Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Haya hilo la RICHMOND ni dogo?
Na nisifa kuwa na kashfa hata moja ya kuangamiza taifa ?
Kama uelewi watu kama hawa kunanchi zinachinja kichwa
huwezi ukacheza na maslahi ya wananchi kienyeji kienyeji
 
Haya hilo la RICHMOND ni dogo?
Na nisifa kuwa na kashfa hata moja ya kuangamiza taifa ?
Kama uelewi watu kama hawa kunanchi zinachinja kichwa
huwezi ukacheza na maslahi ya wananchi kienyeji kienyeji

Kuna ugonjwa unaitwa myopia na mtoa thread hii ameonyesha moja ya dalili za ugonjwa huo!
 
Tatizo liliopo ni kwanini Bw Lowassa hajashitakiwa mahakamani kwa tuhuma hizo zote? Mh Lowassa is not above the law.Na kama wameshindwa kumshtaki wanaogopa nini au hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka? Nani alaumiwe? Akisimama Lowassa akadai hizo ni siasa za maji taka yaani kuchafuliana majina kwani kila nikitaka kuwania Uraisi wabaya wangu wananipaka matope atakuwa amekosea? Bila kutumia nguzo ya mahakama na ikamweka hatiani Lowassa is still innocent na anayo haki ya kugombea the Highest Office of the Republic.
 
Mzee wa Watu kapumzika hana nia ya kuongembea uraisi......anakula kuku kwa mrija,
 
Huyo mtu hakuanza kuhusishwa na kashfa za ufisadi leo wala jana,... wewe kama unapenda sura yake nenda kanywe nae chai. ANA LAANA YA MWALIMU NYERERE, NO WONDER HIZI RECENT CAMPAIGNS ZA KUMDISCREDIT MWALIMU ZINA LENGO MAHSUSI LA KUMSAFISHIA NJIA HUYU MTU MAANA WANAJUA, LAANA YA MWALIMU NYERERE HAINA EXPIRY DATE. Tujikumbushe simulizi za watu(Mzee Kasori) waliokua wanamjua vizuri na ni wazalendo wa kweli wenye uchungu na Tanzania.

SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA (Sehemu ya makala yake)

Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, “ NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO” mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH). Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira. Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira “ ANGER ”. Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)“there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man’s life. The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees” Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa. Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema “si mkweli hata chembe moja”. Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo: “Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma”. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”. Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?. Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”. Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge. Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”. Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.
Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri. Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!! Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli? Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet! There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia. Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.

Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.
Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.
Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty. Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje? Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him. There is also a compelling case that is in Tanzania’s self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government. Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu? Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about. It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.
Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can’t, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages. Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded. These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu. The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi. Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.
BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- “ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.
Namalizia kwa kusema “Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI”. Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha. Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge.
Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.
Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.
Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.
Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji . viongozi wabovu wawajibishwe tu. Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kutu tetea leo kwa matatizo yote haya.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Africa.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
0754 372141


Mh.Umeandika kweli kweli!Je na wewe ulikuwa Unamshauri Vizuri mwalimu?Manake hata enzi ya Mwl siyo kwamba nchi ilikuwa ya Asali na Maziwa!
Hasa Swala Uchumi!umekuwa Ukidorora kadiri Umri wa Uhuru unavyoongezeka!
Si kwamba Mwl ndio 'Point of Ref' ya Kila Kitu?
 
We Ngamia,
Kwanza tuambie ni upi unafiki wa Kasori. Kaandika hapo facts, zisute. Lowassa hajachukua ranch ya taifa? Lowassa hajachukua majumba huko Arusha? Kwa nini Lowassa alikacha ule mkutano pale Msasani? Lowassa muongo, Lowassa mwizi, Lowassa hafai hata kuwa katibu kata katika serikali ya Tanzania. Hapo unafiki uko wapi? Unafiki ni ninyi ambao mnayaona madudu ya Lowassa lakini kwa sababu anawapa chochote au mnakula naye mnaona ni mtu anayefaa sana. Jibu hoja zake, siyo hii ya kuanza kuita mwingine kuwa mnafiki ili hali unafiki unajidhihirisha usoni mwako.

Jasusi,

Muongezee na nyumba anazomiliki afrika ya kusini mojawapo aliwahi kupangisha kwa balozi wa tanzania south africa. Baba wa taifa alipogundua kidogo azimie kwa mshtuko. Kote anakopita Lowassa amefanya uharibifu hafai hata kuwa class monitor wa darasa. Aendelee na ubunge wake Monduli akimaliza akapumzike tu.
 
Footprints nyingine za huyu Lowasa alipokua Waziri wa Maji na Mifugo hizi hapa... Dont say you were not warned! Kila alipopita alihusishwa na kashfa... amebakiza kuwauza watanzania wenyewe tu sasa, ndio maana ana haha kwa huo Urais!

