Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!



Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang'ang'ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
+255717 709618
novakambota@gmail.com
www.novakambota.com
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011

 
Big up Nova. You took back to old school primariiii kwa mwalimu mkuu wakati wa saba saba nk
 
 

Acha hadithi za kutunga ww, kama barua ya kujiuzulu ilikubaliwa usiku wa manane, mbona hautuelezi nini kilimfanya EL kutangaza bungeni asubuhi yake kujiuzulu, na barua hiyo ya kukubaliwa EL kujiuzulu alipewa nani wakati hata spika wa kipindi hicho amewahi kukuaririwa akisema kujiuzulu kwa EL ndilo jambo lililomshtua mno kipindi cha uongozi wake- Hizi hadithi zenu za kutunga pelekeni huko vijiweni kwenu!!!
 
Mi siwaelewi kwahiyo mnataka kusema rais wa 2015 ni Lowassa na si DK Slaa tena??? Au tunaongelea wagombea tu

Tunaongelea rais! tumekuacha wapi mkuu?! ingawaje ni ngumu kumeza, inabidi ukubali hivyohivyo!!!! ukishindwa, fanya kama nilivyofanya mwenzio, hapa nilipo nina azam cola pembeni, kwa issue ngumu kumezeka kama hizo nashushia na hiyo ki2!!!
 
maumivu ya kichwa huanza pole poleeeee,mi napita zangu naelekea mmu,karibuni waungwana.
 
Nadhani tatizo la nchi yetu lipo kwenye kichwa. Na siyo kwenye vidole at sehemu nyingine
 
Watu kwa kucheza na maneno ni mahodari sana, hivi Lowassa kasema nini kuhusu Richmond zaidi ya kusema alimpigia simu Kikwete alipokuwa nje ya nchi akamwambia asubiri ushauri wa makatibu wakuu.

Hapo ndiyo Lowassa kasema Richmond ya Kikwete au ina husiana na Kikwete? Mnanshangaza!
 

Mkuu hujaelewa falsafa yangu

falsafa yangu CCM wote ni wezi.....nani wa kumvua gamba mwenzake?

Lowasa anapoweka wazi wizi wao yeye na rais wake ni chereko na furaha kwa wananchi...lakini ukitake side between Lowasa na Kikwete inaleta logic?? wote wezi "kuvua gamba" ni falsafa na maneno yaliyowekwa kukupumbaza wewe! RA si alijiuzulu, aliyemweka mbunge wa CCM Igunga ni nani? hawa wote wezi huwa tunawashangaa mnaposema EL fisadi na JK msafi,...au huyu ajivue gamba na yule aisjivue...Nape juzi amesemaje?? na wewe leo unasemaje??

EL anasema wezi wote wamefunguliwa mashtaka..yy kwa nini hajafunguliwa mashtaka?? hauoni tusi kwako wewe, CCM na serikali yako?? guys think ebo!
 
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ni CHENGE au alishaondolewa??

Bado yupo, na kwa sasa anaandaa dodoso a.k.a questionaire kwa ajili ya watuhumiwa wa pande zote mbili-upande wa akina Nape na upande wa akina EL! Moja ya maswali yaliyopo kwenye dodoso hilo kwa upande wa akina EL ni:
Qn:1. Mheshimwa Waziri Mkuu Mstaafu, eti kweli inawezekana mtu kama wewe mweneye utumishi uliotukuka inawezekana kweli ukawa fisadi?! I can't believe it at all; is it true?
Instruction to answer this question is YES or NO!

Qn:2. Mr. Honarable Excellence Unquestinable Lawyer Ndugu Andrew Chenge; is it possible kweli kwa m2 kama mimi nisiwe na tujisent kama tule nje ya nchi wakati nina tung'ombe zaidi ya laki moja?

Instructions to answer: Strictly, my answer should be POSSIBLE or IMPOSSIBLE., over!

Na dodoso kwa Nape na wenzake!
Wewe nape a.k.a Vuvuzela mwenye roho ya korosho, roho mbaya mwenye kijicho na roho ya kwanini, kv tu babako alikufa maskini; Briefly, explain with vivid and strictly strong and unquestionable evidence approved by undoubtful lawyers, as to why u should not be fired from the part u fail u to submit the demanded evidence?!
 
Mi nakuunga mkono ccm wasipo msimamisha lowasa inakula kwao
 
Sio kila mtu ana bei. Kama nyie mnauzika shauri lenu, msitusemee sisi.

Unafikiri issue ni kuuzika basi, issue ni kununulika! Unaweza usiuzike lakini ukanunulika! Tusiyemtaka waungwana sio asiyeuzika, bali asiyenunulika na kumweka kwenye kapu lako! Ukishakuwa waziri, say wa nishati na madini.; tayari unauzika kwa gharama yoyote ile.....sasa tunachotaka ni yule asiyenunulika kwa gharama yoyote ile!!!
 

dah mkuu kwan EL asubuhi ili alitangaza kujiuzulu?kwa kumbukumbu zangu MH EL alitangaza kuwa amesikitiswa sana ameonewa sana na amegundua kuwa wish ya kugrant ni UPM kwa hiyo MEMWANDIKIA BARUA YA KUJIZULU MH RAIS,naye ndo alikuwa anasubiriwa aridhie ua vinginevyo.vyanyuma ya pazia ndo hivyo vinavyosemwa mkuu
 
kwani Lowasa akitoswa kitatokea nini CCM zaidi ya majeraha kwa mwenyekiti
 
Inategemea, nyati kajeruhiwa na nani/na nini?, nionavyo mimi nyati kakeruhiwa na muwindaji hodari mwenye siraha nzito- bora nyati akimbie akafie mbali kuliko kujaribu kulipiza. Itakula kwake.
kwa hali ilivyo tete sasa na kwa mujibu wa mleta mada ni kuwa jk kajeruhiwa kweli. Na huyu jamaa akijeruhiwa huwa mbaya kuliko nyati. Lolote laweza tokea
 
Mungu saidia Tz
Tanzania Ipi Mkuu haya mambo ni yakichama zaidi wacha MUNGU awamalize wezi hawa!
Acha kutumia jina la Mungu kuyatetea magamba wacha wapotezane nchi iokolewe hiii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…