Lotion ya kupunguza unene

Lotion ya kupunguza unene

Nuraty J

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
1,729
Reaction score
3,831
Habar wana JF

Dada yangu ameletewa lotion Ya kupaka ili eti apunguze mwili, imetengenezwa ña ORFRAME sijui,, nimejaribu kumshauri asitumie nimeshindwa, ivi nikweli inapunguza mwili jamani au, naona kama anajitafutia saratani
 
Hao matapeli mwili hupungua vizuri ukifanya mazoezi, nakula chakula sahihi, nisikudaganye no shortcut ya kupungua aisee,
 
unaweza uka imagine hio reaction ikojeee, kitu upake nje tu halaf upungue unenee? Hata km ni kweli ila sio safeee,
hii ndio inanifanya niridhke tuu na u slim wang, waweza ubishe ila lkn huku mtaani wananiita magriri maana mm kwenye yale madirisha ya griri kupenya sio tabuuu
 
ORIFLAME wana bidhaa bora sana za ngozi, Comrade Mwifwa tumia bidhaa za hawa jamaa aisee siku ukikutana na mwanadada wa JF hakuachi
 
Nakumbuka nilinunuaga lotion nikaambiwa inapunguza unene na ushuhuda juu nikapewa. Kwenda kuipaka niliwashwa kama nimepaka pilipili kwa masaa mawili, sikurudia tena.
 
Nakumbuka nilinunuaga lotion nikaambiwa inapunguza unene na ushuhuda juu nikapewa. Kwenda kuipaka niliwashwa kama nimepaka pilipili kwa masaa mawili, sikurudia tena.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pole sana
 
Hao matapeli mwili hupungua vizuri ukifanya mazoezi, nakula chakula sahihi, nisikudaganye no shortcut ya kupungua aisee,
Yes...kupunguza unene hakuhitaji lotion. Maana lotion hupakwa kwenye ngozi. Kupungua unene kama ulivyoandika ni suala la mazoezi na kupunguza kula wanga na sukari kwa wingi.

Hapo mwili utajipunguza automaticaly maana mtu ananenepa kwa sababu insulin inamwagwa kwa wingi mwilini ili kudhibiti ongezeko la sukari...ile sukari inayozidi hugeuzwa kuwa mafuta na kutunzwa mwilini...matokeo yake mtu ananenenepa.

Ili mtu apungue, akipunguza wanga na sukari, insulin itatolewa kwa uchache sana, kiasi ambacho mwili utajielekeza kuunguza mafuta yaliyotunzwa mwilini kama chanzo cha nishati. Hapo unapungua uzito automaticaly bila haja ya lotion au chochote.
 
Nyie mnaonenepa huwa mnakula nini tusivyokula?

mmeenda mbali weee mkala sasa mnataka mkonde.
 
Mwambie afanye mazoezi na afanye Balance diet
Mwambie ndg yko aache uvivu hkuna kitu sjui lotion inapunguza unene zaidi ya kuambulia kansa

Ova
 
Nakumbuka nilinunuaga lotion nikaambiwa inapunguza unene na ushuhuda juu nikapewa. Kwenda kuipaka niliwashwa kama nimepaka pilipili kwa masaa mawili, sikurudia tena.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pole dia
Wanawake tuna mambo mengi.
 
Duuh! Vibonge kazi wanayo.

Ila huwa najiuliza inakuwaje mtu anajiachia mpaka anakuwa tipwa tipwa halafu baadae anataka kupungua wakati hii hali alitakiwa aichukie toka mwanzo kwa kujijali katika kula na hata kufanya mazoezi ili awe na mwili wa wastani.

Mwambie atafute wataalamu wa Afya watamshauri vizuri na atapungua tu. Aachane na madawa yenye makemikali ambayo baadae yanaweza mletea shida pia.
 
Duuh! Vibonge kazi wanayo.

Ila huwa najiuliza inakuwaje mtu anajiachia mpaka anakuwa tipwa tipwa halafu baadae anataka kupungua wakati hii hali alitakiwa aichukie toka mwanzo kwa kujijali katika kula na hata kufanya mazoezi ili awe na mwili wa wastani.
Teh...ndicho nachouliza. Wao wanakula nini kitamu wanasahau wananenepa.
 
Back
Top Bottom