Love at first sight

Love at first sight

Hey guys

Imeshawahi kutokea ile hali umemuona mtu mara moja tu ukatamani awe wako?

Imenikuta stendi ya mabus mkoa fulani kuja Dar. Siku nafika pale nikamuona mkaka mmoja amazing,sijui kwanini alikuwa ananiangalia vizuri namna ile...kimoyo moyo nikaweka sala fupi "ee Mungu huyu kaka hata nisipokaa nae seat moja naomba nisafiri nae bus moja tu" halafu nikamalizia na Amen,nikaingia kwenye bus

Nimefika kwenye bus nikakaa nikiendelea kusali sala ile ile ya Mungu asaidie yule kaka kuwepo ndani ya bus nililopo,nikajisemea ngoja nitoke ndani ya bus nijifanye naenda washroom ili nimuone hata mara nyingine,nikatoka nikaenda washroom

Mungu ni mkuu jamani, nilivyotoka washroom nikaingia ndani ya bus nikamuona yule kaka ndani ya lile bus, mimi namba 9 yeye 10

Sikuwahi kuona safari fupi kama ile japo kiuhalisia ni safari ndefu mnoooo, masaa yalikimbia fasta kinyama huku tukiwa tumezoeana kama vile tulikuwa tunafahamiana kabla.

Hiyo ni mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo,tumekamilisha mwaka with my man 😊😊 Japo haiwahusu wala haiwasaidii kitu lakini nawaambia tu...nampenda huyu mwanaume

Naona kila kitu changu kinampenda,macho yakimuona napata ile amani ambayo siipati kwa yoyote,mwili wangu umemkubali mana nina hisia kali sana juu yake,nikiisikia sauti yake napata ile hamasa ya kuendelea kumsikiliza akiongea hata kama haongei na mimi

Sijawahi kuwa mdau ya ngono lakini tangu nikutane naye nataka kila muda tuwe peke yetu chumbani

Cheers to many years with my man 🥂

Am so in love!
Kumbe! Kuku mjanja hunaswa.....
 
Hivi TBH njinjo huwa unanichukuliaje?

Juzi kati nimechapia nimeandika MARUMBANO badala ya MALUMBANO ukaja kunishangaa eti hata mimi
Haya leo eti kuku mjanja,maana yake mimi sio mtu wa mapenzi ama niaje?

Mimi sio binadamu sio?
Easy easy easy Mkuuu 😉
Asikuharibie mood yako
 
Hivi TBH njinjo huwa unanichukuliaje?

Juzi kati nimechapia nimeandika MARUMBANO badala ya MALUMBANO ukaja kunishangaa eti hata mimi
Haya leo eti kuku mjanja,maana yake mimi sio mtu wa mapenzi ama niaje?

Mimi sio binadamu sio?
Kauli zako, misimamo yako, wajihi wako na hulka yako (kimaandishi) inakakisi mtu fulani. Kuna watu humu ndani ni wa kuigwa, inapokuwa ndivyo sivyo, majukumu ya vikongwe siye ni kuwakumbusha tu!
 
Back
Top Bottom