Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Hiyo hotuba tayari Absolom Kibanda alishamwandikia kwenye gazeti la leo la Tanzania Daima, for me there is nothing new than wasting our energy & time. am out on this thread.
 
Yaani aliwaita waandishi na vyombo vyao kuvionya tu na kutishia kuvichukulia hatua kwa "kumchafua?" Kweli mvi siyo busara -- kwake zimekuwa kama uchuro tu.

WHAT A SHAME!!!
 
Nimekubali msemo wake kuwa yeye na rais hawakukutana barabarani. Kwa hiyo urafiki mbele au kwanza watanzania na matatizo yao shauri yao
pili kumbe ikulu kunaendeka tu? na kweli hawa wawili wananufaika na matatizo yetu

Ni kweli mkuu. Mtu hayuko tayari kukubali kuwa alifanya makosa kwa umma. Tunahitaji mapinduzi ya kifikra na mfumo mzima wa utumishi wa umma.
 
Na hapo mwisho anapotaja changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa -- hivi kimakusudi tu, au kwa kapitiwa -- kuacha kuitaja ile changamoto Namba 1 yaani UFISADI?
 
Lowassa Press conference has done nothing but reignite controvecy surrounding him. He would have been well adviced to( as Ole Ntimama said the other day) lay low like an envelope.
 
salma kwa hili la leo huyu jamaa lazima apakwe matope ..anacheza na akili za watu..aache ujinga kabisa na ajue kuwa kuna watu tunamfaham vizuri tu....na leo ameamua kupindisha ukweli..ameona aibu kuwaambia wandishi wa habari dakika za mwisho kuwa hawezi kuongea nao ila akaona ni heri apoteze mda kwa kuongea ushenzi....nimeomba mwongozo kwa mod bado kimya


Mkuu uwezo wake umeishia hapo unakumbuka aliwai shidwa kumjibu mwanafunzi uelewa wasasa nimkubwa vingozi wetu wengi uwezo wao nifinyu haiingii akilini alicho kiongea kuwasumbuwa waandishi watu wamesitisha kazi kufuatilia nini atatamuka kumbe upupu wengi wamefilisika kisiasa
 
Mkuu uwezo wake umeishia hapo unakumbuka aliwai shidwa kumjibu mwanafunzi uelewa wasasa nimkubwa vingozi wetu wengi uwezo wao nifinyu haiingii akilini alicho kiongea kuwasumbuwa waandishi watu wamesitisha kazi kufuatilia nini atatamuka kumbe upupu wengi wamefilisika kisiasa



yle dogo wa ukerewe nakumbuka sana maana siku hiyo alivyonuna
 
Ndugu Dark City,naona EL na yeye ameshindwa kuchukua maamuzi magumu.

Naomba nitofautiane na wewe...EL keshachukua uamuzi mgumu sana labda kama watu hawauoni.

Hivi ni rahisi mtu kuvuta trigger ya silaha iliyokulenga kwenye paji lako la uso???? Sasa EL keshaanza taratibu kuivuta!
 
Mkuu uwezo wake umeishia hapo unakumbuka aliwai shidwa kumjibu mwanafunzi uelewa wasasa nimkubwa vingozi wetu wengi uwezo wao nifinyu haiingii akilini alicho kiongea kuwasumbuwa waandishi watu wamesitisha kazi kufuatilia nini atatamuka kumbe upupu wengi wamefilisika kisiasa

Na hajui kwamba kwa uelewa wao wa mambo mengi tu, waandishi sasa hivi wako hatua moja mbele ya wanasiasa. Hivyo wanasiasa ndiyo kila mara wanajikuta katika hali ya kutaka kujikosha mbele ya waandishi, kuwatisha au hata kuwahonga.

The press is always ahead!
 
Na hajui kwamba kwa uelewa wao wa mambo mengi tu, waandishi sasa hivi wako hatua moja mbele ya wanasiasa. Hivyo wanasiasa ndiyo kila mara wanajikuta katika hali ya kutaka kujikosha mbele ya waandishi, kuwatisha au hata kuwahonga.

The press is always ahead!

Yeah! Press ndiyo kwa kiasi kikubwa zina-set agenda za wanasiasa!
 
