Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Ndio maana baadhi yetu tunahoji kwa nini Lowasa hakujiuzulu wakati ule JK alipomkatalia kuuvunja mkataba wa Richmond baada ya kumpigia simu akiwa nje ya nchi? Kwa nini suala hili liliendelea kuzimwazimwa na Lowasa mwenyewe kwa kuwatumia akina Hosea hadi Bunge lilipounda kamati ile ya akina Mwakyembe?
Alikuwa akimlinda JK,na sasa hivi JK ndie anamlinda kwa siri...Umesahau JK alisema hawakukutana mtaani?

Umesahau alisema kulazimika kujiuzulu kwa EL ilikuwa ni "Ajali ya kisiasa"?
 
Lowassa ametumbukia kwenye pipa la lami. Anachojaribu kukifanya ni kujisafisha kwa sabuni, kamwe hawezi kutakata
Nani kakudanganya wewe lowasa katolewa kafara ni kama vile sokoine waziri mkuu alikuwa strong than prezdaa wewe wa mwaka gani ni mambo ya protoco muwe mnauliza kwa wakubwa wenu ki umri boss.
 
Wameniudhi sana NEC ya CCM. Badala ya kuikabidhi dola watuhumiwa wa ufisadi ili sheria ichukue mkondo wake wao wanalirudisha suala hili kwenye CC yao. Tumefikaje hapa pa kubembeleza wahalifu kiasi hiki? Waachieni akina Mramba basi ah!
wanatamani sana watanzania wasisikie wala kuona kinachoendelea huko dodoma. halafu, mbona kina mramba wanapeta tu? unadhani wana hatia wale?
 
Lowasa anapata kiburi hicho kwa kuwa dili la Richmond lilikuwa la JK, kwa vile JK ni mwoga wa kupiga ishu na Lowasa ana kifua ndiyo akampa jukumu la kusimamia hilo dili. Na kama ambavyo amekuwa akisema mara kwa mara kuwa yeye na Kikwete hawajakutana njiani, ni kuwa anajua A TO Z ya ufisadi wa mshikaji wake ndiyo maana anapata ujasiri wa kumkabili kwa uso wa mbuzi tena mbele ya wa-NEC akijua kuwa jamaa yake yuko weak.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hii ndio Kamati ya Maadili ya ccm iliyokabidhiwa rungu la kumsulubu Lowassa...ina wajumbe wazito, baadhi yao ni:
Mwenyekiti Kikwete, Makamu wenyeviti, Pius Msekwa na Amani Karume, Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Iddi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Manaibu Katibu Mkuu, Kapteni mstaafu John Chiligati na Vuai Ali Vuai.

Sasa wapambe wa lowassa mnaopotosha mambo hapa kwamba lowassa kaibuka kidedea kwa kulia lia kwake mpime wenyewe lowassa atatoka hapa!

Halafu kumbukeni ni hii ya january makamba alivyomuudhi bosi wake kwa kujaribu kutishia nyau!!!!!!!

January Makamba amkera Kikwete


Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya CCM, January Makamba anaelezwa kuwa aliwasilisha mada, juzi Jumatatu, inayozungumzia hali ya kisiasa nchini akipendekeza uamuzi wa kuwachukulia hatua kina Lowassa na Chenge usitishwe ili kuepuka mgawanyiko ndani ya chama.

Katika kujenga hoja, mjumbe huyo alitoa mfano wa mjadala wa Katiba na nguvu kubwa ya CHADEMA nchi nzima kuwa inabidi CCM iepuke mgawanyiko unaoweza kutokea kwa kuwang'oa wenzao wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Hata hivyo, mapendekezo hayo yalionekana kumkera Mwenyekiti, Rais Kikwete, ambaye alihoji ni nani aliyesababisha mgawanyiko, na nini madhara ya kisiasa kwa CCM kutokua na msimamo katika kukemea uovu.

Rais Kikwete alipoonyesha kupinga moja kwa moja mawazo ya kuahirisha ‘uvuaji gamba', alibadili hali ya hewa ndani ya kikao hicho.

