa nchini.
(Pia kwa kutumia tu mfano; Ikapendekezwa Tsh.10,000/= iwekwe kama kifungua akaunti na fedha hii haitarudishwa kabisa na abiria anapaswa awe na akiba isiyopungua kiasi flani kwenye akaunti yake ya kadi; kwa idadi ya watu milioni 40, unahisi sekta ya usafiri itajikusanyia mapato kiasi gani?, tuchukue hatua.)
Cc
TRA
LATRA
National Institute of Transport (NIT)
Dar es Salaam Institute of Technology (DIT)
Wizara ya Uchukuzi
TAMISEMI
Ofisi ya Waziri Mkuu
Ofisi ya Raisi
Karibu.