Lowassa chanzo cha matokeo mabaya kidato cha nne.

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
3,541
Reaction score
2,187
Edward Lowassa yule nguli wa siasa mwenye tuuma za kutosha na anayeendelea kusakamwa kila kukicha, kama vile Richmond, Dowans, vile vile jana tu kahusishwa na mgomo wa madaktari, Wabunge wa CCM kumgomea Mwenyekiti wao! Mara tatizo Uwaziri Mkuu, Mara kamlisha jamaa fulani Sumu. Sasa hii kali, kwa nini tusimtwishe na zigo la kufeli kwa watoto wa kidato cha nne, maana yeye ndo chanzo cha kujenga shule za kata zisizokuwa na walimu, maana kabla ya kuzijenga angetengeneza sera imara ya kuwa na walimu wa kutosha, sasa kutokana na ubabe wake akang'ang'ania kuzijenga bila ya kupeleka walimu na madhara yake ndo haya ya kina " MWANAASHA" a.k.a KILAZA, na hapo hakusoma shule ya Kata. Sasa mnaonaje tumtwishe Hili zigo Mzee LOWASSA maana ndo zake kubeba Mizigo isiyokuwa ya kwake Mfano Richmond?

Note: MWANAASHA means KILAZA au MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI

Ni mawazo yangu tu wala msinitukane changia kwa ustaharabu.
 
we acha matatizo kwani amefeli peke yake tz acha chuki binafsi kwa raisi wako jirekebishe dont judge anyone as you are not perfect
 
OMG...!! Hii kali kuliko zote.!
 
we acha matatizo kwani amefeli peke yake tz acha chuki binafsi kwa raisi wako jirekebishe dont judge anyone as you are not perfect

Chuki gani kwani si kafeli au? Watoto wa kata wangekuwa wanapata huduma kama yeye unadhani wangefanya huu upuuzi?
 
huyu mtoto ataathirika kisaikolojia sasa hivi hebu muacheni jamani.sasa hapa title lowassa lakini message mwanaasha!khaa muoneeni huruma jamani
 
Chuki gani kwani si kafeli au? Watoto wa kata wangekuwa wanapata huduma kama yeye unadhani wangefanya huu upuuzi?

haya bwana sasa kama kafeli we ndo ulimlipia ada kuna mambo mengi ya kuongelea humu sio kusema watu individualy think big acha majungu
 
Hukumu ya haraka huonea! Fikiria kiwango cha Elimu na mitaala ya siku za nyuma, walimu wa wakati huo na sasa!
mazingira ya utoaji elimu, rasilimali vifaa, Rasilimali fedha, wingi wa watu, na kizazi hiki! UTAPATA JIBU! SI HILI LAKO!
 
Sijakusoma kaka ebu fafanua
 
Edward Lowassa yule nguli wa siasa mwenye tuuma za kutosha na anayeendelea kusakamwa kila kukicha, kama vile Richmond, Dowans, vile vile jana tu kahusishwa na mgomo wa madaktari, Wabunge wa CCM kumgomea Mwenyekiti wao! Mara tatizo Uwaziri Mkuu, Mara kamlisha jamaa fulani Sumu. Sasa hii kali, kwa nini tusimtwishe na zigo la kufeli kwa watoto wa kidato cha nne, maana yeye ndo chanzo cha kujenga shule za kata zisizokuwa na walimu, maana kabla ya kuzijenga angetengeneza sera imara ya kuwa na walimu wa kutosha, sasa kutokana na ubabe wake akang'ang'ania kuzijenga bila ya kupeleka walimu na madhara yake ndo haya ya kina " MWANAASHA" a.k.a KILAZA, na hapo hakusoma shule ya Kata. Sasa mnaonaje tumtwishe Hili zigo Mzee LOWASSA maana ndo zake kubeba Mizigo isiyokuwa ya kwake Mfano Richmond?

Note: MWANAASHA means KILAZA au MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI

Ni mawazo yangu tu wala msinitukane changia kwa ustaharabu.
Hapo kwenye red
1.Nchi hii walimu wa kutosha wapo isipokuwa serikali haiwahitaji,kwani haiwajali.Kwa nini kusiwe na upungufu wa watumishi huko TRA,BOT,NSSF,PPF,n.k.?
2.Huyo mwanaasha alisoma shule iliyojaa kitu lakini bado amefeli ila amefaulu kwa mujibu wa serikali kwani ana div.4
 
Haya ndio matokeo ya kuingiza ushabiki wa kisiasa kwenye mambo ya kitaalamu.
 
Back
Top Bottom