Mwananchi wamecover hiyo habari kiupotoshaji,hali ni mbaya kwa lowassa,ajipange tu upya na wapambe wake la sivyo anakwenda na maji,labda ahamie chadema ndio dawa iliyobaki kama anataka kuwakomoa ccm kwa kuwa still ana ushawishi kwa nyie mnaomtetea humu,si mtamfuata akija upinzani au nyie ccm damu?
 
huyu jamaa huwa simu underestimate hata siku moja...yaani ana mambo ya hatari sana na anajua sana kujipanga...JK hawezi kumgusa huyu...kwa hali ilivokuwa pale dodoma na kama haya ndo aliongea basi JK yuko mashakani sana
 
Chama hiki ni cha kujenga nchi kweli? I doubt!


ccm inajenga nchi sio maisha ya watu!!!!!hiyo kauli mbiu yao kwanza lazima muielewe,maana imekaa kiutata utata sana ukiitafakari,ndio mana hawana uchungu na watu
 
"Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 Kina Mzee Daudi Mwakawago Walikuja Na Mafaili Yakiwa Na Tuhuma Dhidi Ya Mtizamo Hasi Wa Jamii Dhidi Yako, Kwa Hiyo Wakati Ule Kama Si Busara Za Kina Mzee Mkapa Leo Usingekuwa Hapo Ulipo, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"

"Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,"

"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.
[/QUOTE]

Hivi siku hizi wameacha ule utamaduni ni wao wa kuwakolimba wenzao???????
 
"Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 Kina Mzee Daudi Mwakawago Walikuja Na Mafaili Yakiwa Na Tuhuma Dhidi Ya Mtizamo Hasi Wa Jamii Dhidi Yako, Kwa Hiyo Wakati Ule Kama Si Busara Za Kina Mzee Mkapa Leo Usingekuwa Hapo Ulipo, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"

"Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,"

"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.

Jeuri yake ni siri za wizi wa mali zetu sasa hapa yeye anajua kwamba alikwapua ila JK alikwapua akaacha alama nyuma easy to trace akianza kumwaga tu JK kitanzini ndiyo maana anaunguruma hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa wale wafugaji wanafahamu wakati wa mvua zizi la ng'ombe hujaa matope sana. Kutokana na karaha ya tope hilo madume hujaribu kuwa wakali kweli ili kulinda sehemu yake iliyo na uafadhali. Lakini ukweli ni kwamba zizi lote lilishajaa matope tupu.

Tuendelee kuangalia hiyo sarakasi.
 
Jana Mh Edward Lowassa hatimaye alitamka maneno yanayomfanya kuonekana hakushiriki katika ufisadi wa Richmond kwa kumpa lawama (zote) Rais Jakaya Kikwete.

"Alibi" ya Lowassa kuwa alimpigia simu Rais kutaka kusitishwa kwa Richmond baada ya yeye kugundua mapema kua ilikua na dosari haileti mantiki yeyote zaidi ya kumuonyesha lowassa kuwa ni mpiganaji tu wa kisiasa na wala siyo kiongozi mahiri wala safi.

kama Rostam ndiyo anatajwa kuwa msukaji mkubwa wa mpango wa Richmond (mpaka kusafiri Marekani kutafuta hawa "wawekezaji") na ni Rostam huyu huyu aliyemsukuma Kikwete amweke Lowassa Waziri Mkuu na ni Rostam huyu huyu swahiba mkubwa kisiasa na kibiashara na Lowassa itakuaje Lowassa anayeaamini siasa za kulindana amtose Rostam kwa kumshauri kwa uwazi mkubwa Kikwete kuwa Richmond ivunjwe?

hii inanipa jibu moja tu Lowassa na Rostam walijua lazima wawe na kinga kama hili suala feki ikijulikana na hapo ndipo walipopiga hii simu kwa JK( kama "alibi") akiwa anakula "raha nje ya nchi "anasherehekea" bado ushindi wa Urais uliosababishwa na hawa maswahiba wake huku wakiwa wanaonyesha wasiwasi Kidogo wa mkataba huu (huku wakijua Rais ana maslahi yake katika hili na atakua mzito kukubaliana moja kwa moja na hili la kusitishwa kwa mkataba huku na wenyewe wakiwashinikiza wahusika wengine hapa Tanzania kuupitisha mkataba ).

