#COVID19 London: Maelfu waandamana dhidi ya chanjo ya Corona, uvaaji wa barakoa na lockdown

#COVID19 London: Maelfu waandamana dhidi ya chanjo ya Corona, uvaaji wa barakoa na lockdown

Ifike mahali dunia ione huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine so watu waruhusiwe kwenda watakapo Ili maisha yaendelee tutakaa hivi mpaka lini?
Corona ni mambo ya siasa zaidi kwenye Uchumi yule anaetaka kusafiri apate chanjo aende atakako tumechokaaa
Kama unajichanganya, ni ugonjwa kama magonjwa mengine, Au ni mambo ya siasa?!
 
Hakuna kitu kama hicho. Leo uingereza wametangaza maambukizi yanaongezeka na wanasema kabisa chanjo haizuii maambukizi ila eti inapunguza watakaolazwa hospitali kwa kuzidiwa. Wakati hata bila chanjo imedhihirika wengi hupo a bila dawa yoyote na wanaolazwa kwa kuzidiwa ni asilimia ndogo sana ya walioambukizwa hata bila chanjo. Kama ni kuangalia mpira huko ulaya kwani sisi hatuangalii?
Umemjibu vizuri, wachangiaji wengi kuhusu haya mambo ya Chanjo wanaongozwa na chuki dhidi ya Magufuli, sio kitu kingine. Hakunaga kitu kizuri chenye proves kama Sayansi, sayansi haidanganyi. Kwenye issues za corona, mwendazake nampa tano, nampa 100%; yule mwamba alisoma Sayansi na akaielewa na sayansi ilimuelewa. Kuna uongo mwingi sana kwenye haya mambo ya corona, watu wametengeneza tatizo ili watajirike. Jana Uganda wamegundulika wanazika majeneza yasiokua na watu, imagine, unamdanganya nani na ili iwaje? RIP JPM, kwa mambo ya corona, nilikukubali sana mjomba.
 
Upinzani dhidi ya chanjo ya corona ñi mkubwa mno huko nchi za magharibi japo serikali zao huwa hazitangazi. Angalia maelfu wanavyoandamana mjini London. Huko watu wengi wamechanjwa na madhara yake wameyashuhudià. Halafu hapa anatokea mtu na kudai hakuna madhara!


Wajinga wako kila kona sio Ulaya tu.
 
Back
Top Bottom