Desteo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 494
- 123
Sihitaji mada yangu ihamishiwe kule love connect. Hapa inatosha. Kimsingi upweke unanitafuna sana. Katika umri wangu wa miaka 34 sijawahi kuwa na mwenza niseme huyu ni wangu japo kwa mwaka. Kipindi kirefu pia niko singo. Najua kuna makosa kadhaa ya kiufundi nimeyafanya huko nyuma ambayo kwa namna fulani yananigharimu. Kimsingi napenda sasa kuwa na mwanamke wa kuishi naye niweze kumwita mke. Ajabu sijui kwa nini sina access na wanawake kama ilivyokuwa awali. Tunaweza kushea changamoto kama hizi ambazo najua siko peke yangu.