SOURCE: TANZANIA DAIMA( LA ENZI ZILEEEE.....KABLA MHARIRI HAJAENDA KUKUTANA NA LOWASA KAMA INAVYOSOMEKA HAPA CHINI, Hahahaa...)

Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili hivi karibuni, zinaeleza kuwa, Lowassa alitumia nafasi yake ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, ya uwaziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo kununua eneo kubwa la Ranchi ya Taifa ya Mifugo ya Mzeri, iliyoko wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Zinaeleza kuwa Lowassa anamiliki kitalu namba 645/5, huku majina ya watu wanaoonekana kuwa wamiliki halali wakiwa ni wengine, jambo linalotia shaka.

Taarifa zinaeleza kuwa maelezo ya wamiliki wa kampuni hiyo yaliyoko kwa Msajili wa Makampuni (BRELA) na yaliyo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), yanaonyesha kuwa Kampuni ya Olospa, ndiyo mmiliki wa ranchi hiyo.

Baadhi ya viongozi wa NARCO waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, wakati ranchi hiyo ikiuzwa kwa Kampuni ya Olospa, kitalu namba 645/5, hawakujua kama ilikuwa na uhusiano wowote na Lowassa.

Kwamba baada ya kuanza kuibuka kwa tetesi kuwa ranchi hiyo ni mali ya Lowassa, walianza kuwa na wasiwasi kuwa inawezekana hakuweka wazi uhusiano aliokuwa nao na kampuni hiyo kutokana na wadhifa aliokuwa nao wakati huo.

"Ni kweli imebainika kuwa Lowassa anamiliki block namba 645/5, na amekuwa akionekana huko mara kwa mara, lakini sisi hatukujua lolote wakati wa zoezi la kumilikisha maeneo hayo," alisema Mshauri Mkuu wa NARCO, Fabian Shempemba, ambaye wakati wa uuzaji wa ranchi hizo alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo.

Alisema taratibu zilizokuwepo za kumilikisha ranchi ndogo za kibiashara kwa wafugaji wadogo, ziliipa madaraka ya kufanya maamuzi ya mwisho iliyokuwa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakati huo ikiwa chini ya Lowassa.

"Baada ya kukubaliwa na serikali mwaka 2002, kwamba ranchi za taifa zigawanywe vipande vidogo vidogo vya kibiashara na kumilikishwa Watanzania, NARCO tulipewa jukumu la kutangaza na kupokea maombi.

"Baadaye Bodi ya NARCO iliwasilisha mapendekezo yake wizarani kuhusu nani anafaa na nani hafai kumilikishwa ranchi hizo ndogo ndogo, halafu wizara ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuamua wamiliki," alisema Shempemba.

Shaka inayoelezwa hapa ni uwezekano wa Lowassa kuamua kununua ranchi hiyo kupitia Kampuni ya Olospa kwa sababu hakutaka kwa wadhifa aliokuwa nao kuhusika kwa namna yoyote na ununuzi wa ranchi.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua.

"Kwani kuna makosa yoyote mimi kununua hiyo ranchi? Sikiliza wee ……, wewe si ndiye uliyekwenda kwanza Wizara ya Mifugo kuhoji habari hizi wiki iliyopita?

"Sasa si vizuri kuzungumza haya mambo kwenye simu, nisubiri Dar es Salaam, nitarudi baada ya wiki moja, kwa sasa nipo safarini Monduli.

"Lakini njoo ukijua kuwa hiyo ilikuwa ni sera ya taifa ya kuzigawanya ranchi za taifa na mashamba makubwa ya mifugo ya umma, katika vipande vidogo vidogo na kuwamilikisha Watanzania wenye uwezo wa kufuga kisasa na kibiashara," alisema Lowassa.

Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kama alivyoahidi ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo na lilipompata kupitia simu yake ya kiganjaini alieleza kuwa atatoa ufafanuzi huo wiki ijayo.

"Nipo njiani narudi Dar es Salaam, nakuomba unipigie Jumatatu nitakuambia tukutane wapi ili tuongee kwa kina suala hilo, na ningependa uje na mhariri wako," alisema Lowassa.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa, Kampuni ya Olospa ilisajiliwa Julai 31, 1992, chini ya wakurugenzi wanawake watatu.

Taarifa zilizoko BRELA zinaonyesha kuwa wakurugenzi hao ni Ruth Mollel, Nengai King'ori Mollel na Olomutai Mollel.

Jina kamili la biashara la kampuni hiyo lililosajiliwa BRELA ni Olosipa Printers and Stationers Limited, ambayo ni kampuni inayofanya biashara za uchapishaji na uuzaji wa vifaa vya ofisini.

