MJ1
mambo mengine huwaga tunayagumisha (nimeliunda mwenyewe hili neno na sijui kama lipo kwenye kamusi ya mtu) tu sisi wenyewe. Kuyafasili mapenzi kwa lugha yetu ya Kiswahili wala siyo vigumu kama unavyodhania. Mapenzi ni dhana. Ni dhana inayofurahisha nafsi. Ni dhana inayomfanya mtu ajisikie naye ni mtu katika watu. Ni dhana yenye utamu na machungu. Ni dhana inayoweza kuleta raha na shida.
Ni dhana inayoweza kumpatia mtu wasiwasi ama amani. Ni dhana inayoweza kumfanya mtu ajione yuko kwenye dunia tofauti kabisa na wengine. Ni dhana inayoweza kumfanya mtu augue au awe mwenye afya.
Nasema mapenzi ni dhana kwa sababu mapenzi siyo kitu. Mapenzi hayashikiki, mapenzi hayaonekani huwezi ukanyoosha kidole na kunionyesha eti yale ndiyo mapenzi, mapenzi hayana rangi na wala hayana harufu.
Mapenzi ni dhana iliyopo kichwani. Kutoka kichwani inaelekea moyoni. Ikitoka moyoni inaelekea usoni. Ikitoka usoni inaelekea tumboni. Na ikitoka tumboni inasambaa mwili mzima.