Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Hutaki kujua fizikia ya unajimu kujua Lowassa siyo Richmond peke yake...hizi hela zimetoka wapi? mfanyakazi wa serikali toka 1989 hadi 1995 tayari milionea (in dollar terms) haingii akilini...hamna mtanzania wa kizazi cha pili (waliozaliwa miaka michache kabla ya uhuru kama akina Lowassa) ambaye anaweza kusema aliachiwa utajiri mkubwa na baba yake..hamna.

ushaidi wa moja kwa moja sina, lakini hii haiwezi kunizuia na kuwazuia watz wengine kumjaji mh Lowassa kama ni mwizi..kumbuka maoni ya jamii hayahitaji ushaidi wa kimahakama na katika siasa haya yanajenga au kuaribu kabisa taswira ya mwanasiasa......wizara ya ardhi lowassa alijitajirisha binafsi kwa deal za viwanja na nyumba za NHC na alimweka rafiki yake Masebu kuwezesha haya....wizara ya mifugo tunajua kuhusu kujimilikisha ranch ya serikali kule Handeni...jengo la umoja vijana je wakati akiwa mlezi wa uVCCM? TRC ilipouzwa mkurugenzi wa PSRC aliwekwa na Lowassa kuhakikisha mgao unaenda vizuri...wengine wataongeza madudu mengine

Mkuu, Nadhani mleta thread amepata majibu mazuri.
 
Hivi kwa nini lowasa analazimisha kuwa rais wakati huo watz wote wanajua uchafu alioufanya kuna kitu jamaa ambacho anakitaka si hivihivi kama ni fedha anazo.
 
Lowasa ni mtu safi! Madhambi mengine aliyonayo ni ya kibinadamu kama mimi na wewe!
 
Wewe uliye na kampeni ya kumchafua unawazidi kitu gani.

Duh! Kweli mkuki kwa nguruwe...TUAMBIZANE UKWELI 2015 MTU WA KUWA RAIS NI EL.SI KWAMBA NINAMPIGIA DEBE BALI ANASTAHILI.KWASASA TUNAHITAJI RAIS KAMA EL.
 
ushahidi unaonyesha kwamba mbali na kisore kikao ambacho mwalimu Nyerere alimuuliza Lowassa maswali mengi ikiwa ni pamoja na alipata wapi fedha au utajiri wa harakaharaka kilifanyika mtaa wa Laibon - osterbay katika nyumba aliyokuwa anaishi mama khadija ambaye ni mke wa Rais wa awamu ya pili, Alhaji Ally hassan mwinyi. Na waliohudhuria katika kikao hicho walikuwa ni pamoja na malecela, kawawa, kikwete, Anne makinda na wengine wengi
 
Kasori amezungumza na Nyerere. Amezungumza kwa simu na Kawawa. Amezungumza na Lowassa mwenyewe. Huyo kwako bado huoni kuwa ni chanzo kinachoaminika? Naungana na Sober. Wabongo bana....

Kasori au Kasoro aache longolongo zake kwenye ukumbi huu.

Mbona hajakilaumu Chama Chake Cha Magamba-CCM kwa KUKIUKA MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA LILIASISIWA NA HUYO BABA WA Taifa? Hivi Kasori haoni kwamba baada ya CCM kuachana na Azimio la Arusha(UJAMAA NA KUJITEGEMEA),CCM waliamua KUKUMBATIA AZIMIO LA ZANZIBAR ambalo ndicho CHANZO CHA KUKUMBATIA UFISADI NDANI YA CCM?????Kasoro kweli halioni hili??? Kama CCM waliamua kuwatukuza MAFISADI/MATAJIRI ambao ndiyo wanakilea na kukiendesha chama chao akiwemo Lowassa,Rostam Aziz na Chenge anapiga makelele ya nini????

