Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,541
- 2,187
Edward Lowassa yule nguli wa siasa mwenye tuuma za kutosha na anayeendelea kusakamwa kila kukicha, kama vile Richmond, Dowans, vile vile jana tu kahusishwa na mgomo wa madaktari, Wabunge wa CCM kumgomea Mwenyekiti wao! Mara tatizo Uwaziri Mkuu, Mara kamlisha jamaa fulani Sumu. Sasa hii kali, kwa nini tusimtwishe na zigo la kufeli kwa watoto wa kidato cha nne, maana yeye ndo chanzo cha kujenga shule za kata zisizokuwa na walimu, maana kabla ya kuzijenga angetengeneza sera imara ya kuwa na walimu wa kutosha, sasa kutokana na ubabe wake akang'ang'ania kuzijenga bila ya kupeleka walimu na madhara yake ndo haya ya kina " MWANAASHA" a.k.a KILAZA, na hapo hakusoma shule ya Kata. Sasa mnaonaje tumtwishe Hili zigo Mzee LOWASSA maana ndo zake kubeba Mizigo isiyokuwa ya kwake Mfano Richmond?
Note: MWANAASHA means KILAZA au MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI
Ni mawazo yangu tu wala msinitukane changia kwa ustaharabu.
Note: MWANAASHA means KILAZA au MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI
Ni mawazo yangu tu wala msinitukane changia kwa ustaharabu.