Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Hii ni kweli Mkuu???
Ni kweli Daudi ni marehemu, lakini sioni connection ya kufa kwake na hizo ripoti. hakuna mlinzi wa dunia wote ni binadamu na tutakufa period.
[h=2]
icon1.png
Daudi Mwakawago afariki Dunia[/h]
mwakawago.jpg


Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam.

Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini, Ubunge Iringa Mjini, Uwaziri, Balozi wa Kudumu UN
quote_icon.png
By asha ngedere
Balozi Mwakawago amepata kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa na kiserikali enzi ya uhai wake, zikiwemo za kimataifa.

Amepata kuwa mbunge wa Iringa Mjini kwa miaka mingi, Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza nay a Pili pamoja na kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kabla ya kumpisha Balozi Augustine Mahiga anayeshikilia wadhifa huo hadi sasa.

Mwakawago alizaliwa mkoani Iringa mwaka 1939 na kupata elimu katika vyuo vikuu tofauti vya ndani na nje ya nchi vikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Makerere cha Uganda na Manchester cha Uingereza.

Baada ya kumaliza masomo yake Makerere, Balozi Mwakawago alikwenda kufanya kazi ya ualimu katika kilichokuwa Chuo cha Itikadi cha Chama cha Mapinduzi, Kivukoni na baadaye kuwa mkuu wa chuo hicho ambacho sasa kinaitwa Chuo cha Sayansi ya Jamii Kivukoni.

Aidha, Balozi Mwakawago amepata kushika nyadhifa kadhaa za kisiasa kwa miaka 20, akiwakilisha asasi tofauti zikiwemo za vyuo vikuu, vyama vya wafanyakazi na katika jimbo lake la uchaguzi la Iringa.

Serikalini, Balozi Mwakawago alishika nafasi mbalimbali ikiwemo ya uwaziri katika wizara mbalimbali ambazo ni Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni; Wizara ya Kazi; Wizara ya Utumishi, pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mwaka 1980 hadi 1982, Balozi Mwakawago aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Paul Mhaiki (sasa marehemu), baadaye akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia kuanzia mwaka 1991 hadi 1993.

Utumishi wake haukukomea hapo, kwani mwaka 1994 hadi 2003 alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na baadaye akawa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone kutoka mwaka 2004 hadi 2005.

Pamoja na kustaafu, Umoja wa Mataifa umekuwa ukimtumia kama mmoja wa wakufunzi wake katika kutoa mafunzo kwa viongozi wa baadaye katika umoja huo.

Aidha, amekuwa akishughulika na asasi ya kimataifa isiyokuwa ya kiserikali ya Miracle Corners of the World (MCW) yenye maskani yake nchini Marekani, ambapo kupitia asasi hiyo alikuwa akishughulikia uongozi wa vijana kidunia katika maeneo yenye matatizo ya kisiasa kama Mashariki ya Kati na katika nchi zilizopita katika migogoro ya kivita.

Balozi Mwakawago alikuwa mzalendo wa kweli, na hivi karibuni alikuwa akichangia mijadala na kuelezea kuhusu maadili ya uongozi, huku akipinga tabia ya ufisadi ya baadhi ya viongozi ambayo imeifanya serikali ionekane haifai.



 
Kwa taarifa tu baada ya ripoti hiyo ya mwaka 1997 iliyotolewa na Daud Mwakawago, huyo Daud Mwakawago hatunaye tena, yupo ahera.

Kwani ina maana watu wooooote waliokuwepo kipindi hicho wapo mpaka leo mzee?!!!Hata ditopile mzuzuri aliyekuwa na jk bega kwa bega nae hatunae tena kaka
 
Ni kweli Daudi ni marehemu, lakini sioni connection ya kufa kwake na hizo ripoti. hakuna mlinzi wa dunia wote ni binadamu na tutakufa period.
icon1.png
Daudi Mwakawago afariki Dunia

mwakawago.jpg


Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam.

Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini, Ubunge Iringa Mjini, Uwaziri, Balozi wa Kudumu UN​
Umri wa kawaida kabisa huo mtu kuishi, kwani mpaka ufike miaka 150?
 
Kwa hiyo sababu mkapa alitumia "busara" JK naye atumie "busara" ili E. Lowasa arudi kupewa number "yake" acheze kiungo na sio winga.

kazi ipo
Mi nawashangaa watu wa lowassa humu ndani,wamejipanga kushangilia ushindi ambao hawajaupata?lengo la wanaotaka kujivua gamba toka mwanzo lilikua ni kulipeleka hilo suala la kujivua gamba cc kwa kuomba kibali cha nec, niwaulize kibali cha nec kimetoka au hakijatoka?

Baada ya hapo kazi imebaki kwa cc kumchinjilia mbali huyo lowassa wenu, yeye ameshajua hilo kwani matumaini yake makubwa yalikua nec,kama nec wamemtosa kwa kuidhinisha kibali kwa cc ambako yeye hayumo na hana watu mnategemea nini?

Watu humu wamejiandaa kupotosha ukweli wa maamuzi yale ya nec ambayo hayaonyeshi dalili nzuri kwa lowassa makusudi ili kuwachanganya wasiojua........lowassa angekua kidedea kama nec ingedinda na kukataa suala hilo lipelekwe cc baliwangeshinikiza limalizwe ndani ya nec!lowassa ajiandae kwenda zake chadema tu!
 
