Local Transport Card: Hii itumike nchini pekee

Achana na mambo ya kutumia simu kufanya malipo. Yaani malipo yote yanayohusu Usafiri wa Umma yawe kwa njia ya CARD tu. Mtoa huduma yeye anapaswa kuwa na kifaa cha kuscan ambacho hakiitaji INTERNET.
 
Tukubaliane tu. Hii itaondoa hizo changamoto. Unajua wawekezaji wanashindwa kuwekeza hususani sekta ya Usafiri wa umma sababu hakuna Data zinazoeleweka na kuaminika.

Kwa kupitia LTC (Local Transport Card) itavutiwa wawekezaji kwa uzuri na usawa.
 
Wataweza tu. Unajua mwanzo huwa mgumu.
Swali jepesi, unaweza vipi kufanya mawasiliano kwa njia ya simu pasipo Simu Card na Simu Kifaa. Hii ndio kitatakiwa kiwapate hao maafisa Usafirishaji.
Ninakutakia kila la kheri.
 
Wizara ya Uchukuzi ni lini sasa mtaanza huu mchakato wa kupunguza kero za usafiri kwa Umma hapa nchini!?
 
Hii tutafanikiwa kwa usahihi kama tutakuwa tunaipenda nchi yetu na tunaiwazia mema usiku na mchana.
Asante.
 
Ni wazo zuri sana ila Napendekeza huo mfumo usitengenezwe na wazawa na wala usisimamiwe na wazawa mifumo mingi iliyo tengenezwa na wazawa ni kichefuchefu sana katika ufanisi wake

Unaweza kukuta mnapanga foleni masa mawili ku swap kadi kwenye mashine na mtandao unasumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…