Kila Mm-bongo anajua kuwa Rostam Aziz alikuwa ni MWEKA HAZINA WA CCM na ni rafiki wa Kikwete kama alivyo Lowassa. Kwa hiyo kumng'ang'ania Lowassa na wenzake kuwa ndiyo mafisadi ndani ya CCM siyo kweli. CCM WOTE NI MAFISADI KUANZIA KWA KINA MKAPA NA KIWETE MWENYEWE na ndiyo maana SERA YA KUJIVUA GAMBA IMESHINDIKANA!!!!!

Kwa sasa hakuna mwenye ujasiri wa kumwambia mwenzake kujivua gamba MAANA WOTE NI MAGAMBA. Kasoro atakuwa amesikia hoja za LOWASA juzi kwenye CC pale alipomvaa Mwenyekiti na Rais wake Kiwete kwa kumwambia hivi,"NIKUKUMBUSHE MHE. RAIS na M/KITI wa chama kwamba MIMI NILITAKA KUVUNJA MKATABA WA RICHMOND NIKAKUPIGIA SIMU UKIWA SAFARINI ULAYA WEWE(Kiwete) UKANIAMBIA TUSUBIRI KWANZA MAANA ULIKUWA UMEPATA USHAURI WA MAKATIBU WAKUU KUHUSU RICHMOND, SASA IWEJE LEO MIMI NATUKANWA NA WANA CCM WENZANGU(Nnape na Chiligati) TENA KWA KUTUMIA HELA YA CHAMA??? KIWETE KIMYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!

Nasikia mkutano wote ulikuwa kimya kiasi ambacho ungeliangusha sindano ingelisikika. Maana Lowassa alikuwa ameamua kutema NYONGO na SUMU yake mbele ya Kiwete,mbele ya Mkapa na Mwinyi!!
 
Kwa ujumla walichokifanya akina Nape dhidi ya Lowasa ni makosa ya kimkakati ambayo sasa yanaigharimu NEC kufanya maamuzi dhidi yake.

Kingine CCM itambue kuwa huyu Bwana amejishikiza sana na kanisa hususan Lutheran na ana sapoti kubwa ya waumini wa kanisa kutokana na michango yake kwenye harambee..

Binafsi sina tatizo na Lowassa as long as siamini kuwa Lowasa anaweza kuwa mchafu na Swaiba wake akabaki msafi, manake dili nyingi walicheza pamoja.. Isitoshe huyu Bwana alikuwa Mchapakazi kulinganisha na waliobakia madarakani..!

uwa nashindwa kuelewa huu UCHAPA KAZI wa Lowassa ni nini haswa...haka kapropaganda kalipenyezwa na mijitu imekanunua kweli kweli
 
Tatizo liliopo ni kwanini Bw Lowassa hajashitakiwa mahakamani kwa tuhuma hizo zote? Mh Lowassa is not above the law.Na kama wameshindwa kumshtaki wanaogopa nini au hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka? Nani alaumiwe? Akisimama Lowassa akadai hizo ni siasa za maji taka yaani kuchafuliana majina kwani kila nikitaka kuwania Uraisi wabaya wangu wananipaka matope atakuwa amekosea? Bila kutumia nguzo ya mahakama na ikamweka hatiani Lowassa is still innocent na anayo haki ya kugombea the Highest Office of the Republic.
Karamagi hajashitakiwa Mahakamani Lakini ameondoka!!!!, Rostam Aziz Hajashitakiwa Mahakamani lakini ameondoka!!!!
Hata kikwete naye hajashitakiwa Mahakamani Lakini wapo wanaotaka aachie ngazi Uenyekiti Hujaona bado??
Ndani ya CCM mahakama ni yao!!!, Gereza ni Lao!!! Na hata Polisi ni Yao!!! sasa wewe unasubiri Waende Mahakamani ili watumie pesa za kodi yetu tena??
Wewe huoni mizengwe ya Kesi ya Prof. Mahalu??
Huoni kesi za EPA??
Mbona hujawaza Waza suala la kagoda???
Huja ona Kesi ya Dowans ?? Hapo Mwizi ametushitaki harafu kashinda???
Huko nyuma watalawa Wetu hawakuzingatia madili wamesituka sasa hivi baada ya kuanza kubali katiba itakayo weka vifungu vya kuwapeleka jela!!!
We angalia mazungumuzo na Chadema yamechukua siku mbili kinyume na taratibu za Ikulu, unafikiri kuna nini!!!
 
