Locations zenye idadi kubwa ya watu Dar

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
4,411
Reaction score
6,473
Habari za muda huu wana jamii forum

Nahitaji mnisaidie tafadhalini,

Ninataka kuwa wakala, ila nataka sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu hapa Dar es salaam, yani yenye muingiliano wa watu ili nifungue uwakala wa pesa, kama m pesa, tigo pesa, airtel money, pia uwakala wa benk.

Sehemu nayohitaji napenda fremu nitakayoipata iwe kubwa maana nataka kuweka partition za vyumba vidogo dogo ili kila mteja ahudumiwe kwa nafasi, bajeti yangu ya fremu ni kuanzia 200k-500k,,,, Naomba kwa anaejua anisaidie location hiyo, zawadi ya shukurani itatolewa

NATANGULIZA SHUKRANI
 
kariakoo ni poa, ila kupata fremu kwa bajeti ya laki mbili hadi tano ni ishu
Zipo mkuu, ni zile zinakua attached kwenye 'main structure'. Inakua sio frame in such, ni kama kibanda fulani. Mfano ule mtaa wa kuuza vipodozi kuna frame kibanda cha mpesa kodi laki mbili.
 
Kariakoo
Mbagala
Tegeta
Buguruni
Ubungo
Mbezi Mwisho
Gongo la Mboto
 
Sehem yoyote ambayo mji unachipuka km vile kigamboni, tegeta, kongowe panafaa cha msingi uangalie usalama kwanza maana mtu anaweza kuja kukuvamia na kukuua kukuibia elfu 50 tu
 
Zipo mkuu, ni zile zinakua attached kwenye 'main structure'. Inakua sio frame in such, ni kama kibanda fulani. Mfano ule mtaa wa kuuza vipodozi kuna frame kibanda cha mpesa kodi laki mbili.
asante mkuu
 
Huku kwetu Usangi Bank hamna kuna jamaa anapiga hela kinoma anauza umeme, vocha, huduma zote za pesa, ni wakala wa bank maarufu mwisho wa mwezi wafanyakazi na wastaafu wanapanga foleni. Jaribu kufikria nje ya mji.
 
usangi ya mkoa gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…