Ndg zangu wamasai poleni sana kwa yanayowakuta kumbukeni si nyie peke yenu mnaonyanya kwa kunyan'ganya Ardhi yenu mliokuwa mnaitegemea kwa kuendeshea maisha yenu ya kila siku
Jueni kuwa sehemu kubwa ya ardhi yenye mabonde mazuri yanayofaa kwa kilimo serikali ya CCM walishawauzia MAKABAILA ambao Mwalimu JK Nyerere aliupinga kwa nguvu zote ili wananchi wa kawaida waishi kwa UHURU ktk nchi yao
Leo nchi hii imegawanwa kila sehemu wananchi wanalia, Angalia Loliondo, Karangwe ,Mbeya, Mpanda, Kibaigwa,Musoma,Geita, Nyarugusu, Urambo, Nyamongo,Nzega,Tanga na sehemu nyingine nyingi tu ambazo Watanzania wanalia kwa uwekezaji usio na faida na wananchi wa kawaida
Watanzania leo hii wanalia sana bila kujua wao wakiwa chanzo kimojawapo cha matatizo haya ambayo kwa baadae yatakuwa zaidi ya haya, kwani nadiriki kusema hivi kwa sababu
1.Wakati Mzee Mwinyi anauza mashamba haya ya Loliondo Augustine Lyatonga Mrema aliuweka wazi ufisadi huu na Watanzania walikaa kimya wakamwona Mrema mwehu,propaganda hii ya Wehu wa Mrema ilisambazwa kwa kasi ya ajabu na CCM mara Mrema havui kofia ana matatizo kichwani Watz wengi waliamini utoto huu wa CCM wakasahau kushughulikia matatizo yao ya msingi ambayo walitakiwa kuyafanya
2.Kama kawaida baada ya kupewa nchi Mkapa aliendeleza yale yale ya kuwamilikisha wageni ardhi kwa nguvu zote na baada ya kuona ardhi inaisha hatimaye viongozi CCM walianza na wao kujimilikisha ardhi kwa majina bandia mf: Mkapa anamiliki ardhi Mtwara zaidi ya ekari 1000
Sumaye pia alijimilikisha ekari nyingi Kibaigwa kwa mgongo wa wawekezaji na Lowasa hivyo hivyo
Hiyo ni mifano michache sana kwa mambo yanayofanywa na serikali chini ya CCM na bado Watz hawataki kusadiki haya na wakati tabu wanaiona kabisa na si ya kusimuliwa
Huu ujinga tulionao madhara yake ndo haya tunayaona leo hii na sio muda murefu tutaambiawa Watanzania wote sio raia halali wa nchi hii tutafute nchi yetu halisi na tutakubali tu ndipo labda tutashtuka
Ufisadi huu umeshapelekwa mara kadhaa BUNGENI lakini wabunge wetu waliowengi wanautetea mf: Bunge la mwaka jana Waziri mkuu alihusishwa moja kwa moja na uuzwaji wa ardhi ya Mpanda kule Katumba kwa sh70 tu ya Kitz kwa kila ekari na Wabunge wengi ambao ni wa CCM walipinga vika ispokuwa Filikunjombe peke yake ambaye alisimama upande wa wananchi hii inasikitisha sana
Kwa haya yanayotokea leo tusíilaumu serikali yetu tuliyoiweka kwa ridhaa yetu wenyewe tujilaumu sisi wenyewe kwa moja au nyingine kuiruhusu CCM kuendelea kutawala