Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usitake ncheke(FF)!Kama hao ni references zako, basi umepotea kabisa! Hao wana mambo yao binafsi na wala hayausiani na chama kabisa. Ukiongelea mgawanyiko ndani ya CCM halafu ukawataja hao unaonekana kama kituko.
Duu ama kweli kamvisha gamba gumu mwanangu. Siamini haya maneno Lowasa ameyatapika. Kumbe Lowasa alikuwa amemfichia siri mwenzake lakini yakamfika aeona ngoja atue mzigo wa mtu mmoja ili wengi wafaidi.Maselef shukrani sana kwa kuipenda Title yangu. Hata picha yangu bomba sema mvivu mmoja ajiitaye washawasha ameikopi kiasi cha kunidhalilisha. Naye ni gamba tena la kiakili. Tuendelee kujadili CCM inavyoendelea kubaka taifa letu huku fisadi mkuu Jakaya Kikwete akijifanya atapambana na magamba wakati yeye ndiye gamba kuu.
Watanzania sasa amua wenyewe. Lowassa kwa mara nyingine amemshinda Kikwete je Bunge letu litaendelea kuchekelea kwa vile wote ni nyani wana mikia?
Haya chini ni maneno mazito aliyomwaga Lowassa akiamua kumwaga mboga baada ya Kikwete kutaka kumwaga ugali.
"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".
"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.
Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: "Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".
Maselef shukrani sana kwa kuipenda Title yangu. Hata picha yangu bomba sema mvivu mmoja ajiitaye washawasha ameikopi kiasi cha kunidhalilisha. Naye ni gamba tena la kiakili. Tuendelee kujadili CCM inavyoendelea kubaka taifa letu huku fisadi mkuu Jakaya Kikwete akijifanya atapambana na magamba wakati yeye ndiye gamba kuu.
Mi cjui bana, maana lishanichosha sasa....hata hivyo, ,kuna jambo moja ambalo nalifahamu kwa 100% ambalo naweza kulisimamia hata The Hague. Nakumbuka aliwahi kusema : "Mheshimiwa Spika, Nimedharirishwa sana! Nimechafuliwa sana! Nimetukanwa sana! Lakini najua, tatizo ni uwaziri mkuu!"
Leo hii: " tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015."
Sooner or later "Babaz Maaskofu, nimedharirishwa sana , nimechafuliwa sana, nimetukanwa sana! lakini kubwa ninalofahamu kwa vita hii ya sasa ni Unaibu Katibu Mkuu wa UN!"
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.
Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..
Wacha hasira mkuu Lowasa anaonekana ana mengi ya kutueleza ila ukumbuke mwanasiasa huongea ukweli kwenye jina lake tuu na sio hoja zake na mengineyo...lowasa haitaji huruma za jk bali jk ndio anahaha atamfadhili vipi lowasa kwa kufichiana siri...ikumbukwe kama jk angejiuzulu yeye ingekuwa balaa zaidi ndio maana akamuomba lowasa abebe adhabu yake ili aweze kujilinda na kumlinda yeye siasa mchezo wa hila
Lol..mwaka huu humu ndani lazima watakifahamu kiswahili fasaha!nimedharirishwa = nimedhalilishwa
nashauri tuzungumze hoja zaidi badala ya kutanguliza na kuanika chuki zetu dhidi ya watu.Mkuu mimi namlaumu JK kwa kuendelea kumpa free airtyme huyu jamaa, yaani alikuwa na nafasi mfano last year wangetoa jina lake kwenye ubunge, next kama walivyofanya kwenye kuwaondoa kwenye CC. Halafu wangemsongesha mahakamani awe bize huko.
Sasa inavyoonyesha JK anaplay uungwana na huyu jambazi ambaye will stop at nothing kutimiza his personal dreams. JK amechelewa kiasi kwamba lolote litakalomtokea EL kwa sasa kuhusu tuhuma za ufisadi itaonekana JK anamwandama.
Politics is so dirty!!!!!!!! Hivi unafikiri ingekuwa ni Mkapa EL angethubutu kubwabwaja maneno kama hayo?