Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

tumechoka na siasa uchwara za CCM na kuona kuna haja ya kuona kuwa wote ndio walitia taifa letu hasara hivyo hakuna atakayetoka hapa kwa mambo yao ya ajabu kama haya
 
yale mabilioni ya JK yakowapi jamani huyu jamaa ni mchumi ila huwa napatwa na shaka sana kuwa vitu anafanya katika Tanzania ni shida kujua kama kweli anaweza kwenda na kujidai eti kuna maendelea
 
Mz. Mamvi weka wazi! Wambie tu utagombea u-presidaa! Kwvl tunaokuhitaji tupo wengi, hakuna haja y kufichaficha! Hii c biashara y heroine!
 
Ila mti mzima mwishoni kamuachia vipande vyake mkuu wa nchi, haya matatizo ndio hasa wanananchi wa Tanzania tunahitaji mkombozi wake.

Wakuu,

Muda si mrefu tutaweza kwenda Live kutokea Monduli ambapo Mhe. Lowassa (Waziri Mkuu aliyejiuzulu) atakapoongea na vyombo vya habari. Tumefanikiwa kupenyeza mtu hivyo tutaweza kuwaletea alichoongea. Nita-update 1st post kulingana na atakavyokuwa anaongea.

Shukrani

=================
  • Mwandishi wetu kamsisitizia kuwa watu wamesisitiza wanataka kujua kauli yake juu ya Richmond/Dowans/Symbio na suala la kujivua gamba ndani ya CCM, vinginevyo mkutano huu hautakuwa na maana na watu wanahisi labda umetishwa. Kajibu kuwa masuala haya atayazungumzia lakini leo si wakati muafaka, kuna wakati atayazungumzia.
  • Mwandishi kamwuliza kama ametishwa, maana anaonekana kila la muhimu hataki kuongelea, kajibu kirahisi tu "SINTOJIBU MASWALI HAYO"
  • Mwandishi wetu pia kamwuliza juu ya 'Uvuaji Gamba', nalo kakataa katakata kuongelea, kasema si wakati muafaka.
  • Pamoja na mwandishi wetu kumweleza umuhimu wa yeye kuongelea suala la DOWANS/Richmond kakataa katakata na kusema ataliongelea wakati muafaka na si leo.
  • Wakuu... Kamaliza! Ila kamalizia na "I think this is enough for your stomach" sasa sijaelewa anamaanisha alichoongea au ......?
  • Juu ya DOWANS: Kaulizwa itakuwaje asihusishwe kwenye mjadala huo ilhali kuna watu ndani ya CCM wameshasema waliojiuzulu ndo walipe? Kasema SINA MUDA WA KUJIBU SWALI HILO!
  • Juu ya urais 2015: Hata mimi nashangaa, miaka bado sana, kwanini tuanze kuongelea urais wa 2015? Waandishi acheni propaganda, msipoandika chokochoko hizi hakuna atakayehangaika nazo.
  • Mitikisiko ndani ya CCM ni ya muda tu, tutapita katika hali hii.
  • MAJIBU: Si kama napuuza jitihada za serikali juu ya suala la ajira kwa vijana, lakini hali ni mbaya sana. Nashauri tuvunje kanuni, serikali ikope fedha na ijenge viwanda tuweze kuwaajiri watanzania wengi. Fedha zipo!
  • Moses Mashalo kauliza juu ya mustakabali wa CCM kwa siku zijazo kufuatia hali inayoendelea kwa sasa ndani ya CCM.
  • KAMALIZA... Maswali yanafuata
  • Uchumi wa dunia upo taabani, taifa letu linakabiliwa na hali mbaya. Shilingi yetu inazidi kuporomoka vibaya. Inflation inazidi kuelekea kubaya zaidi. Kuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kubwa sana. Vijana wakiishi katika hali hii tutakuwa tumekalia bomu la muda na itapelekea kuvunjika kwa amani. Ni vyema tukatafuta suluhu ya mambo haya.
  • Naomba vyombo vya habari tusaidie nchi yetu. Tunapoandika propaganda za chuki kwa nia ya 'kulipuana' tujue tunalipeleka taifa kubaya.
  • Sasa niseme rasmi, IMETOSHA. Sintoendelea kuvumilia kuchafuliwa na vyombo vya habari. Nitachukua hatua kali dhidi ya magazeti yatakayonichafua na vyombo vya habari vyote vinavyonichafua. Ukinichafua nitakupeleka kwenye vyombo husika na niseme uhuru usio na nidhami ni fujo. Uhuru wa vyombo vya habari umekuwa 'abused' sana.
  • Vijana mara nyingi ni radical, wasibezwe na wasilaumiwe kwa wanachofanya bali waelekezwe. Anayekiuka sheria asifumbiwe macho.
  • Vijana wa UVCCM tusiwaingilie, ni taasisi muhimu kwa ajili ya chama chochote cha siasa.
  • Sheria ni sheria, hakuna aliye juu ya sheria. Kama kuna sheria inavunjwa hakuna anayetakiwa kuangaliwa tu.
  • Gazeti flani linaloniandama lilishafikia hatua ya kusema ndo nahusika na maasi ya vijana wa UVCCM, ni uwongo na wala sihusiki kwa namna yoyote na vijana wa Arusha. Nilikuwa nje kwa matibabu, ningejuaje nini wanapanga vijana?
  • Sijakutana na rais Kikwete barabarani, waache kunichonganisha naye na waache kunichafua mbele za watanzania. Walishasema eti nagombea urais mwaka 2010. Naamini hata rais Kikwete anajua kuwa huu ni uzushi tu.
  • Masuala ya Chama huwa yanaishia kwenye vikao, hii ya kubomoana nje ya vikao hayana maana. Siwezi kukihujumu chama changu mwenyewe.
  • Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu.
  • Toka nilipojiuzulu uwaziri mkuu nilikaa kimya, kimya ni hekima toka kwa Mwenyezi Mungu
  • Anaomba kutoulizwa maswali ambayo ni nje ya hoja anayoongelea.
  • Anaanza kuongea sasa...
  • Alishakaa ili aanze kuongea, kaondoka na inaelekea kama kuna jambo anaenda kuliweka sawa kwanza.
  • Ilitarajiwa angeanza saa 4 kamili lakini inaelekea ataanza saa 4 unusu, waandishi wapo wengi. Atajivua gamba?
=============
UPDATE
=============
Full text ya alichozungumza Lowasa