Naunga mkono aliyoyaongea na style yake presentation maana mkutano au press cenference ameitisha yeye. Kama aliyosema siyo yale tuliotaka kusikia hatna haja ya kuyajadili na message will be sent to him.Lakini kama audience constituting waandihi wa habari na wengine walimsikiliza na kuuliza maswali na kusikia ambayo hawakurataji walikuwa na options kadhaa. Wangeondoka immediately after he had stated his position that questions be in the context of what he had presented. Basi angegoma zaidi wangenyanyuka na kuondoka kabisa huku wakimwacha ameduwaa. Pili Watanzania lazima tuwe serious na yale tunayotaka kusikia na kutoka kwa nani.

Haingii akilini kwamba mtanzania sensible alitaka EL afanye kama Wakatholiki ndani ya confession box kuwa nilikosa eno kadha wa kadha. EL kama ilivyo JK are both birds of the same feather na historia itakuja kusema.Tusiwe wasaarifu. Waliposhika madaraka kila zuri mfano amani na utulivu, mshikmano, hazina ya fedha za kigeni $3b, miundo mbinu ya barabara, uwanja mpya wa taifa, viwanda vichache vilivyobinafsishwa na kuendelea kuzalisha walivifanya kama ni mafanikio yao wala si ya chama au serikali zilizopita. Ilikwa ni nadra Mkapa na Nyerere kutajwa kwenye mazuri hayo labda Mzee Mwinyi peke. Kumbuka mpaka Mkapa alianza kuzomewa na watu kama ambaye hakuwahi kufanya jema lolote.

Lakini penye matatizo kama ukame, njaa, ukosefu wa umeme, mikataba mibovu ya madini, radar ya ndege na mengine hayo yalifanywa kuwa ni urithi mbaya wa wa serikali zilizopita. Sasa mtu ambaye alizoea propaganda za namna hii mnamtaka leo asimame ajipige kifua aseme nilikosa. Watu wa kukubali makosa na kusema yalifanywa kwa ubinadamu na kutoa wito wa kujirekebisha walikuwa ni kina Kambarage, Kaduma, Warioba na wengine lakini bahati mbaya Mwalimu ashatangulia mbele ya haki na waliokuwa hai badohawako ktk vyombo vya kimaamuzi.

Majibu sahii ya nini kijiri Richmond/Dowans na sasa Syombion anayo JK kama Rais maana anavyo vyombo vya kumsaidia kujua japo ashasema hajui. Polisi, usalama wa taifa, jeshi, PCCB, Tume ya maadili na ofisi ya rais.Sasa kuendelea kujificha chini ya kivuli cha siwajui ni kujidhalilisha na kuwatusi watanzania. Richmond/Dowans wamekuwa wakilipwa bilions of shs, sasa were we paying the ghosts? JK atuambie kuhusu haya na EL ambaye yuko nje ya vyombo vya maamuzi na kwa kuwa kuna vyombo vingi chini yake Rais jibu litakalotoka hapo tutajua pumba zipi na mchele upi. Lakini itoshe kusema yeye ndiye aliyebariki mitambo ya dowans wapewe symbion na kuzalisha umeme.sasa jiulize utaruhusu kitu cha mtu usiyemjua anunue mtu mwingine? kama ni hivyo hamna maana ya kuwa na mtu kama huyu as rais na vyombo hivi vikienedelea kuripoti kwa wahusika wanahitaji kupimwa.

Majibu mengine ya Richmond/Dowans anayo Sitta Samweli aliyekwa spika wakati huo. Alianzisha mchakato wa kuipeleleza richmond/dowans na ripoti kutolewa na jinsi alivyozima mjadala huo ni ishara ya kifisadi. Huwezi kuanzisha jambo leneye gharama in terms of perdiem kwa wajumbe na na nauli ya kwenda na kurudi nje ya nchi na muda mwingi wa bunge kuongelea swala hilo halafu ukalizima bila majibu na utarajie watu wakuenzi hapana. Ssita asipojitokeza waziwazi na kusema tutasema aliutaka uwaziri mkuu wa EL.Haitoshi kusema wasilipwe, ni wahuni, ni mkataba batili... Hayo kila mtanzania mwenye akili alishajua.Tuanataka atwambie sababu ya kuzima mjadala bila solution for interest of mother tanzania.Haoni kuwa alifanya hivyo na wao wakapata greenlight ya kutumia mahakama kutaka fidia?

