Sijui kwanini?
Ila bandiko lako limenigusa sana mkuu...
Japo sijui nini hasa nikushauri, ila kitu pekee na bora kwako kwa mda huo ni kuamini kuwa wewe ndio chanzo cha furaha yako....
Kuwa busy na kazi zako, take care of ur family, kitu pekee nlchojifunza kwenye maisha ya upweke ni kuwa hupangi "kufall in love"
ila unatembea katika barabara yako ni lazima tu atatokea mtu mtakayependana......
Narudia tena ni lazima (labda utaona umechelewa, ila ni lazima atokee).
So hamna sababu ya wewe kujiona mnyonge wala vipi japo kweli upweke unayumbisha sana.
Hasara ya kujitwisha zigo kutafuta mtu ni kuwa unaishi maisha yasiyo yako ili kumshawishi huyo unayemuwinda hivyo hata ukimpata, matokeo yake ni kuishi maisha ya msalaba zaidi ili kumfurahisha huyo.... Je hayo ndio maisha unayoyataka?
Afu pia kwa afya unahitaji mtu atakayekupenda zaidi!
So, hamna ulichopoteza haijalishi umepitia nini?
Kuwa na furaha yako hyo ndio funguo ya kila kitu.
Usimsahau Mungu katika hilo zoezi.