Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

kwanza kabisa namtaka mod aonyeshe mtunzi wa shairi la VIVA KAMANDA LOWASSA ambaye ni mimi KAMBOTA baada ya hapo sasa naomba nimjibu Mpayukaji( Bwana Nkwazi Mhango) kama ifuatavyo;

Lowassa Ni Msafi, Hahitaji Kusafishwa ( Jibu)
Mjengwa naomba tena, jukwaani nirejee
Niliyoandika jana, napenda niyatetee
Mkuranga kimanzichana, Lowassa aendelee
Nkwazi hujaelewa, umefakamia mada



Mhango kajichanganya, kujibu asichojua
Kauropoka unyanya, pasipo kulitambua
Si hasi wala si chanya, Nkwazi kasimamia
Mhango wajipotosha, kujibu usichojua



Lowassa ni mtu safi, tegua kitendawili
Angelikuwa ni ni fisi, mahakama mhimili
Hojazo ni mufilisi, wewe ndumilakuwili
Nkwazi rudi shuleni, kaisome CCM



Mhango wanishangaza, ukweli kutofahamu
Waonekana kilaza, rejea Dar es salaamu
Kwa hoja ntakuchakaza, wewe mwana wa Adamu
CCM huijui, fitina wamezoea



Lowassa ni kiongozi, hili unalitambua
Achana na upuuzi, ule walomzushia
Usijifanye dandizi, kudandia usojua
Nkwazi mwana Mhango, uliza nakusikia



Beti sita natuama, nimefikia tamati
Lowassa mtu wa maana, hodari wa mikakati
Nkwazi soma kwa sana, tambua hizi nyakati
Lowassa ni mtu safi, hahitaji kusafishwa.


Nova Kambota
Tanzania, East Africa
27 November 2011
Nova Tzdream -
 
Mjengwa naomba tena, jukwaani nirejee
Niliyoandika jana, napenda niyatetee
Mkuranga kimanzichana, Lowassa aendelee
Nkwazi hujaelewa, umefakamia mada

Mhango kajichanganya, kujibu asichojua
Kauropoka unyanya, pasipo kulitambua
Si hasi wala si chanya, Nkwazi kasimamia
Mhango wajipotosha, kujibu usichojua

Lowassa ni mtu safi, tegua kitendawili
Angelikuwa ni ni fisi, mahakama mhimili
Hojazo ni mufilisi, wewe ndumilakuwili
Nkwazi rudi shuleni, kaisome CCM

Mhango wanishangaza, ukweli kutofahamu
Waonekana kilaza, rejea Dar es salaamu
Kwa hoja ntakuchakaza, wewe mwana wa Adamu
CCM huijui, fitina wamezoea

Lowassa ni kiongozi, hili unalitambua
Achana na upuuzi, ule walomzushia
Usijifanye dandizi, kudandia usojua
Nkwazi mwana Mhango, uliza nakusikia

Beti sita natuama, nimefikia tamati
Lowassa mtu wa maana, hodari wa mikakati
Nkwazi soma kwa sana, tambua hizi nyakati
Lowassa ni mtu safi, hahitaji kusafishwa.


Nova Kambota
Tanzania, East Africa
27 November 2011
 
Kumbe ile safari ya Lowasa huko Nigeria haikuwa bure! Kwa hiyo ndio kusema sasa Lowasa ametakasika?
 
Kambota achaujuha, CCM siyo fani,
Kijana acha mzaha,kunambia sina fani,
Sema yenyemkutadha, siyo kuleta uhuni,
Kama kakaumehongwa, tulia kula kizani

Najua uko kazini,wataka akusikie
Lowassa ni yakodini, lazima umsifie,
Ila jua u kizani,ni heri ujililie,
Kambotaunachekesha, noisome CCM!

Sikujua tokamwanzo, ninakinzana na zoba,
Mwenye mgandomawazo, aso kifani mjuba,
Sikujua hamnazo,nilomvisha kikuba
Kambota achaujuha, soma maoni ya watu.