Mwingine ni Mwakyembe na timu yake watuambia waliyofich Kulinda heshima ya serikali na sio taifa na kumwogopa Mungu ni yapi? Hivi serikali gani yenye hesima kuliko umma? Heshima hiyo imetoka wapi? Serikali itapita lakini taifa alipiti.Wana deni hawa maana wasingefanya filtering on what to report huenda kesi ya Dowans huko ICC isingepata nguvu.

Tuungane kulazimisha majibu na suluhu yenye manufaa kwa taifa na liwe ni fundisho kwa serikali zijazo. Mungu atutangulie wote wenye mapenzi mema na nchi
 
Nimepoteza muda wangu kukodolea macho thread hii tangu page ya kwanza hadi ya mwisho. Ninachoona hapa ni uharo ule ule wa kimagamba. Hakuna jipya
 
Kuhusu hoja ya kujenga viwanda na hasa domestic industries hilo halina ubishi.Ni hoja nzito ambayo tumekuwa tukiipigia kelele kila siku.Hata hivyo alipokuwa waziri mkuu hakufanya hayo

Pia kitu ambacho nimegundua,mkakati wake mkubwa ni kupata attention ya vvoters block ambayo mtaji wake mkubwa ni vijana.Ni lazima sasa tujipange sawasawa kwa sababu huyu jamaa anatafuta fursa ya kujiweka karibu zaidi na vijana.

Pia amejionyesha ni mtu wa mikakati kwa sababu hajataka kuongelea mambo sensitive ambayo yangekuwa ni suicide pact.ameyaacha strategically pengine kutokana na kikao kijacho cha NEC.Hataki ku-twist rebellion intuition waliyo nayo wajumbe wa NEC. He he Heeee! CCM mnayo kazi,mkitoka hapo mtakutana uso kwa uso na radical movement ya chadema na vijana!
 
Tunakusiliza mwenye maamlaka ya juu humu JF
Wakuu,

Muda si mrefu tutaweza kwenda Live kutokea Monduli ambapo Mhe. Lowassa (Waziri Mkuu aliyejiuzulu) atakapoongea na vyombo vya habari. Tumefanikiwa kupenyeza mtu hivyo tutaweza kuwaletea alichoongea. Nita-update 1st post kulingana na atakavyokuwa anaongea.