uwa nashindwa kuelewa huu UCHAPA KAZI wa Lowassa ni nini haswa...haka kapropaganda kalipenyezwa na mijitu imekanunua kweli kweli

Hapa sizungumzi kiushabiki,kiukweli EL ni mchapa kazi. Hiyo mara nyingi ni asili ya kabila la MAASAI hasa tukikumbuka namna Marehemu Sokoine alivyokuwa akichapa kazi enzi zake.

Lowassa huwezi kumlinganisha na Waziri Mkuu wa sasa anayejiita mtoto wa Mkulima Mhe.Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye amedhihirisha ni mojawapo ya Mawaziri Wakuu wababaishaji na wavivu wa kufikiri. Fikiria Waziri Mkuu anayeamua KULIA MBELE YA WANANCHI eti kisa ALBINO WANAULIWA BILA SABABU!!!Ajabu kweli kweli,yaani zee zima linatoa mchozi mbele ya wananchi,sasa unategemea wao wafanyeje???Chukua maamuzi magumu ya kukomesha mauaji ya mazeruzeru na siyo kututolea mchozi!!! Ndiyo maana kwa sasa Serikali iliyoko madarakani inayoongozwa na Pinda ni legelege sana kuanzia BUNGENI mpaka MITAANI. Mawaziri wote wa CCM ni legelege maana kiranja wao mkuu Bungeni ni legelege!

Nimalize kwa kutoa mifano michache ya utendaji wa EL kuonyesha uchapakazi wake. Kwanza kabisa EL aliweza kuvunja MKATABA WA Kampuni ya CITY WATER. Juzi kwenye mkutano wa CC tumesikia EL akimwambia Kiwete kuwa alikuwa tayari kuvunja MKATABA WA RICHMOND LAKINI BOSI WAKE KIWETE AKWAMWAMBIA asubiri maana alikuwa amepokea ushauri wa Makatibu wakuu wa Wizara husika. EL angeliweza kuvunjilia mbali huo mkataba maana ana uzoefu!Sasa hapa wa kulaumiwa ni nani kama siyo KIWETE??

Shule zote za KATA ni BRAIN ya EL ingawa shule zenyewe hazina Waalimu,Madarasa na Vitabu lakini lilikuwa wazo makini kama lingepewa uzito unaostahili.
 
Mlioomba facts nyingine kuhusu EL mmezipata toka kwa Mzee Kasori. Ombeni nyingine, nadhani kwa vile JF ni mahali pa kuongea bila woga hembu tuleteeni mengine hapa.. najua watu wanayo. Huko Ardhi vipi mbona mpo Kimya? vipi vita yake na aliyekuwa Katibu Mkuu? Mhaya mmoja hivi, nimemsahau jina.
 
Kifupi huyu jamaa hana kosa la kimsingi kumlinganisha na Karamagi,Msabah, mfano wa Ballali,Chenge,Kigoda, Mramba,Iddi Simba na wengine kama hao. Yeye EL hana tuhuma ya moja kwa moja. Nimefuatilia posts na threads mbalimbali kumhusu, sijaona tuhuma ya moja kwa moja.... Kama tatizo ni utajiri,hata udiwani haupatikani bila kuwa na hela..! Na sidhani kama rafiki yake ambaye hawakukutana barabarani,nahisi hatamwangusha mbele ya jamii kwa mara ya pili!
 
Mlioomba facts nyingine kuhusu EL mmezipata toka kwa Mzee Kasori. Ombeni nyingine, nadhani kwa vile JF ni mahali pa kuongea bila woga hembu tuleteeni mengine hapa.. najua watu wanayo. Huko Ardhi vipi mbona mpo Kimya? vipi vita yake na aliyekuwa Katibu Mkuu? Mhaya mmoja hivi, nimemsahau jina.

Huyo mhaya anaitwa Lutabanzibwa!
 
