Mkuu THE ROMANTIC,
Stori yako haina ukweli wowote kwa kuangalia mtiririko wa matukio yenyewe mpaka Lowassa alipotangaza Bungeni kwamba amemwandikia barua Rais ya kuomba kuachia ngazi halafu pia kuna matatizo ya kikatiba, na hayo yote lazima yalikuwa yanajulikana kwa wote.
Mosi, Kwa kuwa Ripoti ilishasomwa Bungeni tayari, hakukuwa na uwezekano wa kutojadiliwa mpaka Bunge liahirishwe. Kwa hiyo hoja yako kwamba EL angeandika barua ya kuomba kujiuzulu then JK achelewe kuijibu, isingezuwia Bunge kuendelea na mjadala wa Ripoti. Kama JK alitaka kuizima hiyo ripoti basi lazima angewaita wabunge wa CCM hata kabla Bunge halijaanza ili kuweka mambo sawa na huo umekuwa ni utaratibu wao.
Pili, JK asingekuwa mjinga akubali kwamba Lowassa akatangaze Bungeni kwamba ameamua kujiuzulu halafu JK aje kumkatalia, ingewafanya wananchi wawe na mtazamo hasi kwa Rais wao.
Tatu, Waziri Mkuu akitangaza kujiuzulu, maana yake ni kwamba Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjwa mpaka Waziri Mkuu Mpya atakapoteuliwa na kupitishwa na Bunge then ndipo Waziri Mkuu ashirikiane na Rais katika kuteua Mawaziri/Naibu Waziri. Hilo pekee linafanya shughuli za serikali Bungeni zisimame kwa muda mpaka Baraza la Mawaziri litakapoteuliwa na kuapishwa.
Kwa hiyo the whole stori haina mashiko.