Shukrani

=================

  • Mwandishi wetu kamsisitizia kuwa watu wamesisitiza wanataka kujua kauli yake juu ya Richmond/Dowans/Symbio na suala la kujivua gamba ndani ya CCM, vinginevyo mkutano huu hautakuwa na maana na watu wanahisi labda umetishwa. Kajibu kuwa masuala haya atayazungumzia lakini leo si wakati muafaka, kuna wakati atayazungumzia.
  • Mwandishi kamwuliza kama ametishwa, maana anaonekana kila la muhimu hataki kuongelea, kajibu kirahisi tu "SINTOJIBU MASWALI HAYO"
  • Mwandishi wetu pia kamwuliza juu ya 'Uvuaji Gamba', nalo kakataa katakata kuongelea, kasema si wakati muafaka.
  • Pamoja na mwandishi wetu kumweleza umuhimu wa yeye kuongelea suala la DOWANS/Richmond kakataa katakata na kusema ataliongelea wakati muafaka na si leo.
  • Wakuu... Kamaliza! Ila kamalizia na "I think this is enough for your stomach" sasa sijaelewa anamaanisha alichoongea au ......?
  • Juu ya DOWANS: Kaulizwa itakuwaje asihusishwe kwenye mjadala huo ilhali kuna watu ndani ya CCM wameshasema waliojiuzulu ndo walipe? Kasema SINA MUDA WA KUJIBU SWALI HILO!
  • Juu ya urais 2015: Hata mimi nashangaa, miaka bado sana, kwanini tuanze kuongelea urais wa 2015? Waandishi acheni propaganda, msipoandika chokochoko hizi hakuna atakayehangaika nazo.
  • Mitikisiko ndani ya CCM ni ya muda tu, tutapita katika hali hii.
  • MAJIBU: Si kama napuuza jitihada za serikali juu ya suala la ajira kwa vijana, lakini hali ni mbaya sana. Nashauri tuvunje kanuni, serikali ikope fedha na ijenge viwanda tuweze kuwaajiri watanzania wengi. Fedha zipo!
  • Moses Mashalo kauliza juu ya mustakabali wa CCM kwa siku zijazo kufuatia hali inayoendelea kwa sasa ndani ya CCM.
  • KAMALIZA... Maswali yanafuata
  • Uchumi wa dunia upo taabani, taifa letu linakabiliwa na hali mbaya. Shilingi yetu inazidi kuporomoka vibaya. Inflation inazidi kuelekea kubaya zaidi. Kuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kubwa sana. Vijana wakiishi katika hali hii tutakuwa tumekalia bomu la muda na itapelekea kuvunjika kwa amani. Ni vyema tukatafuta suluhu ya mambo haya.
  • Naomba vyombo vya habari tusaidie nchi yetu. Tunapoandika propaganda za chuki kwa nia ya 'kulipuana' tujue tunalipeleka taifa kubaya.
  • Sasa niseme rasmi, IMETOSHA. Sintoendelea kuvumilia kuchafuliwa na vyombo vya habari. Nitachukua hatua kali dhidi ya magazeti yatakayonichafua na vyombo vya habari vyote vinavyonichafua. Ukinichafua nitakupeleka kwenye vyombo husika na niseme uhuru usio na nidhami ni fujo. Uhuru wa vyombo vya habari umekuwa 'abused' sana.
  • Vijana mara nyingi ni radical, wasibezwe na wasilaumiwe kwa wanachofanya bali waelekezwe. Anayekiuka sheria asifumbiwe macho.
  • Vijana wa UVCCM tusiwaingilie, ni taasisi muhimu kwa ajili ya chama chochote cha siasa.
  • Sheria ni sheria, hakuna aliye juu ya sheria. Kama kuna sheria inavunjwa hakuna anayetakiwa kuangaliwa tu.
  • Gazeti flani linaloniandama lilishafikia hatua ya kusema ndo nahusika na maasi ya vijana wa UVCCM, ni uwongo na wala sihusiki kwa namna yoyote na vijana wa Arusha. Nilikuwa nje kwa matibabu, ningejuaje nini wanapanga vijana?
  • Sijakutana na rais Kikwete barabarani, waache kunichonganisha naye na waache kunichafua mbele za watanzania. Walishasema eti nagombea urais mwaka 2010. Naamini hata rais Kikwete anajua kuwa huu ni uzushi tu.
  • Masuala ya Chama huwa yanaishia kwenye vikao, hii ya kubomoana nje ya vikao hayana maana. Siwezi kukihujumu chama changu mwenyewe.
  • Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu.
  • Toka nilipojiuzulu uwaziri mkuu nilikaa kimya, kimya ni hekima toka kwa Mwenyezi Mungu
  • Anaomba kutoulizwa maswali ambayo ni nje ya hoja anayoongelea.
  • Anaanza kuongea sasa...
  • Alishakaa ili aanze kuongea, kaondoka na inaelekea kama kuna jambo anaenda kuliweka sawa kwanza.
  • Ilitarajiwa angeanza saa 4 kamili lakini inaelekea ataanza saa 4 unusu, waandishi wapo wengi. Atajivua gamba?
=============
UPDATE
=============
Full text ya alichozungumza Lowasa


View attachment 39445 View attachment 39447 View attachment 39448 View attachment 39449 View attachment 39450
 
Gamba au si gamba Mh Lowasa kama mtanzania ana haki ya kupiga au kupigiwa kura. Mpaka hapo haki hiyo itakapobatilishwa na mahakama au vikao husika vya chama chake hatupaswi kumuhukumu humu jamvini. Na hata chama chake kikimkatalia nna uhakika katiba mpya itampatia haki hiyo kupitia mgombea binafsi
 
invisible nakuomba ukae uipangilie vizuri hii habari coz haina mwanzo kati na mwisho.au kwasababu ameshamaliza kuongoa mwambie wa jikoni akupe copy ya aliyoyasema naamini kawagawia copy.over
Invisible aliyeshasema ile ni update tu na kwa mpangilio usubiri kesho kwenye magazeti
 
Back
Top Bottom