"Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu"
Nimeyapenda haya maneno ya mwenyeketi. Yamejaa busara na hekima tele.
Nape sioni kama kafanya kitu kibaya. Kama katibu mwenezi, alikuwa anafikisha ujumbe kwa wanachama wote juu ya yaliyoafikiwa kwenye kikao cha NEC cha April.Katika kikao cha Aprili NEC ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.
Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.
Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.
Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.
Kikwete na kundi lake ndani ya Magamba walitaka kumtumia ili akamilishe mradi wao, sasa wameona mradi wao walioutaka kuukamilsha umeshindikana basi hawana mahitaji naye tena!!! Kweli siasa ni mchezo mchafu sana!!!!
Nani amaekuambia CCM kuna mgawanyiko? Katika jamii yoyote, lazima mawazo ya watu yatofautiane. Hamuwezi wote kuwa na mawazo sawa.Tangu lini Kikwete akawa na hekima na busara!? kama ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na mpasuko mkubwa ndani ya magamba ambao umedumu kwa miaka michache iliyopita na wala nchi yetu isingekuwa inaenda mrama katika kila idara....Wakati mwingine tuweke unazi wa vyama pembeni na tuwe wakweli katika kutetea maslahi ya nchi yetu badala ya yale ya chama!!!!
Nani amaekuambia CCM kuna mgawanyiko? Katika jamii yoyote, lazima mawazo ya watu yatofautiane. Hamuwezi wote kuwa na mawazo sawa.
Wapinzani ndani ya CCM lazima wawepo but at the end ni lazima watekeleze maamuzi na matakwa ya chama.
Huo mgawanyiko unaouongelea sijui upo wapi in particular.
Alichokuwa anakieleza Nape ndo lilikuwa kusudio la chama. Tatizo limekuja kwamba maazimio ya chama kuhusu kujivua gamba yameshindikana kutekelezwa, au tuseme hayatekelezeki. Kwa hiyo hata kumhukumu Nape ni vigumu.
Kwa maneno mengine ni kwamba Mwenyekiti ndo anapaswa kubeba lawama kwa sababu falsafa ya ya kujivua gamba imeshindikana. Na sasa EL amemrushia mzigo wa Richmond pia.
Usitake ncheke(FF)!Kama hao ni references zako, basi umepotea kabisa! Hao wana mambo yao binafsi na wala hayausiani na chama kabisa. Ukiongelea mgawanyiko ndani ya CCM halafu ukawataja hao unaonekana kama kituko.Waulize fisadi Rostam, Mwakyembe aliyelambishwa vya kulambishwa, Sitta anayeitwa mnafiki na baadhi ndani ya magamba kwa kutetea maslahi ya nchi dhidi ya malipo ya kifisadi, Wabunge ndani ya magamba ambao hawaridhiki na utendaji wa Kikwete na hivi karibuni walikaribia kumuomba abwage manyanga. Pia usisahau kwamba ukipenda basi chongo utaita kengeza...
Kama huoni vitisho ya kutaka kumuua Sitta na Mwakyembe na wahusika kusema hadharani hivyo kwamba wamepokea vitisho vya kunyang'anywa uhai wao kwa njia za simu, basi hutaona lolote lile la kuonyesha mpasuko mkubwa ndani ya magamba. Kwenye upinzani wa kweli ndani ya chama chochote kile cha siasa kunakuwa hakuna vitisho vya kutoana roho, vitisho kama hivi vya kuchukua uhai wa baadhi ya wahusika ndani ya magamba au chama chochote kile huwa vinaashiria mpasuko mkubwa sana.
Dah!!! Ukistaatabu ya Malaria Sugu.......Usitake ncheke(FF)!Kama hao ni references zako, basi umepotea kabisa! Hao wana mambo yao binafsi na wala hayausiani na chama kabisa. Ukiongelea mgawanyiko ndani ya CCM halafu ukawataja hao unaonekana kama kituko.
Alichokuwa anakieleza Nape ndo lilikuwa kusudio la chama. Tatizo limekuja kwamba maazimio ya chama kuhusu kujivua gamba yameshindikana kutekelezwa, au tuseme hayatekelezeki. Kwa hiyo hata kumhukumu Nape ni vigumu.
Kwa maneno mengine ni kwamba Mwenyekiti ndo anapaswa kubeba lawama kwa sababu falsafa ya ya kujivua gamba imeshindikana. Na sasa EL amemrushia mzigo wa Richmond pia.
... Ni wachache wanaomzodoa Lowasa au wengi? Kumchangamkia ni hadaa au upendo kwake?
Tunasubiri tamko la Makamu wa Kwanza wa Rais wa visiwani anamsimamo gani juu ya mstakabali wa nji hii, maana ukimya wake ni kutokana na kudhoofishwa na matamu ya Ikulu ya Zenj?
Wee unawajua hao kina nani?...na wanafurahia kipi...CCM haishii wajumbe wa CC..Ni wachache wanaomzodoa Lowasa au wengi? Kumchangamkia ni hadaa au upendo kwake?
Tabia hii ndiyo ninayoikataa mimi kuwa mwanaCCM maana yake unatakiwa ufanya kama huna akili timamu vile, unapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Hata kama ungekuwa na upeo gani utadumazwa tu na kuishia kufanya usanii wa maigizo kama binti kawawa anavyofanya kama si mtoto wa mzee wa Simba wa Nyika.
Badala ya kufikiria mambo muhimu ya taifa letu wao ni sherehe na ulaji wa ushindani.