“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 Kina Mzee Daudi Mwakawago Walikuja Na Mafaili Yakiwa Na Tuhuma Dhidi Ya Mtizamo Hasi Wa Jamii Dhidi Yako, Kwa Hiyo Wakati Ule Kama Si Busara Za Kina Mzee Mkapa Leo Usingekuwa Hapo Ulipo, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”

“Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.
 
Mmbwa koko ukimkimbiza atakimbi.

Na ukiongeza spidi katika kumkabili naye atakimbia sana tu. Ila pale ambapo ukimbizaji huo utakapomweka kila kona ni ukuta tu hamna pa kukimbilia zaidi basi ndipo hapo mtu utakapomgundua mmbwa koko na ukali wake wote pindi anaporudi kukukabili wewe moja kwa moja tena bila utani wowote.

Lowassa hivi sasa mgongo wake umetazama ukuta katika hili; ukweli wote kutoka wakati wowote

Watanzani tunachojua ni kwamba kosa la ufisadi mzito ulitendeka hivyo wahusika waote watupishe haraka bila kulialia na kulumbana hapa.
 
Si anajua udhaifu wote? na wakicheza atacheua kila kitu.
 
Ana kashfa ardhi, chini ya Mwinyi. Jamaa respnsibilities kubwa keshapewa sana, na ameprove tamaa yake....
Tatizo ni kuwa wale viongozi wa CCM wanaoonana na watu mitaani na vijijini, hasa ngazi za wilaya na mikoa wamegawanyika sana kutokana na hawa wapuuzi walio kwenye ngazi ya Tafa.
Njaa, tamaa, siasa na pesa ni combination mbaya sana..... almost like money and blood.
Ukweli mtupu Soby!

Inaelekea wewe upo upande wa gamba la JK.

Kaazi kweli kweli,CDM jipangeni tu,ila mjuwe ni magamba yapi yako honest kama yakitaka kujiunga na upinzani...Yale malaini malaini na yasiokuwa machafu sana...Teh teh teh...JF raha tupuu!
 
He is trying to grab a straw!, mbona ana options nyingi lakini anashindwa kuzitumia? Kuna vyama vingi vya upinzani, kuna kujiuzuru na kuachana na siasa, ana uwezo pia wa kuweka kila kitu wazi kwa manufaa ya taifa.

Ameamua kubeba mzigo mzito kutokana na kwamba hawezi kujinasua kutoka kwenye ufisadi, japo fikra zake zinamshawishi ajione ana unafuu kuliko wenzake kwenye medani za ufisadi uliovuka mipaka.
 
Mimi sina shida kabisa na hii issue,

Swali langu tu kwa wale waisokuwa magamba ambao wanampinga EL,je mna uhakika kuwa atashinda urais endapo atasimamishwa na CCM na ndiyo maana mnampinga?

Swali hili na wale ambao si magamba,na bado wanampinga EL kwa nguvu zao zote na wengine kumsafisha JK in the process.
 
Ni kawaida tu. Mtu unapobanwa sana unaamua kusema ukweli wote juu ya jambo husika; na ukibanwa zaidi utakuwa hata tayari kusema uwongo kama utajiridhisha kwamba njia hiyo itakuokoa toka kwa wanaokuwinda kama kware.
 
Sioni la maana, sasa kama Kikwete alimwambia angoje ushauri wa Makatibu wakuu kuna kosa hapo?

Au ya 1997 Zanzibar yanahusu nini?

Hizi habari zimekaa kiudakuudaku hazina mshiko na zimekaa kifataani fataani, mtu aongee kuhusu Nape kwa dakika 7 halafu humu uweke maneno hayajai hata mstari mmoja? Hata angekuwa haongei anaya "spell" tu hayo maneno basi dakika 7 angejaza ukurasa.

Hizi habari ni za kifataani na hazina la maana hata moja, jamani hebu niambieni hapo kuna nini cha maana?

Pole sana dada faizaly vumilia tu

 
hivi lowasa hajavuliwa gamba tu...nape vipi umeshindwa kazi...
Nape siyo level ya Lowassa,JK ndiye level yake,ana uwezo wa kumtimua,mbona hafanyi hivyo?

Ndo maana mimi naona hii si issue wala nini,kwasababu mimi si gamba,na kwa namna ninavyoiona issue,siyo EL tu alitakiwa ajiuzulu,ni serikali yote ilitakiwa isiwepo madarakani.

Ndivyo nionavyo.
 
Ukweli kwenye hicho chama mafisadi ni wengi tu - anachotaka Lowasa ni waendeleze utamaduni wa kulindana kwani wakianikana watakaobaki ni wachache mno!
 
Hapa inakosekana pressure group ya kusukuma hili likikundi la mafisadi likapisha eneo takatifu la nchi. Tunakosa mikakati iliyojengeka ya kuweza kumaliza kazi tuliyoianza siku nyingi wanaJF. Serikali haina msafi, lakini bado tunazidi kupiga kelele bila kuchukua tahadhali mapema kabla ya kitu kibaya hakijatokea. tafakari!
 
natamani ningekuwa ukumbini nione taswira ya Uso wa mkuu wa kaya haya yakitamkwa
 
Lowasa komaa, unafaa kuwa rais wa nchi hii, tuko nyuma yako tunakusapot, 2015 RAIS KAMA SIO LOWASA BASI NI DR. SLAA. HAWA ............ WAMETUHARIBIA NCHI YETU KABISA.
 
Back
Top Bottom