Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

majuzi hapa Muheshimiwa Lowassa aliiitisha kikao na waandishi wa habari akawaambia dhumuni la kikao hicho ni kuwaeleza taarifa aliyo nayo.
Then baada ya waandishi kufika ikabadilshwa ratiba na kuambiwa kuwa Lowassa kawaita kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi.

Nini kilifichwa pale?
Muheshimiwa Lowassa ni Rais wetu atakayetutoa ICU na kutupeleka ktk nchi ya Kanani.

Inshaaalah

Lowassa hawezi kututoa Misri na kutufikisha Canaan kwasababu yeye mwenyewe ni mtumwa wa Rostam Aziz; Huyu mamvi akiukwaa urais mjue mtawala atakuwa Rostam na mawziri wake watakuwa wakina Serukamba, Masha , Makongoro Mahanga na masaburi. Hawa ndio wataleta maendeleo kwa nchi kweli?
 
only Allah can stop Honorable Lowassa...
no one else.
Mark n bind it

hizi ndo akili zenu MAGAMBA ujinga mwingi na hamjiamini hilo loote linatokana na kubebana!
 
Lowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%

Soma nyakati. Lowasa alisha tiwa kwenye black listed yakuwa rais wa Taifa hili tangu enz za J. K. Nyerere. Kikwete anamalizia. Tukumbuke siri za nch hazina urafiki ila kufuwatwa tu. Kikwete anaenda kumalizia itimisho.
 
Acha hadithi za kutunga ww, kama barua ya kujiuzulu ilikubaliwa usiku wa manane, mbona hautuelezi nini kilimfanya EL kutangaza bungeni asubuhi yake kujiuzulu, na barua hiyo ya kukubaliwa EL kujiuzulu alipewa nani wakati hata spika wa kipindi hicho amewahi kukuaririwa akisema kujiuzulu kwa EL ndilo jambo lililomshtua mno kipindi cha uongozi wake- Hizi hadithi zenu za kutunga pelekeni huko vijiweni kwenu!!!

Alipewa barua usiku huo huo. Na hakuwa na jinsi maana tayari ilishajiuzulu. Bungeni alitoa tu ripoti
 
Jinsi kikao kilivyoendeshwa nimeona mpangilio ufuatao.

Mkapa ambaye ni dikteta mkubwa na mla nyama za watu ameshika usukani. Kwa kutumia hulka yake hii na karama zake ameteka mpango mzima na ninaamini kama siyo mkono wa Mungu atatufikisha anakotaka.

Sumaye, rafiki na raisi mtarajiwa wa ndugu Nkapa ameokoa EL asivuliwe gamba na kuipa nguvu zaidi kambi ya EL ili hapo baadaye imuunge mkono na wengine wamsaliti EL wakati wa uraisi wa 2015. Itambulike kuwa Sumaye atakubalika zaidi kwa wananchi kuliko EL lakini hana ujasiri na ngawira kama za EL kuhamasisha uma kwa lengo hilo kama anavyo fanya EL kwa kasi kubwa.

EL anasiri nzito ya Richmond na anaitumia kama silaha, alipenda sana aitumie kujikosha kwa jamii asionekane fisadi ili tamaa yake ya uraisi itimie kwa urahisi lakini amezuiwa na jk kwa sababu zinazojulikana zaidi kwao kuliko kwa jamii. Kwa tabia ya ugeugeu wa swahiba wake na uwoga na kutokujiamini kwenye kazi zake, zaidi kwa vile anapenda sana sifa na kuonekana msafi anaweza kumwangusia kipigo cha woga EL kisogani akammaliza.

Kwa kuhitimisha che nkapa ameshika nafasi ya mwenyekiti wa sisiemu, atapenda raisi ajaye awe fisadi au atakaye mlinda, kwake hakuna mbaya kati ya EL na Sumaye lakini atampenda zaidi Sumaye na na atafanya kila atakaloweza kumpatia SUmaye. Ili kulinda ufisade wa mafisadi wote wa sisiemu na hasa wa nkapa na jk KATIBA MPYA haipo kabisa hata nini kifanyike, kwao na wale wote waliopo madarakani ni nafuu Watanzania wote wafe kuliko wao washitakiwe. Tumaini kidogo lipo kwenye tabia ya ugeugeu wa jk na hasa msaada wa Mungu.

