Lounge zilizopo Moro mjini zinapiga sana kelele (Noise Pollution)

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Kuna mwaka nikiwah sikia Nemc walitoa tamko la swala la kumbi za starehe na mabar zifunge sound proof (vipuguza sauti na mitetemo) ktk Hizi kumbi ili kupunguza kelele ...
Sijui walifikia wapi ?

Aah nipo hapa Moro town kuna lounge inaitwa Star park inapiga mziki mkubwa mnooo yaan ni kelele tupu kwa wakazi wa karibu ....sijui hii star park inakuwaje kuwaje
 
Kesho toa copy pages ya sheria ya mazingira kisha nenda kwa mtendaji na mwemyekiti waambie usikie wanasemaje kisha nenda kwenye vyombo vya usalama uone itakuaje baad ya week uje update
 
Vumilieni tu maana huo ndiyo uwwkezaji #1 kwa wabongo..
Bar na lounge

Ova
 
Kuna mwaka nikiwah sikia Nemc walitoa tamko la swala la xkumbi za starehe na mabar zifunge sound proof (vipu guza sauti na mitetemo) ktk izi kumbi ili kupunguza kelele ...
Sijui walifikia wapi ?

Aah nipo hapa Moro town kuna lounge inaitwa Star park ina piga mziki mkubwa mnooo yaan ni kelele tupu kwa wakazi wa karibu ....sijui hii star park inakuwaje kuwaje
Ina vibe lkn mkuu? nikija niitembelee.😄
 
Maeneo hayo mbona kuna Terminal Pub Msamvu, na ukienda mbele kuna Samaki samaki pia? Au wewe umeona Star park tuu?
 
Wana mziki una fujo mnooo imagine mpaka saa hii saa tisa na dak 30 usiku mkali mziki mnene yaan usingiz hauji kbs
 
Kuna mwaka nikiwah sikia Nemc walitoa tamko la swala la xkumbi za starehe na mabar zifunge sound proof (vipu guza sauti na mitetemo) ktk izi kumbi ili kupunguza kelele ...
Sijui walifikia wapi ?

Aah nipo hapa Moro town kuna lounge inaitwa Star park ina piga mziki mkubwa mnooo yaan ni kelele tupu kwa wakazi wa karibu ....sijui hii star park inakuwaje kuwaje
Kule maeneo ya Forest kuna Bar inaitwa Black and White. Majirani waliwareport Serikalini wamefunga mpaka Sound level meter! Ambayo inawaonyesha Sound level muda wote!. Hivyo kutopiga music kwa sauti isiyokibalika mtaani. Sheria zipo na iwapo wakazi wa mitaa jirani wakaenda lalamika ,Mwenye Bar husika atatakiwa 1. Kupiga mZiki kwa sauti ya chini au kufunga Sound proof system ndani ya Ukumbi usika. Hii imewai tokea Sinza Dar es salaam, Mabibo Kwenye Kanisa mojawapo la kilokole. Sheria ya kuzuia sauti kali ipo na inafanya kazi hapa Tanzania na duniani kote. Kenya toka wiki la jana wameanza funga pubs and night club zilizopo kwenye makazi ya watu.
SHERIA YA KUZUIA MAKELELE!!
NA Ngenzi M.S
Serikali imeanza kuifwatilia sheria ya kuzuia makelele yanayofanywa na bar, mahoteli, kumbi za starehe zilizo kwenye makazi ya watu pmj na makanisa yanayohubiri usiku kucha kwa kuweka spika ya sauti kubwa, mambo ambayo yamekuwa yakitukera watu wengi lkn tulikuwa hatuna la kufanya, sasa Serikali yetu imesema STOP!

Na saa nne usiku ni mwisho wa makelele kwani watu wana kazi za kufanya, watoto wanataka kusoma, wanafunzi wanajitayarisha kwa mitihani, wafanyakazi wamechoka na wanataka kupumzika!

======
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo.

Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10.

Pia, baa na kumbi za starehe za usiku zitakazopiga kelele, zitapaswa kulipa kiasi hicho.

Aidha, NEMC imesema pia kuwa wale watakaohusika na kelele za migodini za kutumia baruti, kupasua miamba zilizo zaidi ya matakwa ya sheria ya mazingira ya kelele na mitetemo, watapaswa kulipa Sh milioni tano ili kupata kibali.

NEMC imetaka watu kuheshimu kanuni za viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali nchini. Imeonya kuwa watakaokiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kanuni hizo zimeanza kutumika mwaka jana (2015).

Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Bonaventure Baya alisema hayo Dar es Salaam jana. Alisisitiza kuwa uchafuzi wa mazingira, unaosababishwa na kelele na mitetemo, umekuwa ukifanyika bila kujali sheria za nchi na sasa watashughulikia suala hilo ipasavyo.

