Love at first sight

Love at first sight

Hey guys

Imeshawahi kutokea ile hali umemuona mtu mara moja tu ukatamani awe wako?

Imenikuta stendi ya mabus mkoa fulani kuja Dar
Siku nafika pale nikamuona mkaka mmoja amazing,sijui kwanini alikuwa ananiangalia vizuri namna ile...kimoyo moyo nikaweka sala fupi "ee Mungu huyu kaka hata nisipokaa nae seat moja naomba nisafiri nae bus moja tu" halafu nikamalizia na Amen,nikaingia kwenye bus

Nimefika kwenye bus nikakaa nikiendelea kusali sala ile ile ya Mungu asaidie yule kaka kuwepo ndani ya bus nililopo,nikajisemea ngoja nitoke ndani ya bus nijifanye naenda washroom ili nimuone hata mara nyingine,nikatoka nikaenda washroom

Mungu ni mkuu jamani,nilivyotoka washroom nikaingia ndani ya bus nikamuona yule kaka ndani ya lile bus,mimi namba 9 yeye 10

Sikuwahi kuona safari fupi kama ile japo kiuhalisia ni safari ndefu mnoooo,masaa yalikimbia fasta kinyama huku tukiwa tumezoeana kama vile tulikuwa tunafahamiana kabla...

Hiyo ni mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo,tumekamilisha mwaka with my man [emoji4][emoji4]
Japo haiwahusu wala haiwasaidii kitu lakini nawaambia tu...nampenda huyu mwanaume

Naona kila kitu changu kinampenda,macho yakimuona napata ile amani ambayo siipati kwa yoyote,mwili wangu umemkubali mana nina hisia kali sana juu yake,nikiisikia sauti yake napata ile hamasa ya kuendelea kumsikiliza akiongea hata kama haongei na mimi

Sijawahi kuwa mdau ya ngono lakini tangu nikutane nae nataka kila muda tuwe peke yetu chumbani

Cheers to many years with my man [emoji1635]

Am sooooooooooo in love!!
Sawa, kumbe hii ndio ID yako.

Ahsante sana kwa kunianzishia uzi na kunisifia
 
Kweli kabisa unamhusisha Mungu katika tamaa za mwili wako? Huyo labda shetani. Tufikirie sana tunapomwongelea Muumba. Ni sawa na jambazi anayeomba aue, aibe na asikamatwe halafu anasema nilmwomba Mungu!!
Acha povu basi ...Mungu mwenyewe kasema tupendane .
Hongera Joanah
Love is a beautiful thing [emoji7], may you two grow old together .
 
Back
Top Bottom