Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Duh!! Kuna watu nilikuwa nadhani zimetimia kumbe EMPTY!!
Tatzo la watz tunajijari zaidi paspo kufikiri mwenzie anaishije/ataishije!! Mtu akishapewa vijisenti tu vya mlo mmoja anasahau alikotoka na hajiulizi vikiisha itakuwaje, na paspo kufukiri hiyo kazi anayoenda kuifanya ina madhara kiasi gani!! Watu wa aina hii bora wafe tu hawana maana!!
Mtu una akili zako unathubutu sema nitatembea uchi!!?? Tena kwa ujinga wa hivi? Alafu mnajiita GT!! Ebu jaribu kufikiria japo kidogo hata jamii inayokuzunguka inasoma kwamba "utatembea uchi!!" tena kwasababu ya Lowasa!! Kama haya yanasemwa na mtu ambaye anajiita msomi kwenye mabandiko yake kila siku, basi JF imedhalilishwa!!
HIZI POINT SIO ZA GT!!
 
Tukiacha his black side, Lowassa ni mchapa kazi! hamna mtu anayeweza kupinga hilo.
Mpaka sasa sijajua msimamo wa chadema kwa nchi hii. Sijui wakiingia madarakani watafanya nini. Wana sera moja tu ya kupigana ufisadi, na hii imeshapitwa na wakati. Sera ya katiba mpya nayo tayari CCM imeshawapiga bao.
Kwani kama hujui jambo nilazima uandike ujinga wako hapa?Wafuate wakupatie sera zao badala ya kukisiakisia tu.
 
Kwa wale wanaoshangilia "ushindi" wa lowassa baada ya suala lake la kuvuliwa gamba pamoja na suala la Nape na chiligati anaowalalamikia kuzunguka nchi nzima "kumchafua" kutinga mikononi mwa kamati kuu,leo nataka kuwakumbusha kidogo kuhusu Jakaya ili huku mkifurahia "ushindi" pia mumfahamu sawa sawa muungwana jakaya ni mtu wa dizaini gani,sina lengo la kutia mchanga kwenye kitumbua chenu cha furaha la hasha ila nataka tukumbushane muijua siasa pia.Wandugu wapendwa mnajua ilikuwaje mpaka Lowassa akawa sio waziri mkuu.....

Kiufupi ni Kwamba Lowassa aliingizwa choo cha stendi na Jakaya!
Lowassa aliutema uwaziri mkuu anaoupenda mpaka leo kutokana na "utoto wa mjini" utapeli wa kisiasa wa Rais Kikwete kwa swahiba wake Lowassa, wala haikua "ajali ya kisiasa".

Mpango mzima ulikua hivi:

Bunge kupitia Kamati Teule ilisoma ripoti yake kupitia mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Hali ilikuwa tete Dodoma na hata Chamwino ambako Rais Kikwete alikuwa amejichimbia.
Baada ya kusomwa kwa ripoti, taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao.
Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani; – Lowassa akapendekeza eti jk aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, Jk baada ya "kupima" akastuka.
Ndipo yeye akaja na maarifa ya kimjini kwa kumwambia Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, halafu yeye jk aicheleweshe kuijibu hiyo barua kwa makusudi mpaka Bunge lihairishwe ili kumpa nafasi yeye jk kama rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Buge wa Aprili haujafanyika Dodoma.
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya "kuigiza" kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao. Usiku wa manane wa siku hiyo, Rais Kikwete aliamua kuwa barua ile ijibiwe na kukubaliwa. Ni kinyume na makubaliano yake ya awali na Lowassa!

Sasa leo tena suala la lowassa baada ya kupata kibali cha NEC liko mikononi mwa kamati kuu ambamo lowassa hayumo!Na watu wake eti wanashangilia "ushindi" wa ice cream iliyowekwa juani huku jakaya akiwa tayari amejeruhiwa na kutajwa kwenye sakata la richmond na pia ikikumbukwa Jakaya hana tena cha kupoteza kwa kuwa hawezi tena kuwa rais!mi nawaomba msiwe wajinga kama jamaa yenu kwa mujibu wa mwalimi nyerere ambae alifahamu ujinga wake zamani kabla kabla ya jk kuja kuthibitisha kwa kumuingiza choo cha stendi!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Story nzima ni uwongo mtupu...