Alisema hivi sasa kanuni za kudhibiti suala hilo, zimekamilika na zimeanza kutumika kikamilifu. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha kanuni na sheria, atachukuliwa hatua kali. Baya alitoa ufafanuzi kuwa yapo maeneo yenye kelele zaidi ya viwango vinavyoruhusiwa kisheria, ikiwamo maeneo ya migodini.

Alieleza kwamba kanuni zimeweka vigezo na tozo maalumu la kuanzia Sh milioni tano hadi Sh milioni 10, kulingana na eneo na aina ya kelele na mtetemo. Alisema mambo mengine ambayo kanuni zimeweka ni faini kwa kila kanuni itakayovunjwa na kusisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa ipasavyo.

Kulingana na hatua hiyo ya NEMC, sasa mtu mwenye kutaka kufanya sherehe mtaani, itakayohuisha kelele zitakazosumbua jamii pamoja na majirani zake, ikiwamo muziki maarufu wa ‘kigodoro’, ibada za makanisani zinazozidi matakwa ya kisheria ya uanzishwaji wa makanisa hayo katika jamii, atapaswa kulipa Sh milioni 10 ndipo aruhusiwe kuendelea na shughuli yake.

Kwa mujibu wa NEMC, ruhusa hiyo inayo lipiwa, pia ina muda na viwango vyake, ambapo kila muda husika unapoisha, kelele zinapaswa kupunguzwa ama kuzimwa. Hii inahusisha pia baa na kumbi za starehe za usiku.

Baya aliitaka jamii kuepuka uchafuzi huo wa mazingira wa kelele na mitetemo, ambao watu wengi wamekuwa wakidhani si tatizo. Alitaka watu kuheshimu matakwa ya sheria na kanuni kwa nyakati za mchana na usiku.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watu wengi, wakilalamikia usumbufu wa kelele na mitetemo kutoka kwa watu wanaoendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika jamii,” alifafanua Baya.

Alitoa angalizo kwa wanaotumia vyombo vya muziki na sauti katika maeneo ya makazi, ambavyo vimeleta madhara kwa afya za watu. Alisema matumizi ya vipaza sauti na vyombo vya sauti kubwa, wanapaswa kuwa na kibali maalumu.

Alieleza kuwa kanuni za kelele na mitetemo, zimeweka vigezo na viwango vya sauti kwa ajili ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya hospitali, makazi, migodini, kumbi za kijamii, kumbi za usiku za starehe, matangazo, baa na maeneo mengine.

Baya alisema baraza limepata changamoto kadhaa, ikiwamo uelewa mdogo wa jamii kuhusu kiwango cha sauti kinachotakiwa na kisichoruhusiwa na baadhi ya watu kwa makusudi huvunja sheria.

Kuhusu faini, alisema sheria ya mazingira imeweka wazi faini kwa wanaokiuka na kuchafua mazingira kwa kelele na mitetemo. Faini hiyo haiingiliani na tozo la Sh milioni tano hadi Sh milioni 10 lililoelezwa, ambapo mtu anapaswa kulipa si chini ya Sh milioni 50 na si zaidi ya Sh milioni 50 ama kifungo jela.

Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sheria za Mazingira wa NEMC, Ruth Lugwisha alisema tatizo la kelele na mitetemo, limekuwapo kwa muda mrefu. Alisema tangu kupitishwa kwa kanuni, tayari watu kadhaa wamewajibishwa.

Alisema miongoni mwa waliowajibishwa ni makanisa, kumbi za starehe na baa. Hata hivyo, hakuwa tayari kuwataja wahusika wala maeneo. Alisema uwajibishwaji huo ulihusisha faini, kufungiwa na onyo.

Tukio la Masasi Oktoba mwaka huu wakazi wanne wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, walifikishwa mahakamani kwa kosa la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya ‘vigodoro’ kwenye sherehe ya ndoa.

Wakazi hao ni Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa). Watuhumiwa hao baada ya kupatikana na hatia, walilipa faini na kuachiwa huru.

Maoni ya wananchi wa Tanga Huko Tanga, baadhi ya wananchi walisema hivi karibuni kuwa matamasha na promosheni mitaani, sasa zimekuwa kero. Waliomba idara ya utamaduni kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazohusika na utoaji wa vibali kwa ajili ya mikutano, maonesho na matamasha jijini Tanga, kupunguza kero ndani ya jamii.

Walitaka mamlaka hizo, kuacha kutoa vibali vya matamasha ya burudani na starehe zisizo na staha katika jamii, kwa sababu zinasababisha kelele mitaani na kuwanyima wanafunzi muda wa kujisomea.

Wananchi hao walidai matamasha yanayoambatana na kelele za ngoma na muziki, yanakwamisha ustawi wa elimu na kukua kwa kiwango cha taaluma, hasa kwa wanafunzi wa sekondari.