Shughuli za kampuni hiyo zinapingana na shughuli za biashara ya ranchi (kufuga na kuuza mazao ya mifugo), jambo ambalo linatia wingu zaidi la mashaka kuhusu kampuni hiyo kuuziwa ranchi hiyo.

Uamuzi wa kuzigawa ranchi za taifa katika vipande vidogo vya kibiashara na kuzimilikisha kwa Watanzania wazalendo, ulifikiwa na serikali mwaka 2002, na utekelezaji ulianzia kwa Ranchi ya Mkata (Morogoro), na kufuatiwa na ranchi ya Mzeri iliyogawanywa vipande 9, ambapo kipande kimoja (Block 645/5) ndicho kinachomilikiwa na Olosipa.
 
Huu ndio ujasiri anaouzungumzia mwl, UJASIRI WA KIFISADI. Lowassa hana limits, ni mtu hatari sana.
 
Nikiwa kama mtanzania ninaetafakari juu ya hali ya siasa tz, ninasimama ktk ukweli kusema zaidi ya Richmond hakuna ruhwa yenye mashiko ya kumuhukumu roho ya paka Lowasa!

Mwenye ushahidi wa ufisadi mwingine wa Lowasa auweke hapa! Kama si zaidi ya propaganda za wapinzani wake kisiasa!

Tatizo mnajiunga JF na mnaanza kutembe hapo hapo bila hata kutambaa, unataka mtu akuweke nini hapa tafuta taarifa wewe mwenyewe, acha uvivu wa kusoma kuna kila aina ya taarifa humu JF nyinye ambao kazi yenu ni kujadili mnachokiona na mnauliza hata mambo mliyoyakalia ndio mnaturudisha nyuma kama Taifa.

Haya mambo unayouliza umeyakalia humu JF watu wameyajadili miaka kadhaa iliyopita yapo humu bure ni kusoma tu! Uvivu tu, sijui hata kama unaweza kushika Jembe kama kusoma tu huwezi.
 
Kule kwemye Hifadhi ya wanyama pori ya Gombe, kuna kiongozi wa sokwe anayetawala sasa.Kiongozi huyu alimpindua aliyepita kwa kisingizio kuwa alikuwa dikteta. Hata hivyoi utaratibu wa sokwe hawa, mawindo yote ya sokwe raia ni lazima yapelekwe kwa huyu kiongozi,yeye ndio anao uamuzi ama wa kula mawindo yote, ama kugawa kwa raia wake na raia wapi awagawie!Huyu kiongozi wa sasa eti ni nafuu kuliko aliyemtangulia,na utaratibu huu hajaubadilisha, ukiwinda ni lazima mawindo upeleke kwake pia! Lakini eti ana unafuu kuliko aliyemtangulia! Hiyo ni Hifadhi ya Gombe.

Lowasa na wengine huko CCM wanafanana kitabia na hawa viongozi wa sokwe wa Gombe. Wote watachukua tu kwanza wao na watachagua wa kuwagawia mawindo kwa utaratibu usio shirikishi! Ila Lowasa anawazidi moja kubwa, anao ujasiri wa kutuongoza kuelekea kwenye mafanikio ya kiuchimi na kijamii kuliko wenzake wote ukiwaweka pamoja.Hiyo ni Tz

Dhambi kubwa aliyonayo EL ukiacha ya Richmond ni kuwa wenzake wanaifananisha safari ya Zuma kuelekea Urais wa Afrika Kusini-na safari yake: atashinda!
 
Ukitumwa siku zote tafakari kwa kina juu yaujumbe uliopewa ukiona hauna mashiko kwa future ya Taifa nibora ukae kimya.jf siyo yamatusi Bali niukweli Daima
 
Huyo mtu hakuanza kuhusishwa na kashfa za ufisadi leo wala jana,... wewe kama unapenda sura yake nenda kanywe nae chai.

ANA LAANA YA MWALIMU NYERERE, NO WONDER HIZI RECENT CAMPAIGNS ZA KUMDISCREDIT MWALIMU ZINA LENGO MAHSUSI LA KUMSAFISHIA NJIA HUYU MTU MAANA WANAJUA, LAANA YA MWALIMU NYERERE HAINA EXPIRY DATE. Tujikumbushe simulizi za watu(Mzee Kasori) waliokua wanamjua vizuri na ni wazalendo wa kweli wenye uchungu na Tanzania.

SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA (Sehemu ya makala yake)

Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, “ NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO” mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH).

Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira.

Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira “ ANGER ”. Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)“there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man’s life.

The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees” Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa.

Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema “si mkweli hata chembe moja”.

Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je?

Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo:

“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma”. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.

Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.



Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli).
Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”

Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.

Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!

Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?

Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!

There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.

Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.

Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.

Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.

Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.

Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?

Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo?
Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.

