Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Richmond richmond richmond. We are so tired with this dude richmond. How about meremeta,iptl and other big scandals. I am stil believe that, most of ccm members are not clean. What hapen now in magamba party is due to prensidential aspiration in 2015. Over
 
Nlishawahi sema ktk jukwaa hili

kuwa HAKUNA KAMWE MWENYE USHAHIDI akajitokeza na kusema kuwa Mh Lowasa kafanya hivi na hili HAKUNA tutabaki tukipige kelele humu Jf kwa kubadilisha ukweli kuwa uongo

NANI MWENYE USHAHIDI APELEKE
Nape,Chiligati,nani hata humu Jf nani?
hakuna kwahiyo tunasema no research to right to speak

Bado Mh Lowasa nauwezo wa kuongoza hii nchi kama atapata nafasi

Afadhali best unisaidie,kweli tuanze kujadili hoja ya kamati ya richmond leo....!cha kushangaza sasa wote waliohusika walalamikaji kwa walalamikiwa wameshashika na nyadhifa nyingine tena vyeti tu. Kupotezeana nafasi za kufikiri tu Richmond toka mwaka 2007 leo 2011. Humumu tayari na kumetolewa mwanya ambaye hajaridhika apeleke ushahidi .......tunajadili nini sasa?????????
 
Wewe mngese peleka makundi yako kwa magamba wenzio kwa watu smart kama sisi tushajuwa kuwa wewe gamba janga la kitaifa so kama kakutuma ba@sha wako wa msoga mwambie mkajipange ziwe nyie.

Toka jana kuna wapenzi na mashabiki wa CCM waliokuwa wanamshambulia Lowasa wamepotea JF.
 
Jk na Lowasa ni maswaiba wa siku nyingi wala msitegemee kama wanaweza kukeukana leo! CCM imeoza na kunuka imeanza kilichobaki ni kuzikwa tu! na mazishi yao yanakuja! Mafisafi makubwa haya! Magamba yanawashinda kuvua kwani ni magumu sana! Nyambafu zao! lazima tuwasafishe wote. Watausikia uras bombani tu!
 
Naomba ninukuu baadhi ya maneno yake wakati ana-redesign (strategies), alisema "kama wote tutaamuwa kuchafuwana, hakuna atakeyebaki". Mwisho wa kunukuu. The guy is the smartest i ever seen in third world politics. He will get there. Mark my word.
 
Mi nawashangaa watu wa lowassa humu ndani,wamejipanga kushangilia ushindi ambao hawajaupata?lengo la wanaotaka kujivua gamba toka mwanzo lilikua ni kulipeleka hilo suala la kujivua gamba cc kwa kuomba kibali cha nec, niwaulize kibali cha nec kimetoka au hakijatoka?

Baada ya hapo kazi imebaki kwa cc kumchinjilia mbali huyo lowassa wenu, yeye ameshajua hilo kwani matumaini yake makubwa yalikua nec,kama nec wamemtosa kwa kuidhinisha kibali kwa cc ambako yeye hayumo na hana watu mnategemea nini?

Watu humu wamejiandaa kupotosha ukweli wa maamuzi yale ya nec ambayo hayaonyeshi dalili nzuri kwa lowassa makusudi ili kuwachanganya wasiojua........lowassa angekua kidedea kama nec ingedinda na kukataa suala hilo lipelekwe cc baliwangeshinikiza limalizwe ndani ya nec!lowassa ajiandae kwenda zake chadema tu!

Mkuu mi nawashangaa sana humu mashabiki wa Lowassa. Maana kama ni mpira upo half time, halafu yuko nyuma kwa goli
moja,... kwa vile mpira bado unadunda lolote linaweza kutokea kwenye CC, ila si jambo la kushangilia kabisa kwa mashabiki wa Lowassa kwa issue ya gamba kurudishwa CC. Wangeiua na kuizika palepale kwenye Nec.