Wasema nirudi Dar,nipambane na mgao!
Nani amekuhadaa,huyo kakupiga bao
Lowassa kaka balaa,ndiye chanzo cha mgao,
Kambota hebukomaa, mambo ya kitoto acha.

Mie kwako nimwalimu, hilo kaka walijua,
Kaiulize kaumu,najua wanitambua,
Nii mwalimu wawalimu, Bongo nzima watambua,
Kambota shikaadabu, kiatu changu huvai.

Hata utetee vipi,Lowassa bado fisadi,
Wenye mawazomafupi, humuona maridadi,
Awatumia ja chupi,waona wanafaidi,
Kambota achautani, haramu haishibishi.

Wino umeniishia,mbele sitaendelea,
Karima akijalia,hoja itaendelea,
Muhimu toto sikia,adabu upate tia,
Lowassa atakuponza,ukweli ukidhihiri.
 
mnapoteza muda na hizo ngonjera na mashairi;mwalimu nyerere alishaacha wosia,huyo jamaa hatakasiki,na nchi itatawaliwa na waislam na wakatoliki tu kwenye nafasi ya juu;wengine mwisho uwaziri mkuu,kama mnabisha muulizeni mzee msuya, malecela na sumaye wanaijua vizuri hii kitu!na waislam waushukuru muungano na vurugu zao za kudai haki kwa fujo otherwise licha ya kuleta uhuru wangeweka pending vilevile......nyie mnadhani mzee malecela alitaka kubadili dini hivi hivi tu?kuna mambo yanaendelea chini ya kapeti,kwa nyie wapiga debe wa wanaoutaka urais hao jamaa zenu wakitaka urais aidha wawe wakatoliki ama waislam!huo ndio ukweli japo ni mchungu kidogo!
 
MHANGO ACHA UJUHA

Mhango acha ujuha, heshima wajishushia
Wasababisha karaha,kuimba kuitikia
Wajiletea jeraha,moyoni hutalilia?
Kwa hili umechemsha, zumbukuku nakuita.


Lowassa wamtamka, uzushi wamtungia
Hoja zako za kubaka, maneno unadandia
Hakika u kibaraka, leo nakupasulia
Ikulu ya kutumia, Kikwete swahiba wako.


Huijui Richmond, kwanini unaropoka
Tena wajifanya fundi, huku unaweweseka
Punguza wako upimbi, punguza kubwekabweka
Nkwazi acha ujinga, heshima wajishushia.


Kanada umetopea, hupakumbuki nyumbani?
Halafu wajitetea, uhesabiwe kundini
Tatizo lako sikia, upeo wa kiganjani
Miaka umenizidi, Kwa hoja usithubutu.

Wamtukana Lowassa, nini amekukosea?
Umegeuzwa galasa, uzushi kufakamia
Kwani kamanda Lowassa, nani alimteua?
Nkwazi wewe mjinga, fumbo hutaling'amua.



Hapa mwisho nagotea, tamati nimefikia
Nkwazi nakushangaa, nini unajivunia?
Siri zako nafichua, Ikulu yakutumia
Nkwazi nipe jawabu, unalipwa bei gani?
 
Kabota nitakubota, hata kama kiroboto,
Yote unayolumbata, si chochote ni kokoto,
Huna mpata na kata, nijuacho u limpyoto,
Kabota acha unywanywa, naona unatumiwa.

Lowassa bado fisadi, hata mmpambe vipi,
Kambota wewe hasidi, watumika kama nepi,
wajiona wafaidi, kumbe kesho ni makapi,
Kabota acha unywanywa, Lowassa akutumia.

Wauliza nalipwaje, Nani huyo anilipe?
Sijalipwa hata punje, mie mwezio si kupe,
Shurti nijikunje, niishi si kwa mahepe,
Kabota acha ushamba, Lowassa atakuponza.

Naijua Richmond, Richmond ni Lowassa,
Kikwete ni Richmond, Richmond ni mkasa,
Kambota nawe ni bundi, Richmond takutesa,
Japo wachumia tumbo, Kambota acha ujuha.