There is also a compelling case that is in Tanzania’s self interest.
Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.

Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?

Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.

It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can’t, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.

Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded.

These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu.

The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi.

Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.

BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- “ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.

Namalizia kwa kusema “Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI”. Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha.

Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge.
Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.

Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.

Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete.

Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.
Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji .

Viongozi wabovu wawajibishwe tu.

Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kutu tetea leo kwa matatizo yote haya.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Africa.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
0754 372141


capt lowasa tafadhali uone aibu,achana na urais huna sifa na una kashfa nyingi
 
Nikiwa kama mtanzania ninaetafakari juu ya hali ya siasa tz, ninasimama ktk ukweli kusema zaidi ya Richmond hakuna ruhwa yenye mashiko ya kumuhukumu roho ya paka Lowasa!

Mwenye ushahidi wa ufisadi mwingine wa Lowasa auweke hapa! Kama si zaidi ya propaganda za wapinzani wake kisiasa!

Hebu chukua mfano wa mchezo wa mpira wa miguu. Mchezaji anapofanya madhambi uwanjani mwamuzi anaweza kumpa onyo kwa kadi ya njano, lakini kama mchezaji huyo atafanya madhambi mengine anaweza kupewa kadi nyingine ya njano ikiufatiwa na kadi nyekundu hivyo kwenda nje ya uwanja. Hata hivyo endapo yale madhambi ni mabaya mno mchezaji anaweza kupewa kadi nyekundu moja kwa moaja na kwenda nje ya uwanja. Hii scenario ya pili ndiyo hiyo inamhusu EL.
 
Mvua za Kutengeneza Kutoka bara la Asia zikajaze Mtera maji! muhahahahahahaha
 
Nikiwa kama mtanzania ninaetafakari juu ya hali ya siasa tz, ninasimama ktk ukweli kusema zaidi ya Richmond hakuna ruhwa yenye mashiko ya kumuhukumu roho ya paka Lowasa!

Mwenye ushahidi wa ufisadi mwingine wa Lowasa auweke hapa! Kama si zaidi ya propaganda za wapinzani wake kisiasa!

Yaelekea uko nyuma ya matukio au unafanya makusudi,ninakushauri kwamba pitia historia yake yote alikowahi kufanya kazi kisha nenda kafanye uchunguzi utamgundua huyu ni nani na amefisadi nini na utashangaa na roho yako,kwaujumla jamaa ni mchapakazi sana tena sana tatizo lake mali zilizombele yake haziachi hata ufanyeje, nenda AICC,Wizara zote alizofanyia kazi mpaka anajiuzuru utapata taarifa zaidi ya tani mia hivi.ukianza na wizara ya Ardhi ni vizuri zaidi.
 
We Ngamia,
Kwanza tuambie ni upi unafiki wa Kasori. Kaandika hapo facts, zisute. Lowassa hajachukua ranch ya taifa? Lowassa hajachukua majumba huko Arusha? Kwa nini Lowassa alikacha ule mkutano pale Msasani? Lowassa muongo, Lowassa mwizi, Lowassa hafai hata kuwa katibu kata katika serikali ya Tanzania. Hapo unafiki uko wapi? Unafiki ni ninyi ambao mnayaona madudu ya Lowassa lakini kwa sababu anawapa chochote au mnakula naye mnaona ni mtu anayefaa sana. Jibu hoja zake, siyo hii ya kuanza kuita mwingine kuwa mnafiki ili hali unafiki unajidhihirisha usoni mwako.


Ni kweli Tanzania kuna siasa za unafiki, kuna wanafiki wengi na uzushi mwingi. Lakini kwa mtu mwenye akili timamu, Lowassa hata kuwa Waziri Mkuu lilikuwa tatizo, si dogo kubwa. Mfano tunao, tena wazi kabisa tuliona ufisadi katika u-PM wake,tunajua kabisa kuwa akiwa PM tena nini kitafanyika, leave alone urais, ambao akiupata atafanya "makubwa zaidi". Barua ya Mzee Samuel Kasori hapa JF si mara ya kwanza kuonekana, na yaliyosemwa yote hayajawahi kukanushwa, even worse baada ya kuwa PM alifanya zaidi ya yale yaliyomo kwenye barua. Tutakuwa wapumbavu sana kama tunafikiiri EL atatufaa, tunatakiwa kufikiri kwenda mbele, sio style hii ya reverse.
Bonga
 
lowasa mwacheni jamaani awe raisi wetu tuondokane na viongoz maneno tunataka watendaji
 
lowasa mwacheni jamaani awe raisi wetu tuondokane na viongoz maneno tunataka watendaji
 
lowasa mwacheni jamaani awe raisi wetu tuondokane na viongoz maneno tunataka watendaji
 
Back
Top Bottom