Kumbuka azimio la gamba ndio litawaongoza wajumbe wa CC na azimio la kujivua gamba halikutamka ushahidi wa kimahakama, limeongelea wale "wanao tajwatajwa kwenye kashfa" na wananchi.. Kama bado kuna mtu anategemea ushahidi wa kimahakama you better go figure chenga ya mwili aliyopigwa Lowassa.

CC haina wenyeviti na makatibu wa mikoa(watu wake ni almost 3/4 ya kundi hili), haina wabunge wake(ambao ni wote kumi wanaowakilisha bunge Nec), haina wajumbe wa UVCCM except Kaimu Mwenyekiti Malissa(Nec alikua na wajumbe 10 kati ya 12 wa UVCCM), kwa kifupi he has a mountain to climb. Sanasana amebaki Malissa, Pindi Chana, na January Makamba, Khatib haeleweki, Wassira haeleweki na Mwenyekiti haeleweki. Wajumbe wa CC waliobaki wote si watu wa njaa ya kumtumikia mtu binafsi...
 
Wacha hasira mkuu Lowasa anaonekana ana mengi ya kutueleza ila ukumbuke mwanasiasa huongea ukweli kwenye jina lake tuu na sio hoja zake na mengineyo...lowasa haitaji huruma za jk bali jk ndio anahaha atamfadhili vipi lowasa kwa kufichiana siri...ikumbukwe kama jk angejiuzulu yeye ingekuwa balaa zaidi ndio maana akamuomba lowasa abebe adhabu yake ili aweze kujilinda na kumlinda yeye siasa mchezo wa hila
Well said. This is absolutely true.
 
Jana Mh. Lowasa alimwambia Kikwete kwenye kikao cha NEC kuwa alipotaka kuvunja Mkataba na Richmond Kikwete alimzuia. Rais Kikwete aliwahi kutuambia Watanzania February mwaka huu wakati akihutubia Wananchi wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya CCM kuwa hawajui Richmond wala Dowans. Sasa wandugu Rais wetu ametudanganya Watanzania au vipi? Ninauzoefu wa maneno yasiyodhibiti ya Rais wetu. Sasa na hili nalo limenishtua tena tufanyeje Rais ajue hatupendi kudanganywa?
 
Msema kweli mtu wa Mungu..Bora Lowassa kuliko JK kwa matendo....angekuwa na maamuzi magumu,,,,no Sharobaro
 
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....

Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..

Pole mkuu! looks like u dont have a clear picture of what Richmond is! Bila JK Richmond isingekuwepo, that is a naked truth!
 
Lowasa anapata kiburi hicho kwa kuwa dili la Richmond lilikuwa la JK, kwa vile JK ni mwoga wa kupiga ishu na Lowasa ana kifua ndiyo akampa jukumu la kusimamia hilo dili. Na kama ambavyo amekuwa akisema mara kwa mara kuwa yeye na Kikwete hawajakutana njiani, ni kuwa anajua A TO Z ya ufisadi wa mshikaji wake ndiyo maana anapata ujasiri wa kumkabili kwa uso wa mbuzi tena mbele ya wa-NEC akijua kuwa jamaa yake yuko weak.
Iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiigweeeeeee!
 
we mjinga! Jifunike kichwani maana naona umeacha blanketi likashuka sakafuni. Halafu morning uje humu jamvini. Unakurupuka tu!

Hii issue ya magamba inawafanya watu wawe na hasira sana!Sijui ni kwa nini!
 
we mjinga! Jifunike kichwani maana naona umeacha blanketi likashuka sakafuni. Halafu morning uje humu jamvini. Unakurupuka tu!

Acha kutoka povu wewe bwawa la maini,mzalendo mwenzio kauliza tu ajuzwe,hujui hali yake na yupo wapi...acha kujifanya unajua kuropokea wenzio...tabia chafu sana hiyo!
 
Kwa sababu walimsema sana Lowassa na kuona wengine CCM ni safi...sasa aibu inakuja taratibu :A S 465:utaona na kusikia mengi tu
 
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....

Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..

