Naunga mkono aliyoyaongea na style yake presentation maana mkutano au press cenference ameitisha yeye. Kama aliyosema siyo yale tuliotaka kusikia hatna haja ya kuyajadili na message will be sent to him.Lakini kama audience constituting waandihi wa habari na wengine walimsikiliza na kuuliza maswali na kusikia ambayo hawakurataji walikuwa na options kadhaa. Wangeondoka immediately after he had stated his position that questions be in the context of what he had presented. Basi angegoma zaidi wangenyanyuka na kuondoka kabisa huku wakimwacha ameduwaa. Pili Watanzania lazima tuwe serious na yale tunayotaka kusikia na kutoka kwa nani.
Haingii akilini kwamba mtanzania sensible alitaka EL afanye kama Wakatholiki ndani ya confession box kuwa nilikosa eno kadha wa kadha. EL kama ilivyo JK are both birds of the same feather na historia itakuja kusema.Tusiwe wasaarifu. Waliposhika madaraka kila zuri mfano amani na utulivu, mshikmano, hazina ya fedha za kigeni $3b, miundo mbinu ya barabara, uwanja mpya wa taifa, viwanda vichache vilivyobinafsishwa na kuendelea kuzalisha walivifanya kama ni mafanikio yao wala si ya chama au serikali zilizopita. Ilikwa ni nadra Mkapa na Nyerere kutajwa kwenye mazuri hayo labda Mzee Mwinyi peke. Kumbuka mpaka Mkapa alianza kuzomewa na watu kama ambaye hakuwahi kufanya jema lolote.
Lakini penye matatizo kama ukame, njaa, ukosefu wa umeme, mikataba mibovu ya madini, radar ya ndege na mengine hayo yalifanywa kuwa ni urithi mbaya wa wa serikali zilizopita. Sasa mtu ambaye alizoea propaganda za namna hii mnamtaka leo asimame ajipige kifua aseme nilikosa. Watu wa kukubali makosa na kusema yalifanywa kwa ubinadamu na kutoa wito wa kujirekebisha walikuwa ni kina Kambarage, Kaduma, Warioba na wengine lakini bahati mbaya Mwalimu ashatangulia mbele ya haki na waliokuwa hai badohawako ktk vyombo vya kimaamuzi.
Majibu sahii ya nini kijiri Richmond/Dowans na sasa Syombion anayo JK kama Rais maana anavyo vyombo vya kumsaidia kujua japo ashasema hajui. Polisi, usalama wa taifa, jeshi, PCCB, Tume ya maadili na ofisi ya rais.Sasa kuendelea kujificha chini ya kivuli cha siwajui ni kujidhalilisha na kuwatusi watanzania. Richmond/Dowans wamekuwa wakilipwa bilions of shs, sasa were we paying the ghosts? JK atuambie kuhusu haya na EL ambaye yuko nje ya vyombo vya maamuzi na kwa kuwa kuna vyombo vingi chini yake Rais jibu litakalotoka hapo tutajua pumba zipi na mchele upi. Lakini itoshe kusema yeye ndiye aliyebariki mitambo ya dowans wapewe symbion na kuzalisha umeme.sasa jiulize utaruhusu kitu cha mtu usiyemjua anunue mtu mwingine? kama ni hivyo hamna maana ya kuwa na mtu kama huyu as rais na vyombo hivi vikienedelea kuripoti kwa wahusika wanahitaji kupimwa.
Majibu mengine ya Richmond/Dowans anayo Sitta Samweli aliyekwa spika wakati huo. Alianzisha mchakato wa kuipeleleza richmond/dowans na ripoti kutolewa na jinsi alivyozima mjadala huo ni ishara ya kifisadi. Huwezi kuanzisha jambo leneye gharama in terms of perdiem kwa wajumbe na na nauli ya kwenda na kurudi nje ya nchi na muda mwingi wa bunge kuongelea swala hilo halafu ukalizima bila majibu na utarajie watu wakuenzi hapana. Ssita asipojitokeza waziwazi na kusema tutasema aliutaka uwaziri mkuu wa EL.Haitoshi kusema wasilipwe, ni wahuni, ni mkataba batili... Hayo kila mtanzania mwenye akili alishajua.Tuanataka atwambie sababu ya kuzima mjadala bila solution for interest of mother tanzania.Haoni kuwa alifanya hivyo na wao wakapata greenlight ya kutumia mahakama kutaka fidia?
Mwingine ni Mwakyembe na timu yake watuambia waliyofich Kulinda heshima ya serikali na sio taifa na kumwogopa Mungu ni yapi? Hivi serikali gani yenye hesima kuliko umma? Heshima hiyo imetoka wapi? Serikali itapita lakini taifa alipiti.Wana deni hawa maana wasingefanya filtering on what to report huenda kesi ya Dowans huko ICC isingepata nguvu.
Tuungane kulazimisha majibu na suluhu yenye manufaa kwa taifa na liwe ni fundisho kwa serikali zijazo. Mungu atutangulie wote wenye mapenzi mema na nchi