EL lowassa alitakiwa kujiuzulu kwasababu ameharibu hali hewa na kujiingiza kwenye biashara wakati ni PM kwa kuleta richmond na kulazimishwa process ipate tender (japo haikuwa na sifa)

EL alipewa nafasi ya kuuzima uchafu (clean the mess) bungeni hasa kamati akashindwa pamoja na kwamba alikuwa PM angeweza kuwaona kina mwakyembe walimalize soo..kwa jinsi IQ yake ilivyo low akaamua kuzira..akitegemea msaada wa rais ..

Lakini JK akamwambia ( kama ambavyo anawaambia watendaje wote) if you can't clean the mess you made you quit..ndio story ya ukweli wamefanyiwa hivyo kina mattaka, kina mgonja, kina mramba and heavy weights..

Thats JK..I knew..hii story yako ni fake..bro..
 
Hivi kulikoni hasa,
mbona mme lo wa ha sa,
mmemwagiwa dawasa,
kila kukicha lowassa!!
 
siasa ni mchezo mchafu, hiki ni kipindi cha Lowasa kusafishwa upya na kwa kuwa tayari darili zinaonesha media zimesha elekea upande wake lazima atakuwa msafi tu tena msafi kweli.

Mie mpaka sekunde hii bado naamini kuwa CCM ikimsimamisha Lowas kama mgombea urais basi Dr.Slaa ataanguka vibaya sana tena sana. Na hakika litakuwa ni pigo kubwa kwa CDM.

Nashauri CCM waendelee na mchakato wa kutangaza kuwa dhana ya kujivua gamba ilikuwa ni ya kuumbuana na si kutoana chamani.
Tangu lini mtu akioga matope anakuwa msafi?
 
Tuongeee tu 7bu ni haki yetu..
Ila yote tisa, KUMI --- ukweli huu hapa

Lowassa he will be President, movie ishageuka, kawa kipenzi kikubwa, kichama, makanisani, na hata watu e binafsi... Juzi Dom, kamwaga sera na ukweli, sasa Nape & Chilli under fire, na Mwenyekiti Taifa CCM, kasema mwenye ushahidi kuwa EL ni fisadi alete, pili kasema Nape & Chilli watachukuliwa hatuwa za kinidhamu na kamati ya maadili ya CCM endapo watakutikana na makosa ya kumtukana na kumdhalilisha hadharani EL,
Niseme tu wazee wa CCM woooote now wapenzi wa EL ile mbaya, na jamaaa ndani ya chama hana mpinzani, na kawachana live Nape na Sita kuwa wakati yy & jk na viongozi wengine wanapigana kufa kupona chama kishinde 2010 election hao wenzao wako bize kuanzisha CCJ, Sita jashoooooo..... The guy is Brainy kamchana hadi JK....
Movie imegeuka 100%, EL atashinda Urais tena kwa kishindoo, mtashangaaaa, mm namsupport publicly, ni mchapa kazi, period....
 
Story nzima ni uwongo mtupu...

EL lowassa alitakiwa kujiuzulu kwasababu ameharibu hali hewa na kujiingiza kwenye biashara wakati ni PM kwa kuleta richmond na kulazimishwa process ipate tender (japo haikuwa na sifa)

EL alipewa nafasi ya kuuzima uchafu (clean the mess) bungeni hasa kamati akashindwa pamoja na kwamba alikuwa PM angeweza kuwaona kina mwakyembe walimalize soo..kwa jinsi IQ yake ilivyo low akaamua kuzira..akitegemea msaada wa rais ..

