Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
lol........kumbe siku hizi ni choo cha stendi?sio cha kike???lol..........
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya kuigiza kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. [/QUOTE]
Unajua nini? Wote ni wajanja, lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mjanja aliekulia Monduli na mjanja aliyekulia Magomeni!!!
Dah!Nimecheka sana kuhusu hao wajanja na sehemu walikokulia
Kwa wale wanaoshangilia "ushindi" wa lowassa baada ya suala lake la kuvuliwa gamba pamoja na suala la Nape na chiligati anaowalalamikia kuzunguka nchi nzima "kumchafua" kutinga mikononi mwa kamati kuu,leo nataka kuwakumbusha kidogo kuhusu Jakaya ili huku mkifurahia "ushindi" pia mumfahamu sawa sawa muungwana jakaya ni mtu wa dizaini gani,sina lengo la kutia mchanga kwenye kitumbua chenu cha furaha la hasha ila nataka tukumbushane muijua siasa pia.Wandugu wapendwa mnajua ilikuwaje mpaka Lowassa akawa sio waziri mkuu.....
Kiufupi ni Kwamba Lowassa aliingizwa choo cha stendi na Jakaya!
Lowassa aliutema uwaziri mkuu anaoupenda mpaka leo kutokana na "utoto wa mjini" utapeli wa kisiasa wa Rais Kikwete kwa swahiba wake Lowassa, wala haikua "ajali ya kisiasa".
Mpango mzima ulikua hivi:
Bunge kupitia Kamati Teule ilisoma ripoti yake kupitia mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Hali ilikuwa tete Dodoma na hata Chamwino ambako Rais Kikwete alikuwa amejichimbia.
Baada ya kusomwa kwa ripoti, taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao.
Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani; – Lowassa akapendekeza eti jk aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, Jk baada ya "kupima" akastuka.
Ndipo yeye akaja na maarifa ya kimjini kwa kumwambia Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, halafu yeye jk aicheleweshe kuijibu hiyo barua kwa makusudi mpaka Bunge lihairishwe ili kumpa nafasi yeye jk kama rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Buge wa Aprili haujafanyika Dodoma.
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya "kuigiza" kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao. Usiku wa manane wa siku hiyo, Rais Kikwete aliamua kuwa barua ile ijibiwe na kukubaliwa. Ni kinyume na makubaliano yake ya awali na Lowassa!
Sasa leo tena suala la lowassa baada ya kupata kibali cha NEC liko mikononi mwa kamati kuu ambamo lowassa hayumo!Na watu wake eti wanashangilia "ushindi" wa ice cream iliyowekwa juani huku jakaya akiwa tayari amejeruhiwa na kutajwa kwenye sakata la richmond na pia ikikumbukwa Jakaya hana tena cha kupoteza kwa kuwa hawezi tena kuwa rais!mi nawaomba msiwe wajinga kama jamaa yenu kwa mujibu wa mwalimi nyerere ambae alifahamu ujinga wake zamani kabla kabla ya jk kuja kuthibitisha kwa kumuingiza choo cha stendi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mi siwaelewi kwahiyo mnataka kusema rais wa 2015 ni Lowassa na si DK Slaa tena??? Au tunaongelea wagombea tu
Waberoya wewe huyo? nendeni taratibu...
Heee kumbe waberoya nae kaingia kichwa kichwa kuamini lowassa kweli amepona kuvuliwa gamba?!!basi watu yaelekea huwa hamfuatilii mambo!wabaya wote wa lowassa walikuwa wanaomba usiku kucha suala la kujivua gamba baada ya kushindikana kwa hiyari liachiwe kamati kuu lakini baada ya kupata kibali cha nec!sasa hapo nani mshindi mnavyodhani??wabaya wa lowassa ama lowassa??maana kibali kimeshatoka na watu mnajifanya mmesahau hiyo badala yake mmekazania kulia lia kwa lowassa ili jumba bovu lisimuangukie peke yake!haitasaidia alitakiwa azicheze karata zake vizuri suala hilo lizimwe kwa nec kugoma kutoa kibali,kachemsha kampa rungu mwenyekiti atambe na kamati kuu yake anayoimudu vyema!
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ni CHENGE au alishaondolewa??
only Allah can stop Honorable Lowassa...
no one else.
Mark n bind it
Mi nakuunga mkono ccm wasipo msimamisha lowasa inakula kwaoLowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%
Sio kila mtu ana bei. Kama nyie mnauzika shauri lenu, msitusemee sisi.
Acha hadithi za kutunga ww, kama barua ya kujiuzulu ilikubaliwa usiku wa manane, mbona hautuelezi nini kilimfanya EL kutangaza bungeni asubuhi yake kujiuzulu, na barua hiyo ya kukubaliwa EL kujiuzulu alipewa nani wakati hata spika wa kipindi hicho amewahi kukuaririwa akisema kujiuzulu kwa EL ndilo jambo lililomshtua mno kipindi cha uongozi wake- Hizi hadithi zenu za kutunga pelekeni huko vijiweni kwenu!!!
kwa hali ilivyo tete sasa na kwa mujibu wa mleta mada ni kuwa jk kajeruhiwa kweli. Na huyu jamaa akijeruhiwa huwa mbaya kuliko nyati. Lolote laweza tokea
Tanzania Ipi Mkuu haya mambo ni yakichama zaidi wacha MUNGU awamalize wezi hawa!Mungu saidia Tz