Kasori Kasori Kasori!. Hivi kila kilichosemwa na Nyerere ni Maneno matakatifu? Kama alimzuia EL kugombea urais kwa sababu alikuwa amejilimbikizia mali nyingi tangu ajiunge na CCM kuliko yeye Nyerere aliyoweza kuipata, kwa nini asimfikishe mahakamani wakati anaiba badala yake anamngoja mpaka agombee uraisi? Hivi ukiwa CCM unaruhusiwa kuiba utakavyo ilimradi tu hugombei uraisi? Je hii haitoshi kuonyesha kwamba Nyerere naye alikuwa anakumbatia mafisadi ili mradi wasigombee uraisi mpaka pale atakapotaka yeye wagombee uraisi? Je hamuoni kwamba kuwashambulia maraisi na viongozi waliorithi utawala wa Nyerere na kudai kwamba angekuwepo Nyerere haya yasingetokea mnawaonea? Watanzania kama tunataka nchi yetu iendelee mbele basi tuyachambue mambo yetu kwa kuangalia mambo ya nyuma ambayo ni mazuri na kuacha yale ambayo ni mabaya. Lakini maamuzi yetu mengi yatategemea mambo yanayotokea kwenye kipindi chetu. Tukumbuke kwamba Nyerere aliachia ngazi wakati mikakati yake ya maendeleo ya nchi yetu ya Ujamaa (Utopia) ilikuwa haitekelezeki. Akaona kuendelea na mfumo ule haiwezekani labda kama uwe na kichwa cha mwendawazimu.
Simaanishi EL ni msafi. Maelezo tunayoyatarajia kutoka CCM na serikalini ni kujibu mapigo ya EL ili tuweze kuona ukweli wa suala hili la Richmond uko wapi. JK alishawahi kuwaambia wabunge wake warudi majimboni mwao kujibu mapigo ya wapinzani kwani uwongo ukirudiwa mara nying unaonekana kuwa mkweli. Hapa EL kamshambulia JK na wa kujibu mapigo ni JK au serikali yake au Chama chake. Sio wastaafu wa kipindi cha Nyerere!
 
Mh,, lowasa kweli anaonyesha wazi ana nia ya kuliongoza taifa la tanzania katika kipindi kijacho,, ana haki ya kufanya hivyo kama mtanzania, inaoneka kuna mambo anaona akiwa rais wa nchi anaweza kuifanyia tanzania na kuifikisha mbele ktk maendeleo yake, hvy tusimnyime hy haki na kama ana kasoro na ushahidi upo itajidhihirisha2.
 
Watanzania wengi sasa tumepigwa na changa la macho kiasi cha kutokuona mema na mabaya.

Labda kwa hapa maana na mimi baada ya Shoka la mwakiembe Kimkata Lowassa Sasa imekuwa kila kona Lowassa Lowassa..

Sasa hili la lowassa ni kosa na najua hakuwa peke yake,, sasa hivi kweli ndiyo kunuka mpaka kila kona yeye tuu mbaya??

mimi nadhani kuna kivuli fulani kilikuwa naye na pia alikuwa ni mtu mwenye maamuzi magumu wakati mwingine na nadhani viongozi wa sasa waliiga kwake kwenye mikutano wananchi kupewa mic na kuhoji live,,

Sasa kama toba ipo hatokuwa safi tena?? na kweli tuzidi kumlaani mpaka mwisho wa maisha yake??

Nimeuliza nikiomba tuchangie kahoja....
 
1.Kukubali cheo cha uwaziri mkuu 2005 cheo ambacho alikuwa amehadiwa Samwel Sitta na hivyo kumfanya kuwa adui wa SITTA
2.kumheshim mno bosi wake (JK ) NA KUOGOPA KUMWEKA HADHARANI JUU YA UMILIKI WAKE (JK ) wa Richmond kwa kipindi kile na akakubali kujiuzili ili kumfichia aibu.
 
mbona hueleweki unachotaka kutuambia au ndo unaingiza siku?
 
Back
Top Bottom