View attachment 39445 View attachment 39447 View attachment 39448 View attachment 39449 View attachment 39450
 
Kweli Magamba wanasiasa wote ni CRAP!!!!!!!! Unaita watu Monduli kuongea hayo, bora hilo la kujenga viwanda mengine yote ni pumbaaa:shock:
 
Marehemu Mzee Nyerere alishamkataa wazi wazi huyo Lowassa mnaempigia chapuo.
ni kupoteza muda tu kumjadili
 
There are currently 1065 users browsing this thread. (201 members and 864 guests)

Wakuu mchango wangu kwenye hii thread ni idadi ya users inatisha mweehe
.
 
halafu hilo la kujenga viwanda ni unafiki wa kushindwa kwa sera zao za kufikiri unaweza kubinafsisha kila kitu wakati foundation yetu kwa mambo hayo bado?

Mfano kama kutoe hela tume toa kwa Rites zimekwenda chini ya uongozi wake, kwenye umeme vivyo hivyo tumetoa mamilioni na umeme hatuna. chini ya uongozi wake na ndio maana akajiuzulu , sasa hapa kama alimbebea mizigo rafiki ni udhaifu wake.

Sasa baada ya kututia hasara yote hiyo ndio anakuja na theory hiyo hiyo kwamba serikali iweke fedha zake kuleta ajira inaweza kuwa sawa lakini pia anatakiwa kuelewa kwanini watu toka nje au ndani wanashimdwa kuwekeza kuleta hizo ajira, ni umeme na barabara.

Jana kulikuwa na taarifa kuhusu bei ya saruji ya Tanzania kuwa aghali kuliko ya Pakistan na hata gharama za uchukuzi toka pakistan mpaka tanzania ni nafuu, kuliko gharama za kusafirisha toka sema dsm kwenda baadhi ya mikoa, sasa hata hivyo viwanda vikijengwa vitaendeshwa kwa umeme upi? au ana mpango wa kufungua dowans/richmond nyingine.
 
Nadhani umempa ushauri mzuri, lakini tueleze una mshauri nani endeleze siasa: mod, inv, painkiller, joka kuu, Riz1, malecela, membe au wewe mwenyewe?.
Ninge.mshauri Lowas aachane na politics afanye biashara hii itamuumiza akili tu
 
Huku mzee wa Mtama huku mzee wa Urambo huku mzee wa Monduli, kazi kweli kweli kama gloves wasivae za Kichina
 
Sio suala la HAKI hapa
jibu swali kama linavyouliza
umekurupuka kujibu
ndio maana mnafeli mitihani nyie
swali:1.atakubali matokeo?
2.atakuwa tayari kufanya kazi na mahasimu wake?(wapambanaji wa ccm)
 
Tunashukuru kwa taarifa mkuu...ila nimpongeze EL kwa kuongea na waandishi wa habari..nadhani alichokuwa nacho ndo hicho watz 2mekisikia ingawa tulikuwa na mengi ya kukuuliza lkn umesema utayapatia muda wake...wacha tusubiri.. hongera kwa haya machache. Barikiwa sana.
 
wakati wakihofia mali zao kupotea kwa machafuko ndio wanajua taifa litaangamia ili hali watanzania wa kawaida tayari tumeangamizwa. we have nothing to loose. we walking dead! laughing like zombie, smiling like rotten monkeys! ahamishe mali zake kwani hakujua tanzania itaangamia alipokuwa anafanya maamuzi ya kitapeli na boss wake?
 
Back
Top Bottom