Lakini JK akamwambia ( kama ambavyo anawaambia watendaje wote) if you can't clean the mess you made you quit..ndio story ya ukweli wamefanyiwa hivyo kina mattaka, kina mgonja, kina mramba and heavy weights..

Thats JK..I knew..hii story yako ni fake..bro..

kama hii ni kweli ina maana na jk naye ajiuzulu kwa sababu alimzuia lowasa kufuta mkataba huohuo unaosema ndio ulisababisha lowasa ajiuzulu?

dah!
 
kama hii ni kweli ina maana na jk naye ajiuzulu kwa sababu alimzuia lowasa kufuta mkataba huohuo unaosema ndio ulisababisha lowasa ajiuzulu?

dah!

Oops..hayo maneno siyo ya kweli..aliambia tupate taarifa za wataalam wa wizara (Makatibu wakuu) kabla ya action..maana alishafanya makosa yeye EL ndio maana alitaka ku-pre-empty ..JK hakuzuia alitaka jambo ambalo lingekuwa na manufaa kwa taifa ambalo ni umeme kupatikana..

EL alitakiwa ku-handle tume ya mwakyembe lakini kwakuwa ana IQ ndogo akashindwa kitu ambacho kiongozi mwenye nafasi kama yake hawezi kushindwa nchi hii..alitegemea msaada wa rafiki yake lakini that is not how JK works..the style is "clean your own mess" period..

Ndio maana Ngeleja anabaki japo siyo mzuri anajua ku-deal na kamati au tume za bunge..hiyo ndio siasa ya Tanzania
 
Tuongeee tu 7bu ni haki yetu..
Ila yote tisa, KUMI --- ukweli huu hapa

Lowassa he will be President, movie ishageuka, kawa kipenzi kikubwa, kichama, makanisani, na hata watu e binafsi... Juzi Dom, kamwaga sera na ukweli, sasa Nape & Chilli under fire, na Mwenyekiti Taifa CCM, kasema mwenye ushahidi kuwa EL ni fisadi alete, pili kasema Nape & Chilli watachukuliwa hatuwa za kinidhamu na kamati ya maadili ya CCM endapo watakutikana na makosa ya kumtukana na kumdhalilisha hadharani EL,
Niseme tu wazee wa CCM woooote now wapenzi wa EL ile mbaya, na jamaaa ndani ya chama hana mpinzani, na kawachana live Nape na Sita kuwa wakati yy & jk na viongozi wengine wanapigana kufa kupona chama kishinde 2010 election hao wenzao wako bize kuanzisha CCJ, Sita jashoooooo..... The guy is Brainy kamchana hadi JK....
Movie imegeuka 100%, EL atashinda Urais tena kwa kishindoo, mtashangaaaa, mm namsupport publicly, ni mchapa kazi, period....

Too early to conclude mkuu..

Siku hata wiki inaweza kubadili upepo wa siasa mbaya kabisa..sembuse 3 yrs
 
helow,
ndugu EL
NAAKUPONGEZA kwa dhati enzi zako za uwazir.mkuu...........
nakumbuka, ndio kwanza mm nilikuwa naanza kazi......

nakupongeza kwa.mishahara kutoka kwa wakati...... ulitangaza tarehe 23 iwe umetoka, tena uliamuru wahasibu.walipa mishahara wafanye kazi hadi weekend iwapo tarehe inaangukia hyo tarehe


WAFANYAKAZI WA KIMA CHA CHINI TUNAZO KURA ZAKO 2015

Hadi sasa, cijaelewa sera za CDM kwa wafanyakazi......mnnn

Hongera kwa moyo wa ushabiki, mashaka yangu nipale utakapo tembea utupu bahati mbaya ukutane David Cameroon
 
Unajifanya unataka kutembea uchi ili kumuunga mkono Lowasa kumbe una ajenda zako za kutimiza masharti ya kupata misaada.
 
ivi Lowasa kaloga wa TZ?? mbona hakauki vinywani mwenu...
 
