"Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 Kina Mzee Daudi Mwakawago Walikuja Na Mafaili Yakiwa Na Tuhuma Dhidi Ya Mtizamo Hasi Wa Jamii Dhidi Yako, Kwa Hiyo Wakati Ule Kama Si Busara Za Kina Mzee Mkapa Leo Usingekuwa Hapo Ulipo, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"
"Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,"
"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".
"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.