Nimeshangazwa na udhaifu wa hoja za Lowassa, hoja dhaifu kama afya yake. Sasa naamini kabisa kuwa Lowassa hajawahi kuisoma taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe kuhusu Richmond. Angelikuwa kaisoma taarifa hiyo, asingeliweza kutoa hoja chovu ya yeye kutaka kuvunja mkataba wa Richmond, kwani Kamati Teule iliijadili hoja hiyo na kuitupilia mbali kuwa ya kipuuzi. Kwa nini Kamati ya Mwakyembe iliita hoja hiyo ya kipuuzi?
Ni kwa sababu, madudu yote ya mchakato wa zabuni mpaka kuiweka kando sheria ya manunuzi kwa amri ya Lowassa na kuipa upendeleo kampuni hewa ya Richmond, vilevile kwa maelekezo ya Lowassa, yalifanyika kati ya Aprili na Juni mwaka 2006. Wazo la Bw. Lowassa kuvunja mkataba lilikuja mwezi wa nane (Agosti) baada ya kelele dhidi ya Richmond kuanza kusikika. Hoja hiyo haimsaidii kabisa Lowassa, inazidi kumwonesha kuwa mtu asiye makini, hasomi kumbukumbu vizuri na ni mbabaishaji wa hali ya juu. Kwa nini haendi mahakamani kuwadai akina Mwakyembe fidia ya kuchafuliwa jina lake, kama hawatamvua nguo hadharani?
X-Mbunge, Dar es Salaam.