Utajaliwa ja ng'oda, Siku yako ikifika
Ja ng'oda utakonda, Lowassa akikutoka
Ukuuishie ukuda, ubaki kulalamika
Fisadi hana rafiki, Jifunze kwake Lowassa

Mambo yalipombana, Kikwete kaumuumbua,
Hawa marafiki sana, Itakuwa wewe bua,
Leo sana wajiona, ujinga wakusumbua,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

Huna mpaka na nune, Kambota wala jaani,
Leo wewe ujivune, kumbe wenda majilini,
Sema sana utukane, itafika arobaini,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

Kaditamati natua, mbele sitaendelea,
Kwa hapa naomba dua, wadudi anisikia,
Ninamuomba mulua, Kambota aone jua,
Kambota chumia tumbo, hebu tumia ubongo.
 
Ninakuunga mkono, wewe mr kambota
Tena kwa maandamano, ya Dar hadi Msata
Ulosema ni manono, kama ya nyama ya bata
Laigwenan msafi, wao walimchafua.
 

Ndio maana nyerere alimwambia mzee kawawa asiwe mjinga kama lowassa.....juzi ndio nimekuja kumuelewa mzee yule!
 

Usiwasemee watu. Semea nafsi yako.
 


mbona ameishasema ya nani?? unajua EL hababaishwi na vi-comment kama hivi....LIA kuwa uliingizwa mjini , ukaaminishwa na sasa unaona kurudi ni kazi....ni aibu hii!

kujiuzulu nchi za duni ya tatu ni ngumu mno...maana tunachukulia kujiuzulu ni kukosa, kwa mawazo yako haya kwa nini akina Mwinyi wajiuzulu kwa kashfa ya mabomu ya gongo la mboto...you have a long way to go!
 
JK na Lowasa wana MoU yao tangu mwaka 1995. MoU wanaitekeleza kwa akili, umakini na umahiri mkubwa sana. Kashfa ya Richmond iliitikisa kidogo MoU hii. Wakakaa wakatafakari jinsi ya kui-handle kashfa hii bila ya kuathiri masuala ya msingi ndani ya MoU hii. Wakakubaliana kugawana kashfa hii kwa awamu. Kuanzia mwaka 2008 hadi 2011 Lowasa akakubali kujitwika zigo hili kimyakimya ili kumvusha JK kwenye uchaguzi mkuu wa 2010. JK akavuka ingawa kwa taabu na mbinu kadhaa chafu.

Kikwete hagombei tena 2015. Hana la kupoteza. La msingi kwenye ile MoU yao lilikuwa kupokezana MADARAKA ya URAIS ifikapo 2015. JK ameamua kuibeba kashfa ile. Juzi kwenye NEC akakubali rasmi kuibeba kashfa ile kwa kumruhusu Lowasa kuihamisha kistaarabu kutoka kwake kwenda kwa JK kupitia CC ya CCM. Lowasa sasa ni MSAFI kuliko hata theluji na yuko tayari sasa kuupokea Urais ifikapo 2015.
Juzi alikuwa maeneo ya akina Chiligati akianza safari ya kuelekea IKULU kupitia harambee za makanisa ambayo ndio majukwaa safi yanayosikika sana. Hakuna wa kumzuia labda Mwalimu afufuke!
 

hapo pekundu ndio ukweli wenyewe...ambao vyombo vyetu vya habari havitaki kusema RICHMOND=LOWASA=KIKWETE...kinyume na hapo uzezeta!
 

Simtetei EL lakini kukataliwa na Nyerere sio kigezo tosha, kwa kifupi ni kwamba watanzania tutafute ufisadi mwingine wa EL uliomfanya akawa tajiri lakini si Richmond, hiyo ni ya JK kama sivyo na yeye alipaswa kujibu mapigo kwenye mkutano wa NEC lakini kwa kunyamaza inadhihirisha anahusika, kwani utajiri wa R1 wa haraka namna hiyo unatoka wapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…