Unataka kuniambia katika suala zima hili Lowassa alimpigia simu boss wake simu moja tu tena akiwa nje ya nchi kuonyesha wasiwasi wa dili hili ambalo yeye alikua hapati "vijisenti" vyetu vyovyote na kuna hatari ya kutumiwa yeye na ofisi yake kumuaribia kisiasa kama ikija gundulika? Lowassa ana akili zaidi ya hizi na hii inaonyesha kuhusika kwake m1 kwa m1 na Richmond na kwamba hili aliloongea jana ni "alibi tu iliyopikwa kama tahadhari ikiwa Richmond ingekuja kunuka....

Na hata kama hii simu siyo alibi yake mh lowassa na Kikwete alihusika 100% lakini hii haimfanyi Lowassa kuwa msafi kwani kama alijua uozo kwa nini aliingiza ofisi yake katika mchakato wa Tender pale TANESCO kinyume na taratibu zilizopo, (hii inamfanya Lowassa kuwa mshiriki mkuu hata kama alikua anatumiwa na Kikwete).. hapa hawezi kuwa exonerated na uchafu wa Richmond kwenye macho na hukumu ya watanzania..
 
Lowasa anapata kiburi hicho kwa kuwa dili la Richmond lilikuwa la JK, kwa vile JK ni mwoga wa kupiga ishu na Lowasa ana kifua ndiyo akampa jukumu la kusimamia hilo dili. Na kama ambavyo amekuwa akisema mara kwa mara kuwa yeye na Kikwete hawajakutana njiani, ni kuwa anajua A TO Z ya ufisadi wa mshikaji wake ndiyo maana anapata ujasiri wa kumkabili kwa uso wa mbuzi tena mbele ya wa-NEC akijua kuwa jamaa yake yuko weak.

Athari za katiba mbovu inayowapa watu wachache maamuzi ndiyo hapa inaonekana wazi. How can two people's make us all dance to their tune? Hapa ilibidi wote watupishe waka sort mambo yao huko kama kupigana wapigane atakaye mshinda mwenzake atambue ndiyo mwanaume..Sasa sote tuko tunasubiri malumbano ya makundi ya watu huku kila siku maisha yakiendelea kuporomoka. I am tired na hapa hakuna fisadi atakaye pona bora tuanza upya kama taifa!
 
“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 Kina Mzee Daudi Mwakawago Walikuja Na Mafaili Yakiwa Na Tuhuma Dhidi Ya Mtizamo Hasi Wa Jamii Dhidi Yako, Kwa Hiyo Wakati Ule Kama Si Busara Za Kina Mzee Mkapa Leo Usingekuwa Hapo Ulipo, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”

“Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

EL will never get away with this.....JK will hit back hard, very very hard!
 
Nani ana ubavu wa kumgusa EL? Mkulu kabisa hana ubavu wa kusema kitu maana wametoka mbali hao na siri zote za Mkulu EL anazijua. Mtapiga kelele ila mwisho wa siku EL will be your next president. He will turn heaven and earth to achieve his dream and Mkulu is there to make it come true.
 
"mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule zanzibar mwaka 1997 kina mzee daudi mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina mzee mkapa leo usingekuwa hapo ulipo, ulisema kwamba kuwa rais ni mipango ya mungu,"

"mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,"

"mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana ccm wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji lowassa.
inafahamika wazi ya kua gamba ni kuanzia rais mwenyewe jk. Ni upunguani kujaribu kijivua gamba ambapo asilimia 99 ya viongozi wa ccm na serikali ni magamba!mungu ibariki tanzania
 
... NGUVU NA JEURI ya Edward Lowasa inatokana na kujengwa na UDHAIFU unaomzunguka na watu wanyoge, legelege na walioupoteza heshima na matumaini kama yeye mwenyewe!

... CCM is no LONGER!!
 
my Take. gamba number one ccm ni ******, liking'oka basi wengineo wote watafuata huko
 
Back
Top Bottom