NAMBA NANE:
Mimba haijifichi jamani, nilijificha wewe, waaapi, kazini walinigundua mapema tuuu, kumbe na bwana hacker taarifa akawa amezipata pia, ila aliamua kukaa kimya, hakuacha kunicheck na kuuliza kama nipo okey, nadhani alipiga hesabu zake akajiongeza tu kua mzigo sio wake. Kupitia mama nikafahamu kua Karim ameenda kujitambulisha rasmi nyumbani na kutoa posa. So I was officially his fiance, kimbembe kinakuja kwa yule mchumba wa mwanzo wa Karimu, hakutaka kuelewa somo, hakutaka kuolewa mitala kwaio ikawa imemuweka Karim njia panda, na kumbuka walikua hawajafunga ndoa bado ,huyo dada alikua bado mwanafunzi wa chuo. Karimu ilionekana anampenda sana huyo dada maana tukiwa tunaongea alikua ananambia Bella am not okey, sipo okey na Halima and that stuffs.
Ilikua inaniumiza kuona ni kama nimevuruga amani ya yule mwanaume, anataka kunipigania lakini hataki kumuuumiza Halima, alichojibu Halima ni kua amemsamehe mchumba ake kwa kunipa ujauzito na atalea huyo mtoto lakini hahitaji mitala kwa mda huo, she can take care of her man. Kwa wakati huo ndio akili ilikuja sasa, ule wakati wakutumia hisia ukawa umeisha, majuto kwa mbali yanakuja yanakata... lakini nikikumbuka kua nilitaka mwenyewe najikuta najipa imani kua kila kitu kitakua sawa...kwaio Halima akawa amejua kua nilimuibia mwanaume wake and I went extra mile kujipea mimba.
Halima alipambana akaolewa the same year, ndoa za kiislam si kama zetu wakristo eti mafundisho miezi kadhaa, matangazo matatu ya ndoa kanisani, sijui vipingamizi, wenzetu
saa nane mahari, saa kumi ndoa, tena hata kwa msaafu unaolewa, kwaio kabla sijajifungua Halima akawa mke rasmi wa bwana Karim. Yale mamlaka ya kumwambia Karim naomba uje SA yakawa hayapo tena.
Halima alidhamiria kunikomesha maana miezi michache mbele akabeba ujauzito , akaahirisha mwaka chuo akaamua kulea ndoa yake na ujauzito wake, hapo nimebakiza siku chache nijifungue, my mom ikabidi aje SA maana nilishindwa kusafiri sababu ya ujauzito kua mkubwa na kuhofia complications during the flight hours.
Nilijifungua salama mtoto wa kike mrembo mnooo, alifanana kila kitu ma mimi ila alifata macho na midomo ya babake, Karim ako na sweet lips in away unatamani uzitafune tuuu, ndio akazipata binti angu mpenzi. Alichoshangaa mama ila aliamua kukaa kimya ni kutomuona Karim hospitali wala nyumbani, guess who was there...Mr. hacker. Kutokana na hali ya ugonjwa mama alishindwa kuniuliza chochote, aliniacha nipone kwanza, Leon was there day and night since the first day nimekua nimepata uchungu, taking care of me and the baby, alileta nahitaji yooote, na alikua huru kufanya hivyo maana si amenihack kwa hiyo anajua ubuyu woote kuanzia kutolewa posa hadi ndoa ya Halima.