Hii story yako ni feki...

kwa mtu anayefuatilia na kuchambua siasa za JK atakuwa amegundua kuwa jamaa ni mpole sana, hamfuatilii mtu ila katika kula kula yako huko ulikopewa ikatokea umekunya basi safisha mwenyewe...yakikushinda basi utalala humo humo kwenye harufu ya mavi yako; hii ndiyo falsafa ya JK...

Kama sasa hivi naona JK ameamua kuwaacha wafu wazikane wenyewe; yeye ameishakula ameshiba na sasa ni kazi kwao wanaCCM kulilinda li chama lao. maana mtu mwenye akili timamu huwezi amini ni kwa nini anamlea lea mwizi kama Lowassa! Nadhani Chadema wajiandae kuchukua ncho 2015
 
Nimeifuma habari hii kule Mtanzania.Wanajamvi muisome ili mpate kujua kilichojiiri.


[h=1]Lowassa alipuka mbele ya kikwete[/h]Na Masyaga Matinyi, Dodoma



Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kimesema, Lowassa aliomba kupewa nafasi ya kuzungumza juzi, lakini Mwenyekiti Rais Kikwete hakumpa nafasi na kumtaka azungumze wakati wa mjadala wa hali ya siasa nchini jana.

Taarifa hizo, zimesema baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, kumaliza kuwasilisha mada kuhusu suala la maadili ndani ya chama, ndipo Lowassa alisimama na kuzungumza.

Pamoja na mambo mengine, katika mada yake, Msekwa alisema masuala yote yanayohusiana na maadili ndani ya chama yashughulikiwe na vikao husika kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
LOWASSA AZUNGUMZA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema; “Kwa kipindi cha miezi saba sasa tangu NEC ikutane, Katibu wa Itikadi na Uenezi na viongozi wengine wa chama wamekuwa wakizunguka nchi nzima kunitangaza mimi fisadi kwa kutumia rasilimali za chama.
“Leo hii napongeza ripoti ya mzee Msekwa ya kusisitiza kutumia vikao vya maadili kushughulikia na maswala yote yanayohusika na matendo ya kwenda kinyume na taratibu zetu za chama, lakini leo ninashangaa tunazungumzia kwenda kwenye utartibu huo, wakati mimi nilishaumizwa na ninatoka damu kwa kipindi cha miezi saba,”
“Lakini Mwenyekiti leo hii, natukanwa kwa ufisadi wa Richmond, wakati makosa yaliyosababisha kashfa ya Richmond yalitokana na makosa ya watendaji walio chini yangu. Mimi niliwajibika kwa ajili ya kulinda heshima ya chama chetu.
AMKUMBUSHA RAIS KIKWETE YALIYOJIRI

“Lakini Mwenyekiti, naamini utakumbuka jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba wa Richmond, nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi, lakini ukasikiliza ushauri wa kamati ya makatibu wakuu (Kikwete akatikisa kichwa kukubaliana naye) , mheshimiwa ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ndiyo uliopelekea mkataba usivunjwe.

“Pia naomba nikumbushe, nikiwa Waziri wa Maji niliwahi kutuhumiwa kuhusiana na kampuni ya City Water, tena nashukuru Mzee Nimrod Mkono yupo hapa, tukaenda kwenye kesi tukashinda. Sasa katika hili la Richmond kosa langu ni lipi? Je kuwajibika kwa maslahi ya chama changu na ya serikali yangu, utakumbuka ripoti ya Dk. Harrison Mwakyembe wakati anahitimisha Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, alisema kuna aina mbili ya uajibikaji, kwa makosa ya kiongozi mwenyewe na watendaji walioko chini ya kiongozi,

“Dk.Mwakyembe akasema Waziri Mkuu aliyejiuzulu amejiuzulu si kwa makosa yake, bali ni makosa ya watu waliokuwa chini yake (huku akiwa ameshikilia Hansard ya Bunge),”
“Mwenyekiti naomba nikukumbushe kuhusu kashfa zinazohusiana na ‘political perception’, kama si busara za kina Mzee Mkapa mwaka 1997 kule Zanzibar, leo hii usingekuwapo hapo ulipo na ulisema urais ni mipango ya Mungu.

