Lowassa ampinga Warioba serikali tatu

Lowassa ampinga Warioba serikali tatu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Waziri mkuuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowasa amesema hakubaliani na Jaji Warioba kuhusu uhalali wa serikali tatu kama rasimu ya pili ya katiba inavyopendekeza.

Lowasa amesema warioba ameficha baadhi ya taarifa kuhusu waliopinga serikali tatu walipotoa maoni yao.

Amelitaka kanisa liombee mchakato unaoendelea wa katiba mpya uyoe dira mpya ta Tanzania ijayo.

Ameyasena hayo Monduli katika kuukaribisha mwaka mpya 2014
 
Aache uchonganishi kwani yeye ameziona wapi kama zimeachwa, kwani yeye mjumbe wa tume.tulishasema machafuko yataletwa na Ccm.wapi msemaji wake bulembo tunawajua hao mungiki
 
Mwambieni hayo ni matakwa ya watanzania. Asilimia 61wametaka serikali 3 na hiyo haijaanza leo toka tume iliyoundwa mwaka 1984 matokeo yalikuwa kama ya leo. Hizo za akina lowasa na nape ni asilimia 25 kwahiyo nazo sio chache ila wameshindwa kwa hoja. Lowasa anahofia urais wake utakuwa sio dili sana kutakuwa na rais wa Tanganyika huru ambaye atakuwa na power kubwa.
 
Msamehe bure, Mzee huyu amepitwa na wakati. Mambo mengi kichwani kwani inawezekana amechanganyikiwa wapi agombee kati ya Tanganyika na Muungano, na hasa kwa vile hajafahamu wapi wataungwa mkono na mafisadi wenzake.
 
Hana lolote.... Ameshaona kwa jinsi Katiba itakavyokuwa uwezekano wa yeye kuwa Rais ni ndoto... Serikali tatu ndo mpango mzima tumechoka kufanywa mandondocha na CCM..
 
Mwambieni hayo ni matakwa ya
watanzania. Asilimia 61wametaka serikali 3 na hiyo haijaanza leo toka
tume iliyoundwa mwaka 1984 matokeo yalikuwa kama ya leo. Hizo za akina
lowasa na nape ni asilimia 25 kwahiyo nazo sio chache ila wameshindwa
kwa hoja. Lowasa anahofia urais wake utakuwa sio dili sana kutakuwa na
rais wa Tanganyika huru ambaye atakuwa na power kubwa.

Si agombee wa urais wa Tanganyika kama wa muungano siyo deal!
 
Aache uchonganishi kwani yeye ameziona wapi kama zimeachwa, kwani yeye mjumbe wa tume.tulishasema machafuko yataletwa na Ccm.wapi msemaji wake bulembo tunawajua hao mungiki
Mkuu sasa mchonganishi nani? Yeye lowassa au?
Msemaji wake ni Abubakar Liongo labda aje aseme waliona wapi hayo ambayo wanadai warioba hakuyasema. ITV wameonyesha katika habari yao juu ya haya aliyoyasema tena kayasemea kanisani kKKT monduli
 
Mwambieni hayo ni matakwa ya watanzania. Asilimia 61wametaka serikali 3 na hiyo haijaanza leo toka tume iliyoundwa mwaka 1984 matokeo yalikuwa kama ya leo. Hizo za akina lowasa na nape ni asilimia 25 kwahiyo nazo sio chache ila wameshindwa kwa hoja. Lowasa anahofia urais wake utakuwa sio dili sana kutakuwa na rais wa Tanganyika huru ambaye atakuwa na power kubwa.

Nakubaliana nawe. Tatizo lowasa yuko confused au agombee urais wa Tanganyika asiwe anaenda AU wala UN au agombee Muungano lakini asiwe na meno Bara. Yuko totally confused!
 
Hakubaliani na Warioba au watanzania. Nimuelewavyo mimi ni “watanzania hatukubaliani naye”
 
Huyu mzee anaota mchana kweupeeeee! Wapambe wake wanamdanganya sana.
 
hayo ni mawazo ya watanganyika cc znz hatumo yetu ni mkataba 66% ila tunasubiri bunge la katiba litaishaje then tuamue kwa kura ya maoni (hapana au ndio) hapo ndo mtajua kama waznz walitaka mkataba sio 3,4 wala 5
 
Waziri mkuuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowasa amesema hakubaliani na Jaji Warioba kuhusu uhalali wa serikali tatu kama rasimu ya pili ya katiba inavyopendekeza.

Lowasa amesema warioba ameficha baadhi ya taarifa kuhusu waliopinga serikali tatu walipotoa maoni yao.

Amelitaka kanisa liombee mchakato unaoendelea wa katiba mpya uyoe dira mpya ta Tanzania ijayo.

Ameyasena hayo Monduli katika kuukaribisha mwaka mpya 2014

mwambieni hatuhitaji Tanzania yenye muungano wa hovyo kama ulivyo...ni bora tuwe na Tanganyika kwanza kisha tuone ikiwa muungano na znz una mashiko.

Anaogopa nini....Besides he is an outdated corrupt bas.tard!!
 
Mevurugwa na Waroba huyooooo... Hajui agombee wapi; hajui wapi kwenye maslahi binafsi. Mgombea binafsi je? Si nasikia mzee mzima, nywele nyepe, ana jeshi la wapambe nchi nzima.
 
Huyu jamaa kweli ana matatizo. Huwa nina wasiwasi na uelewa wake. Aliwahi kusema serikali muundo wa serikali tatu unaweza kusababisha vita. Kivipi? Hakufafanua. Kinachomsumbua hapa ni kutojua wapi agombee kwa maana hapati picha ya ni kwa jinsi gani hela anayogawa atairudisha
 
anashindwa hata kusoma alama za nyakati?
 
Back
Top Bottom