Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Anatapatapa hajui hata la kufanya. Ukiangalia kwa makini..Tanzania imekosa kiongozi anaweza akaongea jambo la msingi likaeleweka na kusikilizwa barabaraa bila mawaa
 
Atakuwa anafanya timing mbaya.Naona hajatosheka na yaliyompata hadi kujiuzulu.Na bado hataki kuweka rekodi sawa.Kuna timing anatakiwa kuwa nayo kati ya uchaguzi,kujivua gamba,na kuweka rekodi ya Richmond straight.Thats the path he has to go if he wants to remain in politics.
 
Mimi nimechukia sana nilitegemea angeongea ukweli kumbe amekuja kubip?
Sasa kwa taarifa yake huu moto aliouwasha hawezi kuuzima.alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya kukurupuka kwake sasa yatamtokea puani.
Kwa nini aitishe mkutano na waandishi wa habari ama hajajiandaa? Kwa nini anatisha watu?hafai kuwa rais.
 
Vijana, vijana, vijana.....
Kila mwanasiasa aka kawimbo.
Bungeni kwenye kauli yake ya "maamuzi magumu" alisema hii kauli ya vijana bra brah...
Wakati serikali yake inagawa malaki ya hekari kwaajili ya kuwekezwa!
Vijana, hizi kauli za kututega.... Ni lazima tuingie kwenye mapambano ya fikra badala ya kubebwa na kauli za wanasiasa ambao wakimaliza kuhutubia wanaenda kujipongeza kuwa "Vijana ukitaka kuwapatia jifanye unajua matatizo yao"
 
punguza hasira! tafadhali rudi jamvini.
 
Huyu jamaa huwa anaasili ya kuchinja akiwa pale jimboni kwake je amechinja jamani nije kula nyama?
 
Kwa level ya Lowassa hakupaswa kabisa kuitisha press conference ya kuongelea vitu vidogo kama hivyo, nadhani leo atakuwa amewanyong'onyeza sana wapenzi wake na kuwapa kicheko adui zake...
KWELI MKUU sijui Mwanakijiji anasemaje leo
 
hakuna jipya mkuu invisible funga thread tusijaze memory ya server bure maana ametia hasira watu wengi sana. Totally disappointment .........................mweeeeeeeeh
 
lowassa itakuwa katishwa na IKULU haiwezekani aongelee udaku na urojo wakati nondo za maana zipo
 
Hapa ndipo Lowassa anaponishangaza siku zote...watu wanadai hawampendi but they are still talking about him more than they talk about other politicians!!I think he's the next presidential candidate kwa upande wa CCM...
 
lowassa itakuwa katishwa na IKULU haiwezekani aongelee udaku na urojo wakati nondo za maana zipo

Hana cha kuongea yule maana dhambi imemjaa mpaka moyoni....lowassa ni wimbo uliochusha na hata ufanye remix hauwezi noga tena...
 
Thread ifungwe tu kwasababu haina mvuto. Tunajadili mambo yaleyale tuuuuu
 

Kama haya ndiyo aliyoongea, ni wazi amekiri udhaifu wake, na najiuliza amewezaje kuwepo serikalini kwa miaka yake yote hii kwa akili hii?
Amepigilia msumari wa mwisho kwenye ndoto zake, and I am standing to be corrected, he is finished for good! Da hata elements kidogo niliyokuwa nayo katika kumhurumia, nimepoteza....he is a rubish, period.
Wenzake hawaogopi kuongea hata kama umetishwa. Yaani hata Millya anaonekana jasiri kuliko yeye, japo katumwa. Kina Sitta pamoja na kuwa serikalini wanaubavu wa kuongea. Yeye anaogopa nini? Au kwa vile the whole vicious circle ina mwelemea yeye!
GONE, GONE GONE! Kweli TB Joshua kamroga badala ya kumzindika, na alimpa "ujasiri" wa Panya kuvaa ngozi ya chui ili kumtisha Paka, kumbe panya ni panya tu!
Shit!
 
Natoa TAMKO:Ni uzembe mpaka leo JF haina live audio flaws. kitu gani kigumu.. tuambie tuchangie.. habari hii tungeipata live humu jamvini.. Mods ongezeni kufikiri bwana!!

Tamko zuri sana lakini pia shangaa tuliambiwa kuna redio maarufu zingeweka live lakini ujue mamia ya Watanzania wamepata taarifa hizi kwa mara ya kwanza kupitia humu JF na wachache kupitia FM radio ya Arusha. Ni jitihada binafsi za Invisible na timu yake kupata kilichopatikana humu. Tuendelee kutoa ushauri siki zijazo yatakuwa mema zaidi
 
hakuna jipya mkuu invisible funga thread tusijaze memory ya server bure maana ametia hasira watu wengi sana. Totally disappointment .........................mweeeeeeeeh
Kosa kubwa sana kufanya mtu kama Lowasa! Amevuruga ujasiri aliotaka kuuvaa na hachomoki tena! Ukiwa vitani lazima uje Mbaya mbaya!
 

Ushauri sawa ila tuende mbele zaidi ili tufanikishe yale tunayopenda kuyaona badala ya kuwaachia wengine watufanyie...Na ikitokea tatizo kidogo tunajitokeza kusaka medali za kulaumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…