Rangi zenu wanafiki zinaanza kujionyesha taratibu..bomu hili ulitakiwa kulichukua na kwenda nalo vizuri...hata kama uko upande wa JK!!! JK kaanikwa hakuna logic ya Lowasa kuhukumiwa wakati kila kitu JK alijua na ndiye bosi wake! RICHMOND=JK! kama hutaki muulize Dr. Slaa..mbaya zaidi JK anamtuma Nape akamchafue Lowasa!

My friend sasa hivi WAPINZANI WA CCM NI NYIE WENYEWE CCM! tutasikia na kuona mengi..hajaja mtoto wa Membe anaitwa Mbopo, bado dada yako mtoto wa JK FaizaFoxy......mbona JF RRRAHA!!!

CDM kazi rahisi tu hapa!
 
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.

Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..

Mkuu leo umeshikwa pabaya..rudisha mood yako, unaaibika..

If Lowasa mwizi then sema Lowasa na Kikwete ni wezi!!!

ulijiaminisha uliandika, unaona mambo yanageuka unabwabwaja

Nyerere siyo bible wala quran tena siyo pythogoras theorem..this is politics!!

RICHMOND=JK! sema lingine mnafiki mkubwa we!
 
Waberoya wewe huyo? nendeni taratibu...
 
Mkuu mi nawashangaa sana humu mashabiki wa Lowassa. Maana kama ni mpira upo half time, halafu yuko nyuma kwa goli
moja,... kwa vile mpira bado unadunda lolote linaweza kutokea kwenye CC, ila si jambo la kushangilia kabisa kwa mashabiki wa Lowassa kwa issue ya gamba kurudishwa CC. Wangeiua na kuizika palepale kwenye Nec.

Kumbuka azimio la gamba ndio litawaongoza wajumbe wa CC na azimio la kujivua gamba halikutamka ushahidi wa kimahakama, limeongelea wale "wanao tajwatajwa kwenye kashfa" na wananchi.. Kama bado kuna mtu anategemea ushahidi wa kimahakama you better go figure chenga ya mwili aliyopigwa Lowassa.

CC haina wenyeviti na makatibu wa mikoa(watu wake ni almost 3/4 ya kundi hili), haina wabunge wake(ambao ni wote kumi wanaowakilisha bunge Nec), haina wajumbe wa UVCCM except Kaimu Mwenyekiti Malissa(Nec alikua na wajumbe 10 kati ya 12 wa UVCCM), kwa kifupi he has a mountain to climb. Sanasana amebaki Malissa, Pindi Chana, na January Makamba, Khatib haeleweki, Wassira haeleweki na Mwenyekiti haeleweki. Wajumbe wa CC waliobaki wote si watu wa njaa ya kumtumikia mtu binafsi...

kamanda we waache watakuja tena hapa kulia lia oooh kaonewa,lowassa mzee wangu namuheshimu sana lakini kiukweli maji yako shingoni,hakutegemea lile suala kuvuka mstari wa nec akijiaminisha anawafuasi wengi nec ambao wangemtetea,toka jana namtafute kwenye simu hapokei na kama humu ndani kuna mtu anajuana na yule mzee aniambe hapa kama anapokea simu,na sio kawaida yake kwa tunaomjua,hii ya kujifanya kushangilia ni mkakati walioupanga watu wake kwamba mambo yakienda ndivyo sivyo wao watateka media na mitandao kama hii ili kuwachanganya watu na cc itoke kwenye mstari kwa kitisho kwamba wananchi hawataielewa cc ikimvua gamba,strategy dhaifu ambayo sidhani kama itafanikiwa!

Suala la nape na chiligati eti watashughulikiwa ni kumfuta machozi lowassa tu aone chama kiko fair,lakini watapewa onyo tu,habari ndio hiyo,chukueni maneno yangu mje mnihukumu huko mbele kama haya niyasemayo hayatatokea!mnojuana na januari makamba muulizeni nini kilimpata alipojaribu kusimama mkutanoni nec na kutaka kushawishi hoja ya gamba izimwe!ile haizimiki tena wadau achaneni na propaganda za wapambe wa lowassa!
 
Back
Top Bottom