“Unakumbuka kina Mzee Sozigwa jinsi walivyokuja na mafaili kwenye mkutano huo wa NEC kwa ajili ya kukumaliza.
“Hata nilipokutana na Mzee Msekwa pale Dar es Salaam, aliniambia kuna watu wananoa mapanga kwa ajili ya urais wa Lowassa.
“Kibaya zaidi, wanaonitukana ni wana-CCM (Nape, Chilligati na wenzao), lakini hata CHADEMA na wapinzani wengine hawanitukani,” alisema Lowassa.
Baada ya Lowassa kumaliza kuzungumza, Waziri Mkuu mstafuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, alisimama na kuchangia.
Katika mchango wake uliovuta hisia za wajumbe wengi, Sumaye alielekeza swali lake kwa Mwenyekiti, Rais Kikwete.
Katika Swali hilo, Sumaye alitaka kujua wanaotajwa kumtukana Lowassa kwa kipindi chote hicho watafanywa nini. Bila kuchelewa wa kusita, Rais Kikwete alisema; “Watachukuliwa hatua.”

Wajumbe wanyimwa fursa kuchangia:

Baada ya Sumaye kumaliza kuzungumza kulitokea hali ya kutoelewana, ambapo wajumbe wengi wa NEC walitaka kuchangia kutokana na yale aliyozungumza Lowassa.

Miongoni mwao ni mwanasiasa mkongwe na kada mwandamizi wa CCM, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye pamoja na kunyoosha mkono kiasi cha kutaka kusimama, lakini hakupewa nafasi ya kuzungumza.
Mjumbe mwingine wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, baada ya kuona uwezekano wa kuzungumza ni mdogo, aliamua kusema hadharani kuwa, katika kikao kijacho, waasisi wa CCJ wafukuzwe CCM.

Baada ya tafrani hiyo ya wajumbe kutaka kuzungumza na kunyimwa fursa, ndipo Rais Kikwete aliposimama na kusema; “Jamani sasa imetosha, tuachie hapa tulipofikia.
“Kama kuna mtu ana ushahidi kuhusu ufisadi wa Lowassa, basi aulete. Yamekwisha, tukafanye kazi, tujenge chama.”
Wajumbe kutoridhika:
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, nyuso za baadhi ya wajumbe zilionekana kujawa na huzuni na hali ya kutoridhika.
Baadhi yao walipozungumza na Mtanzania, walisema ilibidi hatua dhidi ya Nape na wenzake zichukuliwe leo (jana), ili suala hilo lifikie kikomo.

“Unajua hapa tumelaza kiporo, ilitakiwa hii leo kieleweke, watu tuondoke hapa kila kitu kikiwa kimemalizika, sasa mambo yamelala mpaka kikao kijacho. Lazima chama kisafishwe,” alisema mmoja wa wajumbe.
 
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ni CHENGE au alishaondolewa??

Chenge hajawahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, bali alikuwa mjumbe wa Kamati ya Maadili. Nafasi hiyo aliipoteza mara Wajumbe wa Kamati Kuu walipoombwa kujiuzulu na yeye hakurudi tena kwenye CC.

Kulingana na Katiba ya CCM, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ni Mwenyekiti wa CCM - Taifa.
 
Ama kweli! Kumwachia uchi mwanamme mwenzako maana yake nini?
 
Wote wanachezea akili za watanzania. Watanzania wa leo tumeshajua kete wanayojaribu kuicheza. Hapa watajifanya kuwa Lowassa kaonewa, na JK pekee ndiye ataonekana mwenye makosa. Wakishamsafisha Lowassa, wanafikiria kupitisha jina lake kugombea kupitia Magamba ili aje amlinde JK na upuuzi wao.
Kinachonishangaza ni pale Magamba wanapofikiri Tanzania ya leo ni ile ya mwaka 1954. Mnahangaika bure.
 
Back
Top Bottom