loneliness is killing me softly

loneliness is killing me softly

Desteo

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
494
Reaction score
123
Sihitaji mada yangu ihamishiwe kule love connect. Hapa inatosha. Kimsingi upweke unanitafuna sana. Katika umri wangu wa miaka 34 sijawahi kuwa na mwenza niseme huyu ni wangu japo kwa mwaka. Kipindi kirefu pia niko singo. Najua kuna makosa kadhaa ya kiufundi nimeyafanya huko nyuma ambayo kwa namna fulani yananigharimu. Kimsingi napenda sasa kuwa na mwanamke wa kuishi naye niweze kumwita mke. Ajabu sijui kwa nini sina access na wanawake kama ilivyokuwa awali. Tunaweza kushea changamoto kama hizi ambazo najua siko peke yangu.
 
mmmh.you are not alone,ila nina amini maybe hujawa tayari.kama m.me mbona ni rahisi kupata mwenza?hutoki toki?
 
MKuu gear unayotumia kwenye tope la JF haifai tumia gear kubwa ya land cruiser siyo ya bajaj utatoka kapa hapa JF nijumba la sanaa usilete usanii!!
 
Pole mwaya,muombe mungu na uchanganye na watu hasa kwenye ocation mbalimbali,jiweke kwenye muonekano wa kuwa baba wa familia na co mtumiaji tu,tambua ni aina gani ya mke ungependa kuwa naye na kujitahidi kujenga ukaribu na urafiki kwa mainti wa cfa utakazo,epuka kutumia fedha km kigezo cha ushawishi,majigambo na kujikweza havitakusaidia kubwa zaidi kuwa makin na matumizi ya ulimi wako hasa namna unavojieleza kwa wahusika kwan ulimi pekee ni silaha tosha km unatoa mistari yakueleweka!
 
Pole sana. sasa hayo makosa ya kiufundi ulifanya huko nyuma, umesha acha na kujifunza namna ya kuendelea bila kuyafanya tena?
 
Sijui kwanini?
Ila bandiko lako limenigusa sana mkuu...
Japo sijui nini hasa nikushauri, ila kitu pekee na bora kwako kwa mda huo ni kuamini kuwa wewe ndio chanzo cha furaha yako....
Kuwa busy na kazi zako, take care of ur family, kitu pekee nlchojifunza kwenye maisha ya upweke ni kuwa hupangi "kufall in love"
ila unatembea katika barabara yako ni lazima tu atatokea mtu mtakayependana......
Narudia tena ni lazima (labda utaona umechelewa, ila ni lazima atokee).
So hamna sababu ya wewe kujiona mnyonge wala vipi japo kweli upweke unayumbisha sana.
Hasara ya kujitwisha zigo kutafuta mtu ni kuwa unaishi maisha yasiyo yako ili kumshawishi huyo unayemuwinda hivyo hata ukimpata, matokeo yake ni kuishi maisha ya msalaba zaidi ili kumfurahisha huyo.... Je hayo ndio maisha unayoyataka?
Afu pia kwa afya unahitaji mtu atakayekupenda zaidi!
So, hamna ulichopoteza haijalishi umepitia nini?
Kuwa na furaha yako hyo ndio funguo ya kila kitu.
Usimsahau Mungu katika hilo zoezi.
 
Pole mwaya,muombe mungu na uchanganye na watu hasa kwenye ocation mbalimbali,jiweke kwenye muonekano wa kuwa baba wa familia na co mtumiaji tu,tambua ni aina gani ya mke ungependa kuwa naye na kujitahidi kujenga ukaribu na urafiki kwa mainti wa cfa utakazo,epuka kutumia fedha km kigezo cha ushawishi,majigambo na kujikweza havitakusaidia kubwa zaidi kuwa makin na matumizi ya ulimi wako hasa namna unavojieleza kwa wahusika kwan ulimi pekee ni silaha tosha km unatoa mistari yakueleweka!
ukimpenda utamlinda,
ukimwonea huruma utamPM!
 
Sijui kwanini?
Ila bandiko lako limenigusa sana mkuu...
Japo sijui nini hasa nikushauri, ila kitu pekee na bora kwako kwa mda huo ni kuamini kuwa wewe ndio chanzo cha furaha yako....
Kuwa busy na kazi zako, take care of ur family, kitu pekee nlchojifunza kwenye maisha ya upweke ni kuwa hupangi "kufall in love"
ila unatembea katika barabara yako ni lazima tu atatokea mtu mtakayependana......
Narudia tena ni lazima (labda utaona umechelewa, ila ni lazima atokee).
So hamna sababu ya wewe kujiona mnyonge wala vipi japo kweli upweke unayumbisha sana.
Hasara ya kujitwisha zigo kutafuta mtu ni kuwa unaishi maisha yasiyo yako ili kumshawishi huyo unayemuwinda hivyo hata ukimpata, matokeo yake ni kuishi maisha ya msalaba zaidi ili kumfurahisha huyo.... Je hayo ndio maisha unayoyataka?
Afu pia kwa afya unahitaji mtu atakayekupenda zaidi!
So, hamna ulichopoteza haijalishi umepitia nini?
Kuwa na furaha yako hyo ndio funguo ya kila kitu.
Usimsahau Mungu katika hilo zoezi.

kwa niaba ya wote naomba kujibia hapa. Thank u man for your empathy. kiukweli ni ngumu kuona kuwa mambo (hasa ya kimapenzi) hayaendi sawa. Naona sasa niongeze tu maombi maana inafika hatua nakereka sana kwa hali hii.
Kauli zangu naamini ni za kawaida kama za mwingine. Kigezo cha kutumia pesa sinacho. Jambo ambalo naliona sahihi kwangu kama ulivyosema ni kuona mapenzi yanakuja naturally. But when, how, who?
 
ukimpenda utamlinda,
ukimwonea huruma utamPM!

Heshima yako Bishanga,mie tayari ninaye Salvado wangu,ndio maana umeona nimemshauri tu,ila tu ackate tamaa mungu atamkutanisha na wa kufanana nae!
 
Nashukuru wadau kwa michango hii na mingine itakayokuja. Ila kiukweli mtu anapokuwa katika situation kama hii presha ya kusukuma mambo haikosekani. Wakati huu kwa mtazamo wangu na mtazamo wa kijamii ni umri ambao nilipaswa kushughulikia kipato na malezi zaidi kuliko kutafuta mke. Nahitaji mawazo zaidi ambayo yataweza kuwa ni ufunguo wa masahibu yangu haya
 
Welcome to the club, all I can say you're not alone. There things when you push too much doesn't work especially love, let it be natural, the problem is how soon if you have waited for so long, its FRUSTRATING.

Nevertheless, I am sure someone out there is meant for you and also you should know you're the ONLY person who is responsible for own happiness.
 
MKuu gear unayotumia kwenye tope la JF haifai tumia gear kubwa ya land cruiser siyo ya bajaj utatoka kapa hapa JF nijumba la sanaa usilete usanii!!

Anataka kuwaibia akina Lizzy, Preta etc. sijui kama atawakamata kwa gia hii, maana hapa JF watu wapo makini.
 
Anataka kuwaibia akina Lizzy, Preta etc. sijui kama atawakamata kwa gia hii, maana hapa JF watu wapo makini.
wapo makini kama wafanyakazi wa kwenye kinu cha nyukilia!
 
34 wala sio kiama, wengine tulipanga (20 yrs before) kuanza hayo maisha tutakapofika 35, na ikawa hivyo na hakuna kilichoharibika. Tuliza boli go slowly and carefully utavuka salama !
 
Back
Top Bottom