London Marathon 2019: Eliud Kipchoge aibuka mshindi

London Marathon 2019: Eliud Kipchoge aibuka mshindi

Gwizzy

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2018
Posts
629
Reaction score
854
As ya'll heckle here about SGR, parachichi, China bla bla bla. London Marathon is trending in Kenya.
1083225
All the best to our athletes who are doing battle in London!!!!
1083226
1083224

=========================
Mwanariadha mashuhuri na mshindi wa mbio za Olympiki duniani Eliud Kipchoge ameshinda tena mbio za London Marathon 2019, kwa mara ya nne mfululizo.

Kipchoge raia wa Kenya, 34, ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin 2018, alikamilisha mbio za Jumapili kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thelathini na nane (2: 02: 38.) zilizofanyika katika mji mkuu wa Uingereza.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Kipchoge aliwabwaga wanariadha Mosinet Geremew na Mule Wasihun raia wa Ethiopia ambao waliweza kumaliza mbio hizo katika nafasi ya pili na ya tatu.

Hata hivyo Kipchoge ambaye alishinda mwaka 2015, 2016 and 2018 mbio hizo za Marathon, hakuweza kuipiku rekodi yake ya Dunia ya sekunde 59 ambayo ilikuwa 2:01:39 aliyokuwa ameiweka katika shindano la mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza Mo Farah, raia wa Uingereza alichukuwa nafasi ya tano baada ya kumaliza dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Callum Hawkins kutoka Uingereza akimaliza katika nafasi ya 10.

Pia imesema kuwa Brigid Kosgei, 25, raia wa Kenya alishinda mbio hizo upande wa wanawake na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon.

Mwengine ni Kosgei aliyeweza kumshinda bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kwa kutumia mda wa saa 2:18:20 kushinda mbio hizo kwa mara ya kwanza.

Imeongeza kuwa Mkenya Vivian Cheruiyot alichukua nafasi ya pili huku Roza Dereje wa Ethiopia akimaliza wa tatu. Muingereza Charlotte Purdue alimaliza nafasi ya 10.

Voa
 
Hivi inakuwaje hao wakimbiaji wote wana majina ya kilugha, ila huoni wenyewe majina ya kikristo au ya kiislam? ( achilia mambo ya dini).

Kiprochech, kipchoge,kosgei....is it one of the requirement uwe na jina la kilugha?

But I like it, huwa nawaza mfano mie ningekuwa kinara wa kuogelea kwenye mashindano au tennis, mnanisoma Kasinde from Tanzania.... Yeey.
 
Hivi inakuwaje hao wakimbiaji wote wana majina ya kilugha, ila huoni wenyewe majina ya kikristo au ya kiislam? ( achilia mambo ya dini).

Kiprochech, kipchoge,kosgei....is it one of the requirement Uwe na kina la kilugha?

But I like it, huwa nawaza mfano Mie ningekuwa kinara wa kuogelea kwenye mashindano at tennis, mnanisoma Kasinde from Tanzania.... Yeey.
They use their Sir names All of them have got first English names
 
Hivi inakuwaje hao wakimbiaji wote wana majina ya kilugha, ila huoni wenyewe majina ya kikristo au ya kiislam? ( achilia mambo ya dini).

Kiprochech, kipchoge,kosgei....is it one of the requirement Uwe na kina la kilugha?

But I like it, huwa nawaza mfano Mie ningekuwa kinara wa kuogelea kwenye mashindano at tennis, mnanisoma Kasinde from Tanzania.... Yeey.
wenye majina ya kidhungu/kiarabu hawawezi kukimbia...hao wenye asili yao ndio wamefuzu.

ujiunge kikosi cha kuogelea sasa homie...
 
Kipchoge finished in 2hours 2minutes, meaning he has unlocked the prize money for finishing under 2hours 5 minutes............ Total take home for the champ $ 155,000 that is approximately KShs 15,500,000 (TZS 341,000,000)..... Na bado sijaongeza endorsments
 
Back
Top Bottom