Damas Mboya, mkazi wa Ngamiani, alisema matamasha na promosheni zinazofanyika mitaani nyakati za mchana na usiku, hudumaza maadili na ni kero kwa jamii kwakuwa zinatumia vipaza sauti kucha usiku kucha.

Merina Kimweri, mkazi wa Chumbageni, alisema “Naishauri serikali na mamlaka husika, zipunguze idadi ya vibali vya kuruhusu shughuli hizi, hasa zinazofanywa mitaani bila viingilio.

Nasema hivyo kwa kuwa mara kadhaa zinaambatana na burudani za ngoma za kukesha, maarufu kama vigodoro na baikoko ya usiku, ambapo washiriki wakuu ni wanafunzi” .
 
Attachments

  • D2039610-F52C-49DA-B46C-48B2AF2A0013.png
    D2039610-F52C-49DA-B46C-48B2AF2A0013.png
    213.9 KB · Views: 5
  • 715C8091-8ABF-4155-8D33-AA65747C8684.png
    715C8091-8ABF-4155-8D33-AA65747C8684.png
    75.3 KB · Views: 5
  • 79A592AE-4FFD-4AA9-853E-58501FF4A78F.png
    79A592AE-4FFD-4AA9-853E-58501FF4A78F.png
    99.4 KB · Views: 5

Sheria zipo ni kweli. NEMC hawasimamii.
 
Acha wivu ww..
Kama vip tuanze na swalaa swalaa za saa 11 asubuh
 
kuna pia vijikanisa vya kilokole vinapiga sound utadhani wanashughuli ya singeli ukiwaambia utasikia ooh wewe una dhambi, kuna mmoja jamaa yangu alivamia pale riverside akakatakata maspika na vipaza sauti, hadi leo wamehama kabisa maana ilikua keroooooo ukiwauliza wanaleta ubishi kisa washahonga vijisadaka hukomserikali za mtaa. SHAME
 
Mathayo 6:5​

“Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao
Kwa kifupi Mungu apendezwi na Wanaosali kwa makelele na Show off nyingi
 
Kuna mwaka nikiwah sikia Nemc walitoa tamko la swala la xkumbi za starehe na mabar zifunge sound proof (vipu guza sauti na mitetemo) ktk izi kumbi ili kupunguza kelele ...
Sijui walifikia wapi ?

Aah nipo hapa Moro town kuna lounge inaitwa Star park ina piga mziki mkubwa mnooo yaan ni kelele tupu kwa wakazi wa karibu ....sijui hii star park inakuwaje kuwaje
Katika Taasisi zilishoshindwa kazi na kutumia resources za serikali isivyo ni hao wadudu, siku moja nilikuwa Ubungo Maziwa Dar, kuna bar inaitwa Half London kama siyo London kamili, wamefunga maspika makubwa sana yana vibrations balaa, cha kushangaza ni pale nilipowakuta baadhi ya wafanyakazi wa NEMC nawafahamu wanakunywa pombe hapo na muziki unaendelea kwa sauti ya kutesa.
 
“Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao
Kitendawili
 
Na saa nne usiku ni mwisho wa makelele kwani watu wana kazi za kufanya, watoto wanataka kusoma, wanafunzi wanajitayarisha kwa mitihani, wafanyakazi wamechoka na wanataka kupumzika!
  1. Kelele za muziki ziishie kwenye jengo la starehe walipo wateja wa biashara husika na siyo nje ya mipaka hiyo
  2. Saa nne usiku siyo fair, wanafunzi wanatofautiana, wengine wanasoma mchana na usiku wanalala, kamazi ya watu yana mambo mengi, wengine wanauguza wagonjwa majumbani muda wote
  3. Sheria hii isimamiwe ipasavyo kwakuwa matajiri wenye biashara zao wanatumia rushwa kuwapooza maafisa wa serikali wanaohusika na ufuatiliaji wa hizo adha na hasa maafisa afya ndiyo tatizo kubwa.
 
NEMC imetaka watu kuheshimu kanuni za viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali nchini. Imeonya kuwa watakaokiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kanuni hizo zimeanza kutumika mwaka jana (2015).
Kama wako serious wangeweka central call point watu wapeleke malalamiko huko na wao watoe maagizo kwa maafisa wao walioko mikoani, wilayani na kwenye miji midogo
 
Kila wilaya yupo afisa mazingira na yupo tayari kisaidia. You just need to report
 
Wajua wanachokifanya, ukireport wanataka mwende mpaka zilipo kelele, na muda mwingine wanawapa wahusika taarifa in advance mkifika mnakuta muziki umezimwa na ushahidi unakuwa hamna japo unakuta kuna spika kubwa kama kitako cha pipa
 
Watakachofanya ni kusikiliza wakazi wa mitaa husika! So dont give up wewe waone wahusika watasaidia
 
Back
Top Bottom