makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wana JF,
Hawa jamaa wawili JK na EL wanajuana vizuri sana. Kumbukeni enzi zao za ''BOYS 2 MEN''!!!!
Kila kitu kiko wazi. EL na JK wanajaribu kucheza na akili za Watanzania kwa kufanya The Comedy Show. Hawa watu 2 watatusumbua sana huko tunakoenda. Mkutano wa jana ilikuwa ni gheresha tu na kuvuta masikio ya Wadanganyika!
Watu tulikuwa tuko roho juu kwamba pengine EL angechukua maamuzi magumu kama alivyodai Bungeni juzi kwa kufuata nyayo za rafiki yake RA wa Igunga. Lakini waaapi!!! Huo ubavu wa kuchukua MAAMUZI MAGUMU ANAO???Kwanza JK alishamwambia yeye atulize bori maana hakuna kitakachomtokea yeye na AC kuhusiana na KUJIVUA GAMBA. EL na AC wataendelea kupeta ndani ya Chama Cha Magamba. Kelele za Vuvuzela Nape ni danganya toto!!!
Yale yale ya RA. Kwamba unajivua gamba halafu kesho CCM hao hao wanakuja kuomba UWAFADHILI NA UWASAIDIE KUPIGA KURA! Hakuna cha kuvuana gamba baali ni usanii wa CCM wa kucheza na akili za Wadanganyika.
Kuna ASKOFU au Mchungaji wa Kanisa moja pale Dar aliwahi kutamka mwaka huu kwamba: LOWASSA ASIPOKUWA RAIS MWAKA 2015 MNIUE! Hizo habari ziliandikwa na magazeti mengi sana na sikumsikia EL akikanusha habari hizo. Hivi karibuni EL ameonekana akienda kwa Nabii Joshua wa Kanisa la Emmanuel huko Nigeria. Watu wamemwona kupitia kwenye Runinga ya Emmanuel TV akiombewa mara mbili. Habari za kuaminika ni kwamba HAYO NI MAANDALIZI YA URAIS MWAKA 2015! Rejea taarifa ya Askofu hapo juu.
Nihitimishe kwa kusema kuwa Kiwete na Lowassa wanajua kabisa nini wanakifanya ndani ya CCM na UVCCM. Kumbukeni kauli za EL kuwa yeye na JK hawajakutana barabarani. Kumbukeni walivyochukua Fomu za Kugombea Urais kwa mbwembwe mwaka 2005 na kufuatia uundaji wa Serikali ya JK 2005. Kumbukeni baada ya EL kujiuzulu Uwaziri Mkuu mwaka 2008 JK alitamka nini! Kwamba kilichompata rafiki yake EL ni ajali ya kisiasa.
Wazungu wanasema kuwa,''BIRDS OF THE SAME FEATHER FLOCK TOGETHER''. Kiwete na Lowassa hakuna wa kuwatenganisha.Hakuna cha UVCCM,hakuna cha Nape wala hakuna cha SS. Ni lazima EL aukwae Urahisi mwaka 2015!!!!