Kwa wanaharakati na CDM tuonyesheeni njia na Mungu atakuwa upande wenu, nilazima tujikomboe mikononi mwa hawa mafisadi Mkapa na JK na maswahiba wao
 
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya “kuigiza” kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. [/QUOTE]

Unajua nini? Wote ni wajanja, lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mjanja aliekulia Monduli na mjanja aliyekulia Magomeni!!!

Wajanja wa magomeni wengi wanauza ice cream, kashata na kahawa!!
 
Lowassa ni chaguo la Mungu...
tuombe uzima mpaka 2015 atakaposhinda ktk uchaguzi na kututoa huku ktk nchi ya utumwani na kutupeleka ktk nchi ya kanani...
Tuseme inshaalah

Lowasa huyu huyu au mwingine? Si huyu aliyetuambia uchumi wa nchi unapaa? Si huyu aliyekuja kutudanganya na mvua ya kutengeneza toka thailand? Si huyu aliyefanya madudu ya Richmond? Huyu ndo awe rais wa tz???

sitarajii watanzania wataruhusu jambo baya kama hilo. Natamani ccm wampitishe awe mgombea wao ili nchi ikombolewe! UNITED WE STAND against evils.
 
ACHA MAGUGU YAMEE PAMOJA NA NGANO ZIKIKUA VITAJITENGA.
kama waswhili wasemavyo uongo hujitenga na ukweli. Lowasa alibebeshwa zigo la Richmond..... Kwa kipindi chote alikaa kimya.. hajawahi kujitetea katika vyombo vya habari wala mahali popote...... sipendi kumuhusisha mungu lakini naona ukweli umeanza kuonekana na mpaka kufikia 2015 kila kitu kitakuwa hadharani.
 
duuh,kweli mmejiandaa kuitia najisi nchi hiii, endeleeni lakini maisha hayaishii tu duniani Mungu anatusubiri pia
 
Shairi nimelikubali! Tungependa utuletee shairi linalomuhusu hicho kibabu mkono wa kulia! nasikia ndio kashikilia mikoba ya hicho chama!
 
`take it from my understanding man..!Kusema EL ameshashinda ni mapema mno,tena mie naona nddio amewekwa kwenye danger zone zaid. Kwanini?kumbuka EL aliuwa anauwezo wa kuomba u rais kabla ya JK,lkn JK alianza jiulize why?ikaja EL akapewa U PM miaka 2 tu nje, JK rais..hapo...,richmond EL kakiri mwenyewe alibeba mzigo wa chama na serikali ....JK hakubeba hapo...twende pamoja sasa kuna kila dalili EL bado anataka kuendelea na siasa na pengine u rais aupate ndio maana hajaachia wadhifa kama gamba. My take....ukiangalia mtiriko wote EL ndio huwa anakuwa looser, na ujue JK awezi kuwa na uhakika asilimia 100 kuwa EL ameridhika na mambo hayo yaliyotokea na kama anaamini hivyo basi nae lolote laweza mpata mbeleni maana EL mekuwa kwenye matatizo na shid anyingi wakati wa uongozi wake JK hivyo haujui atakufanyia nini. Ngoma bado si swali kwa EL sema kama wataaminiana kiukweli hili imeisha,lkn bila trust hali kisiasa si swali kwa EL maana NEC imeongeza muda wa mjadala wa swala hilo, hivyo EL bado haja jisafisha na muda unaenda kujipanga kugombea u Rais.

Ningekuwa mie EL kweli na hali ilivyouwa dodoma NEC juzi ningeakikisha mie na wanaonisupport hilo swala linaisha pale bila kurudi CC,na kama ingekula kwangu basi maana hata mbele inaweza kula kwangu. Alishakuwa ameteka NEC kwa ushindi na ndio maana hoja ya kurudisha CC imepita kirahisi tu sasa alishindwa nini kujinasua katika hilo. Huu mchelchelea wake EL ndio unamfanya atumie nguvu na muda mwingi katika progress za siasa zake.

By Political Analyst
 
shairi lenyewe hivyooooooo, ingawa una ujumbe mzuri.
 
Back
Top Bottom